Ushauri: Chakula Bure mashuleni kirudishwe ili kuboresha uelewa wa wanafunzi

Shule nyingine mzazi anapeleka mahindi na maharage kwaajili ya chakula cha mtoto, nadhani wale ambao hawapeleki, watoto wao wanashinda njaa
 
Wazo zuri, sema wazazi waelimishwe kutoa michango, ila kusema serikali iwalipie kila kitu ni kulemezana,
Halafu hapo hapo serikali itapata kichaka cha kutoongeza mishahara au kuajiri
Wazazi wachangie wanapoweza,

Mikoa ya Moshi na Kilimanjaro wamefanikiwa,

Nachosema, Kwa mikoa yenye hamasa ya chini, wabunge waongeze juhudi, waombe michango Kwa banks, companies na asasi zingine, pungufu ya hapo waombe serikalini,

Pia jambo hili la chakula mashuleni liwe la kitaifa Nchi nzima.

Nchi yetu ni ya wakulima, Serikali haiwezi shindwa kuhakikisha mtoto anapata kikombe Cha uji.🙏🙏
 
Shule nyingine mzazi anapeleka mahindi na maharage kwaajili ya chakula cha mtoto, nadhani wale ambao hawapeleki, watoto wao wanashinda njaa
naona hili mikoa mingi ijifunze kwa weli maana mpaka sasa hivi shule za msingi kijijini kwetu wanakula
 
Shule nyingine mzazi anapeleka mahindi na maharage kwaajili ya chakula cha mtoto, nadhani wale ambao hawapeleki, watoto wao wanashinda njaa
Ndo hapo tutafute sababu za wazazi kutochangia,

Kama ni Umaskini ndo chanzo, Serikali iweke mkono wake.
 
naona hili mikoa mingi ijifunze kwa weli maana mpaka sasa hivi shule za msingi kijijini kwetu wanakula
Huku mijini ni mtihani ndugu yangu,

Wanashindia ubuyu Kwa kuomba wenzao wenye uwezo.

Jambo hili ni muhimu likawa flat Nchi nzima.
 
Hakuna chochote cha kuomba mzee, tusiwe omba omba ndo mwisho tunatengeneza kizazi cha ombaomba,
Watoto ni wa wazazi, hivyo wao watoe michango yote, watoto walishwe na wazazi wao na wajue jinsi wazazi wanavyoteseka hivyo waongeze juhudi.

Kuombaomba tutalea kizazi ambacho hata kusafisha mtaro wa barabaran wanasema serikali iingilie kati 🤣
 
Poleni "wadanganyika" chakula hakirudi kamwe mpaka siku mkijitambua.

Watoto wao hawasomi huko kwenye njaa , wamewaachia nyinyi.

Ukimuangalia huyo dogo hapo na nembo ya shule aliyopo unafikiri anaelewa kitu kinachoitwa njaa?

Siku akija kuwa kiongozi kwa mfumo huu wa vimemo, kujuana , kutembelea jina la baba atajua kuna shule huko Ikwiriri wanafunzi wanashinda njaa?

Never .
 
Kwahiyo tusitoe ushuru masokoni Ili tuzoe taka wenyewe,

Au tugomee tozo za mazao tunazolipia Ili tupate pesa ya kuwapa watoto shuleni?
 
Ni ubinafsi tu,

Madelu alikula chakula Cha Bure Cha Nyerere!!
 
Wananchi wa Jimbo la Iramba, tumkatae Madelu nchemba uchaguzi ujao sababu ni kiongozi wa Umma na waziri lakini anatusaliti kupeleka mwanae private school ilhali anasahau shule za kata.

Tunahitaji viongozi aina ya Mwl Nyerere na Magu ambao watoto wao walisoma shule za kata za Serikali. Na walijali elimu
 
Kiongozi wetu mkuu wa sasa ni mama na mwenye vichengerwa kadhaa, tafadhali unaweza kukumbukwa hata Kwa hili jambo dogo lenye mchango mkubwa sana mbeleni.
Mwenye shibe atamkumbuka mwenye njaa nchi hii!!!?
 
Hiyo hoja isubiri kwanza tumalize mambo muhimu:
  • tuwalipe kwanza mafao wenza wa wastaafu.
  • tutor kwanza elimu ya katiba
- tupeleke kwanza wasanii wakajifunze uendeshaji wa bandari Dubai.
 
Hiyo hoja isubiri kwanza tumalize mambo muhimu:
  • tuwalipe kwanza mafao wenza wa wastaafu.
  • tutor kwanza elimu ya katiba
- tupeleke kwanza wasanii wakajifunze uendeshaji wa bandari Dubai.
Tanzania nchi yangu😭
 
Enyi viongozi mnaofanya biashara serikalini, hamwoni kuwa Kwa namna moja au ingine mnahujumu uwezekano wa Nchi kurudisha chakula Bure Kwa wanafunzi mashuleni?
 
Ni mwaka gani palikuwa na chakula mashuleni?.
 
Chakula Serikali ilichotunza katika maghala, itoe kidogo Kwa watoto Walio mashuleni wapate japo uji🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…