Usajili wa Bernard Morrison kurudi Yanga, kuna mvutano mkali unaendelea!

Usajili wa Bernard Morrison kurudi Yanga, kuna mvutano mkali unaendelea!

Mashabiki wa yanga naona mnatoa povu sana kwa morison.inaonekana mliumia sana alivyoondoka kwenu.Mimi sioni kosa lolote la morisoni,maana mambo mengine niyakawaida kwenye soka sasa mnamtolea povu utafikiri kaua.Ata uko simba morisoni katoa msaada mkubwa kwa timu.makosa yake niya kinizamu kitu ambacho nikawaida kwa binadamu na sio yanayohusu majukumu yake uwanjani.Kwahiyo hata kama ataondoka simba ataondoka kwasababu za kawaida zamkataba kumalizika sio vinginevyo.Mashabiki wa bongo tunatatizo lakutaka mchezaji wa timu anayochezea naye awe shabiki lia lia watimu anayochezea bila kujua kua mchezaji pale ni kazini.Anawajibika kulingana na mkataba wake na mwajiri kwahiyo kila upande una haki dhidi ya mwingine nasio vinginevyo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hao wanaofikiria kumrudisha huyo jamaa Yanga wanawaza/wanafikiri kwa kutumia akili kweli au?

Kuwakoga Simba ili iweje? Ndio maana soka letu halikui kwa mawazo ya kipuuzi kama haya.

Huyo hafai kurudishwa/kurudi Yanga. Wamwache aende zake.

Hata C. Chota Chama haitapendeza kurudi Simba. Hana jipya tena. Vilabu vitafute vipaji vipya ili kukuza soka letu.

Tu-focus kwenye mashindano ya kuliletea taifa heshima katika mashindano makubwa, mfano AFCON na World Cup kutokana na wachezaji waliopikwa na kuiva kwenye vilabu vyetu vya soka.

Tusajili wachezaji walau kwa kigezo cha kuchezea timu ya Taifa huko walikotoka badala ya kuwaokota toka vichochoroni.

Huu U-Simba, U-Yanga, U-Azam n.k tusipouacha soka letu litaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu.

Mnaudhi sana!!!!
Una ela zakuwalipa hao wachezaji unaowawaza au unaongea tu.au unafikiti wanakuja bure.Alafu ni mchezaji gani wa maana atakayekuja kucheza bongo nchi ambayo haina hata viwanja vya maana mpira unachezwa kwenye tindiga.hao wanaokuja ndo level yetu sio zaidi ya hapo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Muache asepe, morrison ni mchezaji mzuri endapo ataacha uchoyo na kupenda kucheza kwa show off

Huko aendako akijirekebisha hayo mapungufu yake atakuwa ni mchezaji hatari na wakuhofiwa na wapinzani
bm3 hawezi kubadilika. Ndivyo alivyo.Kwa umri wake ndiyo hivyo tena.
Na si ajabu hapo alikuwa anatafuta kesi na Simba, sababu ndiyo zake.SA alipiga hela,Yanga kapiga hela pia kupitia kesi.

Na hakuna klabu alienda akaondoka kwa amani.
 
Bocco, Mugalu, Kagere, Morisson, Nyoni, na wengine hawana msaada tena pale SIMBA, wamefikia ukomo wao.

SIMBA inahitaji akili mpya na vitu vipya.
 
Lakini kumbuka wametumia almost mwaka mahakamani kuhakikisha wanamrejesha morrison, sasa huoni kwamba hii kwa upande wao ni kama golden chance?

Umetoka home umebeba mapanga na mimbwa kibao kwenda kuwinda sungura , umefika huko machakani umezurura umepoteza muda wako mwingi na hujapata chochote, halafu unafika home unakuta kumbe ulivyotoa uliacha mlango wazi una shangaa unamuona swala anajizungusha zungusha hana pa kwenda, utamuacha?
Atakuwa mgonjwa huyo.
 
Ila bana bestie ki soka la Tanzania Tanzania hao viongozi wanaeza ona pia kumchukua tena kuna mtu wanamkomoa. 🙁
Watakuwa wanamkomoa nani, wakati mkataba umeisha hajapewa mwingine , ameondoka km free agent. Hahitajiki ndiyo maana ataachwa aondoke , aende anakotaka.
 
Una ela zakuwalipa hao wachezaji unaowawaza au unaongea tu.au unafikiti wanakuja bure.Alafu ni mchezaji gani wa maana atakayekuja kucheza bongo nchi ambayo haina hata viwanja vya maana mpira unachezwa kwenye tindiga.hao wanaokuja ndo level yetu sio zaidi ya hapo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
[emoji38][emoji38] Sawa. Ila umeongeza msamiati katika lugha yetu ya kiswahili, "unafikiti"

Mikakati ikiwekwa vyema, hela za kuwalipa zitapatikana. Wachezaji wa kiwango watavutiwa kujiunga na vilabu vyetu.

Viwanja vyote sio tindiga kama unavyowaza. Mazingira ya Kiafrika % kubwa ya viwanja vinafanana.
 
Kiukweli Morison ni mchezaji mzuri sana na mpira anaujua hasa lakini kinachomwangusha ni mambo mawili makubwa nayo ni:
1. Nidhamu mbovu ndani na nje ya uwanja. Hapa nahisi kuna kilevi anakitumia si bure hasa nikikumbuka tukio la kuvua bukta tena kwenye mechi ya fainali halafu.maajabu klabu yake ya Simba haikumpa adhabu yoyote. Lile tukio lilimuacha hata kocha Nabi mdomo wazi kiasi alikuwa anajaribu kumlazimisha avae bukta japo si mchezaji wa timu yake. Kiufupi jama ni mwezi mchanga/ saa mbovu kama hawa wengine tunaoishi nao mtaani hawatabiriki leo mzima kesho majira hayasomi sawasawa.
2. Mizaha, ubinafsi na kucheza na jukwaa. Siku akiingia uwanjani akaacha mizaha na kucheza na jukwaa ujue siku hiyo atafanya kazi kubwa ya kuisaidia timu basi hapo kuanzia mashabiki, watangazaji, waandishi, n.k. kila mtu atamsifia. Akishapata sifa hizo mechi ijayo kichwa kinavimba anaanza tena kucheza na majukwaa anaigharimu timu.

Kuwa na mchezaji kama Morison kwenye timu inayotafuta mafanikio ni tatizo sana. Kwani hujui wakati gani ataisaidia timu au wakati gani ataiangusha timu. Kwa aina ya viongozi tulio nao wasioona mbali kwenye vilabu vyetu hivi viwili vya Simba na Yanga sitashangaa kusikia Morison kasajiliwa Yanga au hata karudi na kuongezea mkataba Simba.
 
Unasema muachieni huku moyoni unaumia
Niumie kwa kipi?

Simba hakuna mchezaji tegemeo, ni timu ambayo iko kwenye rank za juu kiubora baran africa na hapa east africa hakuna wakunlinganisha naye

Inagombewa na wachezaji wengi wakiamini ndio timu ya ndoto zao
 
Mpira wa bongo ni wa hovyo hovyo tu...

Hivi Simba wakati wanamsajili Morrison, si walijua kabisa jamaa ni kichwa cha moto...sasa wanavuna walichopandiwa na Morrison mwenyewe...

Haya waone nao Yanga wanataka kula matapishi tena kwa kumrudisha mtu aliyewatia hasara hadi za kwenda CAS...

Viongozi wa hivi vilabu ni wajinga wajinga fulani hivi...
 
Kama Yanga sc watakubali kumrudisha huyu jamaa, watakuwa wameturau sisi wapenzi, mashabiki na wanachama. Kike Ni kirusi (virus) Kama hamuamini jaribu. Mambo ya kusajili kwa kukomoana yamepitwa na wakati. Na sidhani Kama itatokea
Kama manara alikuwa anawatukana hamna akili na mkamchukua sembuse Morrison amabae hajawahi kuwatukana kama manara
 
Mashabiki wa yanga naona mnatoa povu sana kwa morison.inaonekana mliumia sana alivyoondoka kwenu.Mimi sioni kosa lolote la morisoni,maana mambo mengine niyakawaida kwenye soka sasa mnamtolea povu utafikiri kaua.Ata uko simba morisoni katoa msaada mkubwa kwa timu.makosa yake niya kinizamu kitu ambacho nikawaida kwa binadamu na sio yanayohusu majukumu yake uwanjani.Kwahiyo hata kama ataondoka simba ataondoka kwasababu za kawaida zamkataba kumalizika sio vinginevyo.Mashabiki wa bongo tunatatizo lakutaka mchezaji wa timu anayochezea naye awe shabiki lia lia watimu anayochezea bila kujua kua mchezaji pale ni kazini.Anawajibika kulingana na mkataba wake na mwajiri kwahiyo kila upande una haki dhidi ya mwingine nasio vinginevyo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Mkuu unaongea uongo kweupe unasema Simba anaondoka kwa sababu za kimkataba imekuaje asimamishwe? na inakuaje makosa ya kinidhamu unayaita ya kawaida kwako makosa makubwa ni yapi?
 
Back
Top Bottom