PostGE2025 Ushahidi wa mauaji kwa watu wasiohusika na maandamano

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Am
Amiyn Allahumma Amyn
 
Correct
 
Pole sana; hatutaikiwi tena nchi hii kwaani inawenyewe. Wanyonge tutamalizwa.
 
Mkuu, itapendeza ukiweka na eneo tukio husika lilipotokea ili kuweka kumbukumbu sawa.
 
Yote haya yanapaswa kujibiwa na wenye dhamana ya ulinzi wa watu na mali zao.

Sisi kama wananchi hatuna chombo cha uchunguzi. Kwa waliokuwa na uniform na wasio na uniform anayepaswa kuwa accountable anajulikana.

Wananchi hatuna silaha za kivita, watu hawa wasio na uniform wana silaha za kivita ni akina nani? Tukumbuke weeks/a month back Mange kimambi alitoa taarifa juu ya kuingizwa kontena lenye silaha ambalo halinasibishwi na Majeshi yetu(taarifa kama hii ilipuuzwaje)

Katika mlolongo wote huu wa kuwa accountable anajulikana narudia.
 
Good observation.

Mpaka nachelea kusema waliotoa maagizo ya kutuliza maandamano “hawakukusudia hili”

Lakini hadi pale watakowajibika ndipo watajikosha na hili, Until then hili ni la kwao.

Ukiwa msomaji mzuri wa comments mtandaoni, Kuna watu wanazungumzia kuwa “zoeeni hiki ndicho alichofanya Hayati Mkapa (RIP) Pemba mwaka ule.. (Sina hakika na ukweli wa kinachoongelewa katika hizo comments na sijafunua vitabu vya historia kuhusu hili. )

Kauli iliyonukuliwa ya hayati Mkapa kwenye hotuba ya Rais Samia ilikuwa bahati mbaya?
 
Samia Suluhu Hassan damu hizi haziatakuacha salama hata kidogo usijetafuta mchawi.
Unfortunately kuna watu wataangushiwa huu mzigo.

Tuendelee Kuweka records sawasawa, mfululizo wa matukio ya utekaji kwa miaka minne, Kauli ya kiongozi mkuu juu ya utekaji na mauaji, kauli za jeshi la polisi, kutokumuwajibisha mtekaji hata mmoja… kejeli kwa waliotekwa na kulaumu victims… Waliotekwa walitekwa na waliokemea utekaji walitekwa.

Wana kesi ya kujibu.
 
Kwanza nikwambie katika umbwaji wa binadamu katika ulimwengu wa kiroho kuna maana kubwa sana,binadamu siyo sawa na mnyama,hao waliofanya hivyo tayali huko waliko wameshaanza kupata matatizo kutokana roho za watu waliowauwa,
Mfano mfupi siyo kila kichaa kalogwa,wengine ni sababu ya kufanyia mambo yao gizani kama kuuwa wanajikuta mwishowe wanachanganyikiwa
 
Hao ni wasomi wachache wanaokuja kupata vyeo vikubwa kama akina Mafwele na akina Muliro. Na hawa ni commanding officers.

Mimi naongelea utitiri wa haya maroboti ya huku chini yanayotumwa kwenda kupiga watu risasi hata kama ni familia mmekusanyika mnakula au watoto wamekusanyika ndani wanaangalia katuni.
 
Hebu tupia humu tuzione mkuu.
 
Sidhani kama kulikuwa na kitu kama hicho mkuu. Ni ushenzi tu wa polisi katika matumizi ua ovyo ya silaha
 
Hata kama walipewa maagizo ya kuua polisi walivuka mipaka na kwa hili Gen Z hawatasemehe na nichelee kusema maandamano yajayo watu watatua polisi there will be no mercy.Hizo video za vijana waliouawa kwenye banda la mpira,waliouawa nje ya nyumba zao zimechochea chuki kubwa mno.Tanzania itaingia kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe
 
Wakati hayo yote yanatokea Muliro na Wambura na makamanda wa Polisi wamejificha kambini Lugalo na familia zao wakilindwa na JW
 
Naam, kuna mengi endapo utatazama jambo hili katika angle tofauti. Japo sijasikiliza hiyo hotuba, unaweza quote hiyo kauli aliyowahi sema Mkapa ambayo imekua refered?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…