Ushahidi wa Nyaraka na vielelezo kuhusu UZanzibar wa Rais Samia huu hapa

zitto junior amekumaliza wala sina haja ya kukujibu tena
 
Sawa kabisa. Huo mjadala wa Muungano wa JMT unaweza kuendelea ikiwa ni pamoja na suala zima la uhitaji wa katiba mpya. Quite ok.

Mimi nimeshangaa kwamba tunaletewa “ushahidi” kuhusu “uZanzibari” wa Rais Samia. Labda nilikuwa usingizini tena ule wa hybernation kabisa. Sina habari kuwa Mh Samia kaukana uZanzibari wake. Au serikali imetangaza rasmi kuwa huyu Rais si Mzanzibari.

Pili, kwa mujibu katiba iliyopo, anastahili kabisa kuwa Rais na kufanya yote “yanayomfurahisha” kama watangulizi wake.

Hivyo, tusipoteze muda na huyu mtu. She’s just an individual riding on our own collective folly. Tatizo letu ni kubwa sana. Turudi tulipojikwaa na kupambana kurekebisha misingi.

Natamani wengi wetu tungekuwa na uwezo na utashi wa kufuatilia mabishano yanayoendelea huko US kwenye Supreme Court kuhusu hoja ya Trump kudai “total pesidential immunity”. Labda tungeelewa binadamu wenzetu wanavyopambana kuzuia ujinga kama huu unaoendelea hapa kwetu. Mapambano waliyoanza nayo huko 1700s wanaendelea nayo hadi leo. Hakuna kujisahau.
 
Hadi muda huu CHADEMA mmeshajichanganya sana. Aliyewashauri muingize udini na ukabila kwenye siasa zenu kawadanganya.
 
Zanzibar ni nchi na wala hatuhitaji ushahidi kuwa mama Samia ni Mzanzibari, tatizo ni wewe usiye na nchi.
 
Sema ukweli ki vyovyote vile ata kama inakugharimu, tokea tuanze kutawaliwa kwa hila tumepiga hatua gani ya maana?
Samia suluhu Hassani ni mzanzibar kwa mama bibi babu na mumewe ila hajafukuza wamasai kwa kuwa ni mzanzibar!
Rais wa Tanzania kuna mambo yasiyo ya Muungano hawezi kuyatekeleza huko Zanzibar, sasa kwanini atekeleze mambo yasiyo ya Muungano huku Tanzania Bara wakati anatoka upande wa Zanzibar?
Yaani anatekeleza mambo ya Tanganyika wakati yeye ni Mzanzibar
 
Wewe una kitambulisho cha Mtanganyika Mkaazi ?
Mkuu kwani wewe haunakitambulisho cha Mkazi?. Hili swali unaweza ukawa umeuliza kama dhihaka lakini ajabu ni kwamba kuna kitambulisho cha mkazi hata huku Bara. Mimi binafsi ninacho.

Hicho kitambulisho huwa kinatolewa ofisi ya Mtendaji wa Kata, kina rangi kama bluu hivi, kimeandikwa Kitambulisho cha Mkazi, kina nembo ya taifa ni cha kitabu kipo kama kadi za chama 😂 na kina namba ya ukazi.


Nikiwa nacho karibu nitakipiga picha ni update hii comment. Lakini pia watu wazima maBro waliokuwa serious na maisha watakuwa wanakijua na pengine wanacho pia.

-----Update----
Hicho hapo chini kumbe nipo nacho karibu hapa.
 

Attachments

  • IMG_20240430_181359.jpg
    1.6 MB · Views: 4
Njoo na hoja yako wacha ya kudandia!
 
Hicho ni cha Sungusungu
 
CHADEMA tafuteni hoja zenye mashiko, huu usanii wa TUNDU LISSU hauwezi kuwaongezea chochote kwenye kukubalika na wananchi. Kwani kuna tatizo gani kwa Samia kuwa na kitambulisho cha Mzanzibar mkazi?

Samia hakutengeneza Muungano bali ni waasisi wa Taifa letu wakiongozwa na JK Nyerere na Abeid Aman Karume.

Wakati wa muungano Tundu Lissu alikuwa hajazaliwa. Leo anapata wapi uwezo wa kukosoa makubaliano ya waasisi wa Taifa hili.

Tundu Lissu anamkejeli Rais Samia ambaye ndiye kiongozi wa juu aliyemtembelea hospitali Nairobi kumjulia hali wakati akiwa amelazwa baada ya WATU WASIOJULIKANA kumshambulia akiwa Bungeni Dodoma.

Samia alimtembelea pia Brussels alikokuwa anaishi maisha ya ombaomba kama mkimbizi baada ya kumkimbia Magufuli immwdiately baada ya uchaguzi wa mwaka 2020.

Huyu Samia ndiye aliyemfutia kesi za kubambikiza nankumlipa stahiki alizodhulumiwa kama mbunge wakati wa Magufuli.

Mtu hana shukrani kwa huyu Rais aliyemjali kama mdogo wake.

Nawahakikishia mashabiki wa Tundu Lissu kuwa cheo cha mwisho cha juu cha Tundu Lissu kupata maishani itabaki ni Makamu Mwenyekiti tu wa CHADEMA.
 
Hicho ni cha Sungusungu
Hicho ni kitambulisho cha Mkazi acha siasa za kitoto. Tafuta hoja ya kupinga hoja iliyo dhahiri sio janja janja. Tatizo Chadema ni kama imeacha kuwafundishi vijana wake mbinu za kihoja.

Mapungufu ya hichi kitambulisho cha Mkazi kwa upande wa Tanzania Bara/ Tanganyika kimepuuzwa sana hakijafanyiwa marekebisho kama usajili ya kisasa, na mambo kama hayo.

Kama hukijui au hujawahi kusikia habari za kitambulisho hicho basi jua bado una mengi sana ya kujifunza juu ya siasa na utawala wa nchi hii. Hichi kiwe kipimo kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…