USA vs China: Nchi ipi ina miji mizuri zaidi?

USA vs China: Nchi ipi ina miji mizuri zaidi?

Wachina wenyewe wanaota ndoto kuhusu marekani, kwa mwaka watu laki mbili kutoka china uenda marekani kusoma, ukiangalia miji ya kichina ni kama artificial vile
Kwa mengine lakini linapokuja suala la miji, Marekani haigusi kwa China.
 
Miji mizuri ipo Ulaya. Usalama, usafi wa mazingira(Hasa hewa), usafiri wa umma na huduma za kijamii.
 
Suppose una degree zako na experience ya kazi nchini kwako then baadae unaanza kutafuta opportunities nchi za nje
Iwe ni Mechanical Engineer, mwalimu, mhasibu, mbeba maboksi, mwosha magari au kazi yoyote ni rahisi kupata ajira Marekani kuliko China
China hata kupata citizenship ni Impossible
Upo sahihi sema life pia ni mtu mwenyewe umeandaliwaje kwenye hii Dunia maana hapo USA usidhani ni rahisi tu kuishi na ku save..
 
Wazee nendeni hata Hong Kong hapo Watanzania tunaingia bila visa ni nauli yako tu uone bara bara za chini ya bahari,tren na matakataka mengine jiji safi utadhani ndani uwanja wa ndege wao umehengwa baharini wale jamaa vichwa vyao vipo sawa sana..
Singapore ni visa pia ya arrival ila sio kama Hong Kong.
Thailand pia ukatembee huko Pataya..
Cambodia ni visa ya Arrival sio mbalj na Thailand unaweza kwenda na bus tu pale ukitoka hapo unaitafuta Vietnam.
Unakua umeziacha Nchi kadhaa za Visa kama NK,Japan na SK pekee kwa ukanda huo ukiwa Hong Kong kule wanakouza magari usiku utayaona wakileta magari ya ujanja ujanja kutoka Japan na kuweka kwenye yard zao wajanja wapo kila sehemu..
 
Majiji ya China yana yote hayo isipokuwa yanazidiwa na majiji ya Marekani kwa Utamaduni mchanganyiko uliopo huko
Nitaongelea fursa,
China haina fursa nyingi za ajira, masomo na siasa kwa mgeni kutoka nje kama ilivyo Marekani. Marekani ndio nchi pekee hata Msukuma kutoka Gamboshi anaweza kuhamia na kuwa hadi mbunge, fursa za uchumi zilizoko China kwa wageni kutoka Africa labda ni kubeba box tu na kutafsiri lugha, Marekani vyuo vina matrilioni ya pesa ya kusaidia kusomesha hadi wahamiaji Trump anaofikiri ni haramu, haya ni machache tu.
 
Wenyewe wanasma hakuna jiji duniani kama New York City. Wachina wenyewe kila siku wanapambana kufika New York City...
Ni wale wachina wakutoka vijijini ndio wanaiota Marekani ili wakabadillishe mazingira..
China kwa sasa ni habari nyingine huwezi kufananisha na mijj ya kale ya Marekani zilizovuma miaka ya 70 na 80 kw sasa choka mbaya..
 
Hii miji ndo unasema imechoka?
premium_photo-1725408106567-a77bd9beff7c.jpeg

photo-1429554429301-1c7d5ae2d42e.jpeg
photo-1591553161262-0eeddc1f5c23.jpeg
istockphoto-2197944616-1024x1024.jpg
photo-1589083130544-0d6a2926e519.jpeg
istockphoto-2194272599-1024x1024.jpg
photo-1477959858617-67f85cf4f1df.jpeg
photo-1500916434205-0c77489c6cf7.jpeg
 
Ukimuuliza mwafrica achague nchi yakuishi kati ya china au USA atachagua USA,problem solved
 
China ni cheap labor ndio maana makampuni ya marekani na ulaya yamewekeza huko na India pia, mshahara wa kumlipa expert mmoja pale USA, China unawalipa Hao Hao experts watatu au wanne. Na kingine ni soko maana watu ni wengi hivyo kama Apple wakitoa simu mpya basi soko wanalo...
Kwa upande wa uzuri, kwa sasa China inajitahidi kimuonekano ni pazuri ila siyo sehemu ya kwenda kutafuta maisha, hasa kwa wapambanaji kama sisi tutaenda tu huko huko USA japo gharama za maisha ziko juu
 
Kwa wabeba boksi nendeni Marekani

Kwa sisi wafanyabiashara na watu wa shipping fursa iko China.

Wafanyabishara wa Kariakoo China imewafanya kuwa mabilionea

Mkinga au Mchaga wa K/koo na mawinga wao wanapapenda China kuliko Marekani
​
 
Kwa upande wa uzuri, kwa sasa China inajitahidi kimuonekano ni pazuri ila siyo sehemu ya kwenda kutafuta maisha,
China inakupa fursa ya kufanikiwa sio lazima ulowee kwao.

Mtu anayeenda China akiwa na business mindset anafanikiwa haraka kuliko anayeenda Marekani

China means business
​
 
Back
Top Bottom