Urusi vs Wagner: Wagner wasitisha 'Uasi' na safari ya kwenda Moscow yasitishwa, wadai hawataki kumwaga damu ya Warusi

Urusi vs Wagner: Wagner wasitisha 'Uasi' na safari ya kwenda Moscow yasitishwa, wadai hawataki kumwaga damu ya Warusi

Magari ya Deraya/Armoured vehicles yaonekana mitaa ya Rostov Oblast, Russia baada ya tamko la kutangazwa kwa vita Dhidi ya Urusi la kiongozi wa Wagner mercenaries:
Mytake: Putin haaminiki hata na washirika pamoja na wananchi wake.
Lukashenko amekimbilia Uturuki, Medvedev na familia yake wamekuwa evacuated kutoka Moscow, Putini ameelekea St Petersburg na wanajeshi wengi wa Urusi wanaungana na Wegner tuendelee kula mtori nyama zipo chini;

Ila imekuwa ghafla sana tofauti na matazamio.So sad
 
Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imeonya kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa hatari ya machafuko kote nchini Urusi, Taarifa ya London inakuja wakati huu pia ikitoa tahadhari kwa wasafiri baada ya Kundi la Wagner kudaiwa kuteka baadhi ya maeneo nchini Urusi.

Serikali ya Uingereza iliendelea kushauri dhidi ya safari zote kwenda Urusi.
Hapo sasa ndipo Putin watamkumbuka UK
 
Helikopta za kijeshi za Urusi zimeufyatulia risasi msafara wa mamluki wa Wagner ambao tayari umekaribia nusu ya njia kuelekea Moscow, shirika la habari la Reuters liliripoti, hatua inayokuja baada ya mamluki hao kuuteka mji wa kusini wa Rostov-on-Don.

Mwandishi wa habari wa Reuters aliona helikopta za jeshi zikifyatua risasi kwenye msafara wa Wagner wenye silaha uliyokuwa ukipita katika mji wa Voronezh.
 
Tuliwaambia humu Urusi ni Supa-pawa wa mchongo mkabisha, jioneeni sasa hii aibu...

Kichuguu
Unajua tofauti ni kwenye institutions. Marekani haindeshwi kwa amri ya rais bali wanafuata institutions zilizopo kikatiba. Ila Urusi na nadhani hata China wao wanafuata amri ya rais; hapo ndipo tofauti ilipo. Kwa marekani Rais akipata kikohozi, nchi bado itaendelea, lakini kwa Urusi na China rais akipata kikohozi basi nchi yote nayo inapata kikohozi.
 
Lukashenko amekimbilia Uturuki, Medvedev na familia yake wamekuwa evacuated kutoka Moscow, Putini ameelekea St Petersburg na wanajeshi wengi wa Urusi wanaungana na Wegner tuendelee kula mtori nyama zipo chini;

Ila imekuwa ghafla sana tofauti na matazamio.So sad
Lukashenko nini kinamkimbiza wakati nchi yake haina vita? Huyu ni kibaraka wa Putin, tena Jeshi lilipaswa kumwambia asirudi nchini humo.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom