Ushahidi wa Nyaraka na vielelezo kuhusu UZanzibar wa Rais Samia huu hapa

Ushahidi wa Nyaraka na vielelezo kuhusu UZanzibar wa Rais Samia huu hapa

Anachosema ni kwamba mtu ni Mtanzania ila at the same time ana kitambulisho rasmi cha mkazi wa zanzibar means Zanzibar ni sovereign state ndani ya Muungano. Swali linakuja, kama zanzibar ni sovereign state why hakuna nchi ya Tanganyika ili kuwe na party mbili zinazoungana?

Yaani Rais wa zanzibar anatakiwa awe mzanzibari mkaazi ila Rais wa Tanzania anaweza tokea Zanzibar pia ila kwa Tanganyika hatuna Rais na hauwezi ukagombea zanzibar?? Hiyo picha ina raise so many questions about nature ya muungano wetu.
Zanzibar siyo sovereign state bali ni autonomous state within the Government of Tanzania. Yaani ina maamuzi kwenye mambo fulani kasoro Ulinzi, Mambo ya Ndani
 
Zanzibar siyo sovereign state bali ni autonomous state within the Government of Tanzania. Yaani ina maamuzi kwenye mambo fulani kasoro Ulinzi, Mambo ya Ndani
Unajua maana Ya Sovereign state..
Zanzibar ina mamlaka yote ina Raia , Inaserekali ina Ardhi na ina power..

Wana Jeshi la Ulinzi pia Na Jeshi La mambo ya. Ndani pia Japo yanafanya kazi ndani ya Zanzibar..

For Your Info Zanzibar Ni Nchi ambayo Ina umri Mkubwa kuliko Hata Tanganyika..
Zanzibar Inakwenda Far Beyond Mwaka 1570s Na Tanganyika Ilianzishwa Mwak 1920s na waingereza
 
Mimi nadhani ni heshima kubwa na Uzalendo kwa mtu kuitwa kwa Utaifa wake, Sioni haja ya kuficha Utaifa wa mtu kwa sababu zozote zile.

Kwa nia njema kabisa naweka nyaraka za wazi za Uzanzibar wa Rais wetu Samia Suluhu Hassan

View attachment 2977513View attachment 2977516

Hata kwa Sheria za Tanzania, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano anapotokea Tanganyika(Tanzania Bara), Mgombea Mwenza (Makamu wa Rais) ni lazima awe Raia wa Zanzibar, Kwahiyo kumbe Wazanzibar wapo na ni lazima wawe Wazanzibar ili kugombea Uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO

Pia soma
Mbona uzanzibari sio shida. Kwa sheria ya zanzibari hata mbara akiishi zanzibar kwa miaka mitatu mfulilizo na kuweka makazi yake huko anakua mzanzibari. Wala uzanzibari sio utaifa maana taifa ni Tanzania. Uzanzibari ni ukazi tu. Sema tu kuna mizengwe kwa watanganyika kupatiwa vitambulisho wanapostahili.
 
Mkuu kwani wewe haunakitambulisho cha Mkazi?. Hili swali unaweza ukawa umeuliza kama dhihaka lakini ajabu ni kwamba kuna kitambulisho cha mkazi hata huku Bara. Mimi binafsi ninacho.

Hicho kitambulisho huwa kinatolewa ofisi ya Mtendaji wa Kata, kina rangi kama bluu hivi, kimeandikwa Kitambulisho cha Mkazi, kina nembo ya taifa ni cha kitabu kipo kama kadi za chama 😂 na kina namba ya ukazi.

Nikiwa nacho karibu nitakipiga picha ni update hii comment. Lakini pia watu wazima maBro waliokuwa serious na maisha watakuwa wanakijua na pengine wanacho pia.

-----Update----
Hicho hapo chini kumbe nipo nacho karibu hapa.
Lakini cha Ajabu ni kwamba Kitambulisho ulichonacho ni Cha JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA means hata Zanzibar ikiwemo..
Nafikiri Mtoa mada ananzungumzia vha Tangam
nyika
 
Hicho ni kitambulisho cha Mkazi acha siasa za kitoto. Tafuta hoja ya kupinga hoja iliyo dhahiri sio janja janja. Tatizo Chadema ni kama imeacha kuwafundishi vijana wake mbinu za kihoja.

Mapungufu ya hichi kitambulisho cha Mkazi kwa upande wa Tanzania Bara/ Tanganyika kimepuuzwa sana hakijafanyiwa marekebisho kama usajili ya kisasa, na mambo kama hayo.

Kama hukijui au hujawahi kusikia habari za kitambulisho hicho basi jua bado una mengi sana ya kujifunza juu ya siasa na utawala wa nchi hii. Hichi kiwe kipimo kwako.
Hicho ni Cha JMT na sio cha Mtanganyika na ndo maana Kina nembo ya JMT na jina la JMT
 
Nadhani nafasi ya urais ingebakia kwa mtanganyika tu.

Kisha kuuenzi muungano moja kati ya PM ama makamu wa urais hasa PM ningependa awe ni mzanzibar hasa aliyebobea kujua mazingira ya bara na siasa zake.

Hawa walau kwa uadilifu wao wangemsaidia Mtanganyika lakn pia kwa vile hawana nafasi ya kuwa Rais wa bara hivyo kuwa na siasa za kusaka madaraka hawatakuwa nazo.
 
Mbona uzanzibari sio shida. Kwa sheria ya zanzibari hata mbara akiishi zanzibar kwa miaka mitatu mfulilizo na kuweka makazi yake huko anakua mzanzibari. Wala uzanzibari sio utaifa maana taifa ni Tanzania. Uzanzibari ni ukazi tu. Sema tu kuna mizengwe kwa watanganyika kupatiwa vitambulisho wanapostahili.
Sheria ipi hiyo?
Mkuu tusipende kupotosha Sheria kwa matakwa yetu..

Ili uwe mzanzibar Lazima uwe Ni mzaliwa wa zanzibar Soma Kif. 5 cha Sheria Namba 2 ya mwaka 2002 ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar..
soma Pamoja na katiba ya SMZ ibara ya 6..

Kuhusu Utaifa wa Zanzibar Katiba ya Zanzibar Ibara ya 23 (3) inalitaja Zanzibar kama taifa

Au Labda Nikuulize Utaifa maana yake nini??
 
Nadhani nafasi ya urais ingebakia kwa mtanganyika tu.

Kisha kuuenzi muungano moja kati ya PM ama makamu wa urais hasa PM ningependa awe ni mzanzibar hasa aliyebobea kujua mazingira ya bara na siasa zake.

Hawa walau kwa uadilifu wao wangemsaidia Mtanganyika lakn pia kwa vile hawana nafasi ya kuwa Rais wa bara hivyo kuwa na siasa za kusaka madaraka hawatakuwa nazo.
Cha kushangaza ni Kwamba PM au waziri Mkuu wa Muungano hana mamlaka Juu ya zanzibar
 
Lakini cha Ajabu ni kwamba Kitambulisho ulichonacho ni Cha JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA means hata Zanzibar ikiwemo..
Nafikiri Mtoa mada ananzungumzia vha Tangam
nyika
Zanzibar hautakaa ukikute hivi, hapo ndio inaibuka hoja ya Tanganyika kuvaa koti la muungano. Kwa hoja hii inakubalika kabisa.

Ukikisoma ndani hicho kitambulisho ni full TAMISEMI ila sasa kilivyowekwa wekwa ndio kinahitaji marekebisho ya hali ya juu. Kiende sawa na wakati tuliopo.
 
Kitambulisho cha Mkazi wa Zanzibar siyo sawa na Hati ya Uraia aka Passport. Wazanzibari hawana Passport yao wenyewe wanatumia passport ya JMT. Labda tuangalie nini lengo la Wazanzibari kuwa na Kitambulisho cha Mkazi wa Zanzibar. Jee, Mtanzania Bara anaruhusiwa kupewa Kitambulisho cha Mkazi wa Zanzibar, na kama ni ndiyo, ni kwa vigezo gani?
 
Zanzibar hautakaa ukikute hivi, hapo ndio inaibuka hoja ya Tanganyika kuvaa koti la muungano. Kwa hoja hii inakubalika kabisa.

Ukikisoma ndani hicho kitambulisho ni full TAMISEMI ila sasa kilivyowekwa wekwa ndio kinahitaji marekebisho ya hali ya juu. Kiende sawa na wakati tuliopo.
Na hapo Ndo kuna Hoja ya walio wengi..
Kwamba Kwanini Tanganyika inakuwa Ngumu Midomoni mwa watu ila wazanzibar wako Proud na Nchi yao??

Na kwanini Tanzania Iwe Ni Muungano ila Ukichunguza kwa Makini ni Tanganyika Inayobeba Zanzibar??

Sijui umenielewa Maneno ya mwalimu Nyerere Bado mpaka Leo Yana Mashaka sana..

Hii Ni Page ya Kitabu chake kilichochapwa mwaka 1993 Kuhusu kwanini hakuna Serkali moja na kwanini hakuna Serkali Tatu..

Ukisoma Hoja zake Ni dhahiri kwamba Zina Gape kubwa sana..
Screenshot_20240430_160933_Chrome.jpg
 
Kitambulisho cha Mkazi wa Zanzibar siyo sawa na Hati ya Uraia aka Passport. Wazanzibari hawana Passport yao wenyewe wanatumia passport ya JMT. Labda tuangalie nini lengo la Wazanzibari kuwa na Kitambulisho cha Mkazi wa Zanzibar
Vitambulisha vya mkazi hivi hata wilayani huku bara walikuwa wanavitoa. Watendaji kata wamevitoa sana katika maeneo yao. Binafsi sio hoja sana ya kuwa na kitambulisho cha mkaazi.
 
Zanzibar ni nchi na wala hatuhitaji ushahidi kuwa mama Samia ni Mzanzibari, tatizo ni wewe usiye na nchi.
Zanzibar ni nchi???
Je, unataka kusema kwamba huyu Rais SSH tuliyenaye hivi Sasa anatawala nchi mbili tofauti za Zanzibar na Tanzania kwa wakati mmoja?? Je, ni Rais wa nchi mbili kwa wakati mmoja aunamaanisha Nini??
Je, unataka kusema kwamba SSH ni Raia wa Zanzibar ambaye ameikimbia nchi yake ya kuzaliwa ya Zanzibar na kuja kutawala ktk nchi ya ugenini iitwayo Tanzania???????Au unamaanisha Nini?
Fafanua tafadhali Sana.
 
Sidhani kama hii ni hoja ya maana nchini wakati huu. UZanzibari wa Rais Samia ni jambo lililo wazi kila Mtanzania mwenye akili anajua. Na si suala kabisa katika nafasi aliyopo. Ana stahiki zote. Yeye ni Mtanzania kamili; hajapungukiwa kitu hapo.

Sijui mleta mada unataka kuthibitisha kitu gani hasa hapa. Kama ni kumjibu Nape tu basi una kazi ngumu sana. Kuna mamilioni ya wehu nchi hii. Labda kama huoni tabu kushinda unajibizana na wendawazimu.

Kwa sisi wengine, tuwe wazi, unatupunguzia sana thamani ya JF kwa mada za aina hii kama vile vile anavyofanya Mwashambwa.
Ondoa hilo neno " wehu" . Tumia busara na lugha nzuri katika kuchangia.
 
CHADEMA mnafeli sana, daima mnatafuta kura kwa migawanyo, mara mkae kidini, mara kikanda mara kama hivi kizanzibar na Bara, yan mnatapa tapa kwa kila mbinu kuhakikisha mnafika ikulu, ila kibaya mnajiharibia, kwa style hii ya ubaguzi watu wa mipakani wanawaogopa tayari, zenji hawatakaa wawakubali,
Zenji ipi unayoiongelea hapa? Kama ni Zanzibar basi nikutaarifu kuwa hakuna watu wanaouchukia huu muungano kuwazidi wazanzibar wenyewe
 
Zanzibar ni nchi???
Je, unataka kusema kwamba huyu Rais SSH tuliyenaye hivi Sasa anatawala nchi mbili tofauti za Zanzibar na Tanzania kwa wakati mmoja?? Je, ni Rais wa nchi mbili kwa wakati mmoja aunamaanisha Nini??
Je, unataka kusema kwamba SSH ni Raia wa Zanzibar ambaye ameikimbia nchi yake ya kuzaliwa ya Zanzibar na kuja kutawala ktk nchi ya ugenini iitwayo Tanzania???????Au unamaanisha Nini?
Fafanua tafadhali Sana.
Kama haujuwi jibu ya swali lako sina uwezo wa kukusaidia, unaonesha hujuwi hata Tanzania ni nini.
 
Back
Top Bottom