Ushahidi wa Nyaraka na vielelezo kuhusu UZanzibar wa Rais Samia huu hapa

Sijawahi kusikia "Mtanzania Visiwani". Ni "Mzanzibari". Kwahiyo sielewi pointi yako ya wakazi wa Mafia na Ukerewe.
Ndo unatakiwa Ujiulize Kwanini Tuite bara wakati Ukerewe Na mafia Sio Bara ni Visiwani??

Tuwekee hicho kipengele kutoka Katiba ya Zanzibar kinachozungumzia Mzawa wa Zanzibar ni nani vis-a-vis Kitambulisho cha Mkazi wa Zanzibar.
Mkuu Uko Familiar na Katiba ya Zanzibar?
Na sheria inaitwa zanzibari Acts (Sheria no 5 ya mwaka 1985) ?

Kwa mujibu wa Katiba ya SMZ (Serkali ya Mapinduzi ya Zanzibar) Ibara ya Sita Mzanzibar ni Yule aliyezaliwa Zanzibar na kuishi zanzibar

Nakuongezea kasome sheria ya uzanzibari..
Utajua Mzanzibari wa kuzaliwa anakuaje na mzanzibar wengine wanakuaje
 
Nchi mbili zliungana, yaani Tanganyika na Zanzibar, kama Zanzibar ipo, Tanganyika iko wapi?
 
Inasikitisha sana, yani wachumia matumbo wanajitoa ufahamu kutetea vitu ambavyo vipo wazi kabisa. Hawa wazanzibar wametake advantage ya ujinga wa watanganyika. Ha ha wazanzibar kuanzia wilayani mpaka ikulu what a nonsense.
 
Sijaona mahali inataja sifa na vigezo vya kuitwa Mkazi wa Zanzibar/Mzanibari na uhusiano wa Hati ya Mkazi wa Zanzibar.

Kuitwa "Mtanzania Bara" au "Mbara" lengo ni kuwatenganisha Wazawa wa Tanganyika na Wazanzibari na Wapemba katika Muungano. Mafia na Ukerewe vipo Tanganyika. Wakazi wa huko wote ni Wabara hata kama wanaishi visiwani. Muhimu hapo ni territorial boundaries kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
 
Sijaona mahali inataja sifa na vigezo vya kuitwa Mzanzibari
Ooh Unataka Sifa za Kuitwa Mzanzibari?
Hizo sifa zipo kwa mujibu wa Sheria ya Uzanzibari ya mwaka 1985 (Sheria namba 5 ya mwaka 1985) "Zanzibari Act"

Kwa mujibu wa sheria Hiyo Mzanzibari ni
  • Raia wa Tanzania (Tanganyika +zanzibar) ambaye Kabla ya Muungano/Muungano Umemkuta akiishi Zanzibar "Kabla ya 1964 alikuwa akiishi Zanzibar"
  • Aliyezaliwa zanzibar Baada ya 1964 bila kujali Sehemu ya Muungano alikotokea..
  • Aliyeishi zanzibar Kwa Miaka isiyopungua 15 akiwa na nia na Tabia njema
ZIngine soma hapa chini Kifungu cha 3 mpaka cha sita cha sheria hiyo..
Utajua Jinsi ya kupata Uzanzibar na jinsi ya kuupoteza Uzanzibari






Sheria hiyo Pia makamu Wa Rais wa Zanzibar ameifafanua kidogo hapa
Your browser is not able to display this video.
 
Asante. Umefafanua kiungwana sana na nimekuelewa.
 
Nadhani tuko pamoja, Mamluki njooni mupinge na hili
 
Katiba irekebishwe, linapotokea lolote kwa rais wasiwe marais wa Tanganyika
 
kwahiyo ana kitambulisho cha utanzania, uzanzibar wakati anaowaongoza wana utanganyika peke yake.
 
.....hapo labda tutajadiliana tena 2028 2029 nitakapokua nakaribia kurudi kwangu Kizimkazi.....

Baada ya kauli hii nikasikia kuna wadau wamenyakwa huko nyanda za juu kusini
 
Ubaguzi unao wewe Bara ni nchi gani? Anza na hilo ili ujielewe.
 
Zanzibar ina watu milioni moja sisi huku bara tupo milioni 64.

Hatujielewi na huu umaskini unatupiga na kutuacha tumechanganyikiwa vichwani mwetu.
 

Dah wazee mumejisahau sana, Wazanzibar wanakuwa sahihi wanapolalamikia huu muungano. Kwa hiyo wao wawe hawaruhusiki kuwa Maraisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…