USA wako serious sana. Uchumi wao ni mkubwa sana 30 trillion USD

Hizo tech ndo nchi nyingien gaina au umekaririshwa hapo
 
Kabisa mkuu. Na viwanda vya US ni viwanda kweli sio hv processinh
 
Uchumi wa China ni mkubwa kwa kutumia kigezo cha PPP, ndo maana marekani wameshindwa kushindana nae kwenye soko huru wanaishia kuweka vikwakwazo. Mtu akiwa na dola 100 china anawwza kuafford vitu vingi zaidi kuliko aliyoko USA mwenye kiasi hicho hicho
 
Mkuu,

Wape nafasi Waafrika wanaotaka kujadili chumi kubwa za dunia wazijadili bila kuweka ulazima wa chumi za Africa ambazo hazimo katika list ya chumi kubwa za dunia.

Ifikie wakati wanaotaka kufanya maongezi ya kidhahania kuhusu nchi nyingine waweze, si kila kitu kazima kitaje Africa ili kuwa na maana.

Mwishowe watu wataanza kujadili michezo ya winter kama skiing ambayo Africa haipo, na hapo napo utataka kuichomeka Africa.

Kama tunalinganisha chumi mbili kubwa za dunia obviously tutaongelea US na China. Hapo kutaka kuichomeka Africa ni ubishi tu.
 
Mkuu,

Ukiongelea soko huru Mchina naye amefanya hela yake Yuan iwe na thamani ndogo kuliko inavyopanda kwa soko huru ili ku promote exports za viwanda vyake.

Hivyo usiseme upande mmoja tu wa soko huru, kuna upande mwingine wa soko huru ambao China haiutaki na ukiruhusiwa itapata shida kushindana na Marekani.
 
Na deni la taifa ni $36 trillion
Hahaa.

Ukipima debt to GDP ratio ndiyo utaelewa kwa nini Mwigulu Nchemba anasema "deni letu linahimilika".

Ingawa ukisema deni linahimilika kila siku na kuendelea kukopa kuna siku halitahimilika.
 
Muda si mrefu Uchumi wa USA unafika 30 trillion USD.

Uchumi wa USA ni mkubwa Sana. Ni rahisi kuitawala dunia kwa huo uchumi

Mchina ana safari ndefu Sana.

Ana watu 1.4 billion na uchumi bado ni 18 trillion.
Mchina alipo toka na alipo sasa hivi si pakubeza.
 
Uchumi mzuri ni ule unao zalisha na sio unao toa huduma.
Hapana siyo kweli. Ndiyo maana hizo nchi ulizotaja zinategemea kwa zaidi ya asilimia 70 kwenye huduma.
 
Unatakiwa uwafungulie darasa maalumu la mambo haya. Maana wanaonekana ni weupe sana vichwani.
 
Hizo tech ndo nchi nyingien gaina au umekaririshwa hapo
Technology zao ni za hali ya chini kulinganisha na Marekani. Ila kulinganisha na Africa ni kama mbingu na nchi.
Huo ni ukweli.
 

kujadili ni tofauti na kucheka na kukejeri, sijamkataza na wala sina uwezo wa kumkataza mtu kujadili chochote ila tu kwangu inashangaza kidogo kucheka na kudharau mtu ambaye amefanya jitihada kubwa kujinasua wakati wewe unayemcheka uko chini kabisa kwa vipimo vyote vya kibinadamu tuvijuavyo, tanzagiza ukinunua gari dogo wanakucheka kwamba ni gari kike wakati hao wanaokucheka hata milo 3 kwa siku ni shida, ni ngumu kidogo kuelewa ni hivyo tu …
 
Umejuaje kama yeye ni Muafrika na siyo mmarekani?
 
Saudi Arabia wanajenga ski city ya $billion 500 kwa ajili ya michezo ya barafu.
 
Nani kacheka au kukejeli na kacheka au kakejeli kwa muktadha gani?

Weka post hapa tuichambue.

Mtu anaweza kuicheka au kuikejeli China kwa muktadha wa kutoka Marekani na akawa sawa tu. Kwa sababu mjadala ni kati ya China na Marekani Tanzania haipo hapo.

Ni sawa na mtu anavyoweza kuikejeli Manchester United kwa kuilinganisha na Manchester City bila kuhitaji kuichomeka Simba wala Yanga.

Ukileta habari za Tanzania unalazimisha tu.
 
Saudi Arabia wanajenga ski city ya $billion 500 kwa ajili ya michezo ya barafu.
Saudi Arabia si Africa mkuu. Nimeitaja Africa.

Yani nimesema watataka kuichomekea Africa hiyo ukaona haitoshi wewe umeichomekea Saudi Arabia.

Mradi uchomekee tu.
 
Hapana siyo kweli. Ndiyo maana hizo nchi ulizotaja zinategemea kwa zaidi ya asilimia 70 kwenye huduma.
Kati Instagram na mafuta ni kipi muhimu katika maisha ya kila siku kwa binadamu?
Hivi ulisha wahi kujiuliza ni kwa nini Urusi na Ukrain zina GDP ndogo lakini baada ya kuingia vitani uchumi wa dunia nzima ulitikisika ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…