Inaendelea No 5,
Siku ya kuonana na Lily ilifika, alikuja akiwa amevaa kipensi cha kiume kifupi sana na singlend ili nione tattoo zake 😏, nilimchukia sikumuangalia kwa upendo, nilimuona kama shetani wa mguu mmoja, kwa mara ya kwanza nilitamani kua katili nimrukie nimpige hadi aombe msamaha na upande mwengine nilimuonea huruma, nilimuuliza Lily "mimi ndie nilikufanya uwe hivi au ulikua una tatizo lako ndani ndio limetoka baada ya kutikiswa na misukosuko?" akasema mimi ndio nilimfanya awe hivyo, nikamuuliza tena mara ya pili na kumtaka atulie kwanza kabla hajajibu swali, baada ya ukimya kidogo akasema ukweli mimi ndie niliyeitikisa hali iliyokuwepo ndani ya moyo wake na sio kwamba mimi ndie niliyesababisha awe hivyo,
Nikawa nashauku ya kujua ilikuaje, nikaingia kazini na kua therapist wake, nikamuomba afunguke asihofia chochote kwani tupo pale kwa nia ya kutengeneza na sio kuharibu, akatoa bangi aliyokwisha isokota tayari akaiwasha na kuvuta kama pafu tatu kwa mkupuo, nikatulia tulii huku nisimsikitikia aina ya maisha aliyoyachagua, Lily akafunguka, familia yake ndio ilisababisha, wamezaliwa wanne wote wa kike, baba ake alikua mfanyabiashara mkubwa wa madini Mwanza na mama ake alikua mfanyakazi wa bungeni kabla hajastaafu, yeye ni wa mwisho, anasema alikua akiona Mama yake anambagua sana kiufupi mama yake hakuonesha kumpenda hata kidogo pamoja na dada zake wote isipokua baba yake tu, anasema hakumbuki kama mama yake aliwahi kumkumbatia au kumshika mkono, au kumuongelesha kwa upole na upendo, waliishi maisha hayo hadi kuna kipindi alihisi yule sie mama ake, alipomaliza elimu ya sekondari ikabidi amuulize baba yake mbona mama yake anamchukia sana? baba akamwambia "kosa ni langu mwanangu, nilitamani sana kupata mtoto wa kiume ili tu nipate mrithi wa familia yangu na wa biashara zangu, wakati mama ako ana ujauzito wako nilikua nasema sana atazaa dume tukajijengea kichwani hilo, wote tulitamani mtoto wa kiume, maandalizi yote tulifanya kwa ajili ya kumpokea mtoto wa kiume hadi ulipozaliwa wewe wa kike, tulifedheheka lakini mimi nilijikaza na kumuachia Mungu, kwa bahati mbaya mama yako hakukubali hiyo sio kama anakuchukia ila anajihisi vibaya kukuona mtoto wa kike wakati mwanzo alikutengenezea picha ya mtoto wa kiume" japo baba ake alijaribu kuremba maneno lakini ukweli ulibaki kua mama ake Lily alimchukia mwanae kwa kuzaliwa wa kike na dada zake walirithi chuki ya mama yao dhidi yake hakuna la zaidi, ni pigo kubwa sana kwa mtoto kusikia kitu kama hicho,
Taratibu Lily akaanza kuact kama wakiume kwenye macho ya mama ake, akaanza kuvaa nguo za kiume anasema mwanzoni mama ake hakuelewa ila baadae ni kama alifurahi hapo kidogo akaanza walau kuongeleshwa na kwa mara ya kwanza mama ake alitabasamu mbele yake, kipindi hicho baba ake alikua kwenye biashara zake na aliweza kutokurudi nyumbani hata mwezi mzima, akasema siku hiyo baba yake alirejea na kumkuta akiwa kwenye mavazi ya kiume alikasirika sana akamkemea asirudie tena uvaaji huo akaacha, baada ya muda majibu ya chuo yalitoka na akapangiwa chuo cha Dar, Baba ake ndie alimleta chuo na ndio ikawa mara ya mwisho kuonana na baba ake kwani miezi michache baadae alifariki kwa ajali mbaya sana ya gari, akasema mtu pekee aliyempenda yeye kama alivyo aliondoka kwenye ulimwengu akawa mpweke sana, hakuna mtu kwenye familia yake ilijua au kujali kama anapitia depression kali sana, akiwa chuo alijiunga na vikundi mbalimbali angalau ikapunguza anachopitia, na siku niliyokutana nae kwenye ile semina licha ya kujitenga lakini niliweza kumuona na kukaa nae karibu akasema kilikua kitu kikubwa sana katika maisha yake, hakuwahi kuwaza kama msichana kama yeye anaweza akasema anaumwa na mtu akaacha shughuli zake na kwenda kumuangalia zaidi kumpelekea na zawadi, akasema hakuwahi kuamini kama msichana kama yeye kuna siku mtu anaweza akamjali kiasi ambacho akampeleka sehemu tofauti tofauti just kuenjoy, hakuwahi kupata raha kama nilizompa na anashindwa kukubali kua zile raha zilikua za muda mfupi tu, kama ambavyo baba ake alimuacha kipindi ambacho anamuhitaji,
Ilikua ni painful story, nikamkumbatia na kumwambia maneno mazuri, nilimsisitiza sana kujipenda yeye kwanza dunia imejaa watu makatili sana asikubali kuweka furaha yake kwenye mifuko ya watu wengine, amsamehe mama ake na zaidi anisamehe mimi, sikupanga kuja kwenye maisha yake na kumuumiza ila anatakiwa kujua watu huja na kuondoka kwenye maisha yetu, ajifunze kuwaacha waende asiwang'ang'anie mwisho wa siku yeye ndie anaumia, asiishi kutaka kuwafurahisha watu hata akiwa ni mama ake sababu binaadam hua hawaridhiki na kila siku huja na visa vipya.....
Baada ya kutulia tukakubaliana tubaki kua marafiki, tulikula na kunywa na kila mmoja alirudi kwake akiwa ana amani, kumbe yule nyoka alikua anarekodi mazungumzo yetu na akamtumia babe wangu vipande vipande alivyoona vinafaa kuniharibia......🙌🏻'
Itaendelea