Ushauri: Chakula Bure mashuleni kirudishwe ili kuboresha uelewa wa wanafunzi

Twende haraka kwenye mada.

Mama mwenye Upendo Kwa wanae, Yuko radhi ashinde njaa, ajinyime kununua kipande Cha kanga Ili mtoto wake apate kula chakula na kupata mahitaji muhimu, Watoto mashuleni katika shule za kata ni watoto wa Serikali wawapo mashuleni.

Viongozi wengi wa juu waliopo sasa ni mashuhuda kuwa zamani wanafunzi tulikula mashuleni Bure uji, ugali wa wanga, Hadi maziwa, tulionekana Kwa nje maskini lakini tulipata huduma muhimu ya CHAKULA muhimu shuleni na Elimu ilipaa na kuthaminika sana. Nini kimetokea, mbona mmebadilika ghafula?

Wazazi wanapokabidhi watoto wao Kwa Serikali kupitia shule za kata Ili wapewe Elimu, ni JUKUMU la Serikali kuhakikisha watoto wanapatachochote kitu tumboni Ili masomo yaeleweke na kumrahisishia mwalimu kufundisha Kwa muda wawapo shuleni.

ELIMU Bora inachagizwa na Mazingira Bora ya kufundishia kama madarasa, walimu wenye Viwango Bora, Madawati, nk nk

Uwezo wa kulisha wanafunzi wetu tunao, Nia tunayo? Ari tunayo kuhakikisha watoto wanapata chakula Bure mashuleni.?

Kuna watoto shule za msingi na sekondari wanatembea zaidi ya 5km kwenda na kurudi shuleni, na hurudi jioni saa kumi Hadi 12 jioni bila kula chochote shuleni, kusoma imekuwa ADHABU?

Nikisema Serikali itoe chakula Bure mashuleni, haimaanishi Bure, wazazi wanalipa Kodi serikalini Kwa njia mbalimbali.

Pia wazazi wengi Hasa wazazi wakulima wanalima chakula na kikiuza katika maghala ya Serikali.

Hivyo pakiwepo Nia thabiti, tunaweza kuhakikisha tunaanza japo na UJI mashuleni, wanafunzi wapate japo kikombe kimoja.

Shule Zina Utaratibu wa kuwafungia watoto mashuleni Hadi jioni saa kumi bila kula chochote.

Nauliza, hivi mtoto wa MKULIMA aliyetoka nyumbani bila kula chochote nyumbani wazazi wakienda shambani kulima, anawezaje kuelewa nasomo darasani bila kula chochote ?

Narudia tena, Serikali haitapata HASARA yoyote kuhakikisha wanafunzi wanapata japo kikombe Cha uji mashuleni Nchi nzima.

Kiongozi wetu mkuu wa sasa ni mama na mwenye vichengerwa kadhaa, tafadhali unaweza kukumbukwa hata Kwa hili jambo dogo lenye mchango mkubwa sana mbeleni.

Angalizo: Katika chaguzi zijazo msipokuja na HOJA nzito na muhimu kama Chakula mashuleni, maji safi, Nishati ya umeme shule za vijijini Kwa wanafunzi kujisomea usiku,sahauni kuchaguliwa.

Karibuni, Amen.
Uko sahihi sana boss, lakini ugali na maharage hauleti akili. Ni kweli wakishiba watakuwa na utulivu wa tumbo, lakini sio uelewa.
 
Kushinda njaa Hadi jioni bila chochote ni balaa zaidi.

Al least tuanze hata na kikombe Cha uji wa lishe.
 
Vya bure gharama, ukizaa mtunze mwanao
Umenena vyema,

Tanzania ni mama yetu, Serikali ya mama Tanzania isiwashindishe njaa watoto wake Hadi sasa 11 jioni Eti wajisomee na haiwapi hata kikombe Cha uji!!
 
Kikubwa ni Elimu kuwapa wazazi ili watambue umuhimu wa jambo hili na kushirikiana na serikali kutoa michango itakayowezesha wanafunzi wanapata chakula wawapo shuleni,na hivyo kusoma kwa utulivu na amani pasipo kuwa na mawazo ya njaa.
Ikiwa Serikali itashindwa kuhakikisha watoto wanapata kikombe Cha uji mashuleni,

Lini Serikali itaweza kununua laptop Kwa Kila mwanafunzi kama pale kanchi kadogo Rwanda?

CCM inatupeleka wapi jamani?
 
Ahsante Kwa marekebisho.

Naamini wataelewa na kuacha Roho mbaya.
Suala la WANAFUNZI WAPATE CHAKULA SHULENI hili kila mmoja amekubaliana nalo. Hongera kwa hoja.

Tofauti tu zipo kwenye chakula kitoke wapi;

Kuna waliotaka KITOLEWE BURE NA SERIKALI
Kuna waliotaka WAZAZI NDIO WACHANGIE
Sasa mie naileta hii WANAFUNZI WAJILISHE WAO WENYEWE!!!!

Yeaaah, hii ndio fursa ya kuwafundisha wanafunzi kujitegemea. Utasema labda wengine ni wadogo basi sawa. Tunaweza kuwaacha wa la kwanza hadi la tatu lakini baada ya hapo wajilishe na wawalishe wadogo zao!

Kama ambavyo wanafunzi wanaofagia na kusafisha mazingira yao wanaandaliwa kubeba majukumu yao kiusafi. Hebu piga picha wanafunzi wangekuwa wanajitafutia chakula chao wenyewe???

Sawa mazingira mengine hayaruhusu, basi sawa. Kuwe na miradi itakayotoa pesa za kununulia chakula inayoendeshwa na wanafunzi. Labda hao wa mjini watafanya biashara, whatever nayo ni elimu tunayoihitaji watoto wetu waijue pia. Basi wafanye kwa vitendo.

Kwa kumalizia nitaruhusu serikali itoe ruzuku za asilimia fulani kusapoti jitihada za kupata chakula, lakini isitoe chakula chenyewe. Iwawezeshe wanafunzi kupata nyavu lakini sio kuwagawia samaki. Kumbuka katiba yetu ni UJAMAA NA KUJITEGEMEA.
 
Kiongozi aliyepo ni mama na ana wahujuu kadhaa,

Huku saint kayumba ni wajukuu wake pia,

Atuonyeshe tofauti ya kiongozi mama, mwenye wajukuu na viongozi wa kiume ambao mara nyingi hutelekeza familia.
 
Suala la WANAFUNZI WAPATE CHAKULA SHULENI hili kila mmoja amekubaliana nalo. Hongera kwa hoja.

Tofauti tu zipo kwenye chakula kitoke wapi;

Kuna waliotaka KITOLEWE BURE NA SERIKALI
Kuna waliotaka WAZAZI NDIO WACHANGIE
Sasa mie naileta hii WANAFUNZI WAJILISHE WAO WENYEWE!!!!

Yeaaah, hii ndio fursa ya kuwafundisha wanafunzi kujitegemea. Utasema labda wengine ni wadogo basi sawa. Tunaweza kuwaacha wa la kwanza hadi la tatu lakini baada ya hapo wajilishe na wawalishe wadogo zao!

Kama ambavyo wanafunzi wanaofagia na kusafisha mazingira yao wanaandaliwa kubeba majukumu yao kiusafi. Hebu piga picha wanafunzi wangekuwa wanajitafutia chakula chao wenyewe???

Sawa mazingira mengine hayaruhusu, basi sawa. Kuwe na miradi itakayotoa pesa za kununulia chakula inayoendeshwa na wanafunzi. Labda hao wa mjini watafanya biashara, whatever nayo ni elimu tunayoihitaji watoto wetu waijue pia. Basi wafanye kwa vitendo.

Kwa kumalizia nitaruhusu serikali itoe ruzuku za asilimia fulani kusapoti jitihada za kupata chakula, lakini isitoe chakula chenyewe. Iwawezeshe wanafunzi kupata nyavu lakini sio kuwagawia samaki. Kumbuka katiba yetu ni UJAMAA NA KUJITEGEMEA.
Ndugu Uhakika bro, umewahi kuwa na watoto?

Unaanzaje kuwaambia wanao Walio darasa la nne nyumbani kwako wajitafutie chakula wenyewe?

Yaani unamshauri kiongozi wetu tena mwanamke awambie wanae Walio shule za msingi wajitafutie wenyewe chakula, na kusoma wasome sangapi?
 
Ndugu Uhakika bro, umewahi kuwa na watoto?

Unaanzaje kuwaambia wanao Walio darasa la nne nyumbani kwako wajitafutie chakula wenyewe?
Nimewahi kuwa mtoto

Nilitia jitihada katika kukitafuta chakula nyumbani (nilikuwa nikilima tangu mtoto).

Palipopunguka wazazi walijazia

Ndio maana ninaomba serikali iende ikabariki jitihada za watoto kujilisha.

Unajua hii hali ya kumpatia mtoto kila kitu, akikua ndio anaendelea kumtafuta 'mama' mwingine wa kumpa kila kitu. Kama tu unavyoomba wapewe chakula bure

Serikali, mama, baba, yeyote anatakiwa kubariki jitihada za 'watoto' kujitafutia maisha.

Mtoto anapaswa kufundishwa kuwa baba yeye mwenyewe. Ukidhani ipo siku atabadilika ghafla na kuyabeba majukumu yote ghafla utachelewa. Mambo yanaenda kidogokidogo (gradually)
 
Tunataka uchaguzi ujao, vyama makini vije na mkakati kuhakikisha chakula mashuleni kinapatikana, na zaidi ya hapo,

Shule ziunganishwe sollar na wanafunzi wote kuanzia shule za msingi Serikali inunue LAPTOPS Kwa ajili ya kujisomea kuendana na viwango vya kidunia.
 
Twende haraka kwenye mada.

Mama mwenye Upendo Kwa wanae, Yuko radhi ashinde njaa, ajinyime kununua kipande Cha kanga Ili mtoto wake apate kula chakula na kupata mahitaji muhimu, Watoto mashuleni katika shule za kata ni watoto wa Serikali wawapo mashuleni.

Viongozi wengi wa juu waliopo sasa ni mashuhuda kuwa zamani wanafunzi tulikula mashuleni Bure uji, ugali wa wanga, Hadi maziwa, tulionekana Kwa nje maskini lakini tulipata huduma muhimu ya CHAKULA muhimu shuleni na Elimu ilipaa na kuthaminika sana. Nini kimetokea, mbona mmebadilika ghafula?

Wazazi wanapokabidhi watoto wao Kwa Serikali kupitia shule za kata Ili wapewe Elimu, ni JUKUMU la Serikali kuhakikisha watoto wanapatachochote kitu tumboni Ili masomo yaeleweke na kumrahisishia mwalimu kufundisha Kwa muda wawapo shuleni.

ELIMU Bora inachagizwa na Mazingira Bora ya kufundishia kama madarasa, walimu wenye Viwango Bora, Madawati, nk nk

Uwezo wa kulisha wanafunzi wetu tunao, Nia tunayo? Ari tunayo kuhakikisha watoto wanapata chakula Bure mashuleni.?

Kuna watoto shule za msingi na sekondari wanatembea zaidi ya 5km kwenda na kurudi shuleni, na hurudi jioni saa kumi Hadi 12 jioni bila kula chochote shuleni, kusoma imekuwa ADHABU?

Nikisema Serikali itoe chakula Bure mashuleni, haimaanishi Bure, wazazi wanalipa Kodi serikalini Kwa njia mbalimbali.

Pia wazazi wengi Hasa wazazi wakulima wanalima chakula na kikiuza katika maghala ya Serikali.

Hivyo pakiwepo Nia thabiti, tunaweza kuhakikisha tunaanza japo na UJI mashuleni, wanafunzi wapate japo kikombe kimoja.

Shule Zina Utaratibu wa kuwafungia watoto mashuleni Hadi jioni saa kumi bila kula chochote.

Nauliza, hivi mtoto wa MKULIMA aliyetoka nyumbani bila kula chochote nyumbani wazazi wakienda shambani kulima, anawezaje kuelewa nasomo darasani bila kula chochote ?

Narudia tena, Serikali haitapata HASARA yoyote kuhakikisha wanafunzi wanapata japo kikombe Cha uji mashuleni Nchi nzima.

Kiongozi wetu mkuu wa sasa ni mama na mwenye vichengerwa kadhaa, tafadhali unaweza kukumbukwa hata Kwa hili jambo dogo lenye mchango mkubwa sana mbeleni.

Angalizo: Katika chaguzi zijazo msipokuja na HOJA nzito na muhimu kama Chakula mashuleni, maji safi, Nishati ya umeme shule za vijijini Kwa wanafunzi kujisomea usiku,sahauni kuchaguliwa.

Karibuni, Amen.
Kuna vidonda havisikii dawa. Ni mpaka mwili ukatwe ndiyo vinapona.
 
Nimewahi kuwa mtoto

Nilitia jitihada katika kukitafuta chakula nyumbani (nilikuwa nikilima tangu mtoto).

Palipopunguka wazazi walijazia

Ndio maana ninaomba serikali iende ikabariki jitihada za watoto kujilisha.

Unajua hii hali ya kumpatia mtoto kila kitu, akikua ndio anaendelea kumtafuta 'mama' mwingine wa kumpa kila kitu. Kama tu unavyoomba wapewe chakula bure

Serikali, mama, baba, yeyote anatakiwa kubariki jitihada za 'watoto' kujitafutia maisha.

Mtoto anapaswa kufundishwa kuwa baba yeye mwenyewe. Ukidhani ipo siku atabadilika ghafla na kuyabeba majukumu yote ghafla utachelewa. Mambo yanaenda kidogokidogo (gradually)
Ikiwa ilipitia taabu Ukiwa mtoto,

Usilipize Kwa wanao. Huo ni unyanyasaji.

Nakubaliana nawe, mtoto anapaswa kufundishwa kujitengemea pole pole muda wa ziada.

Lakini kumuunguza direct mtoto kwenye uzalishaji Ili ajilishe huo ni unyama.

Ikiwa unatumia pombe, acha ulevi Ili pesa ibaki Kwa ajili ya kuhudumia familia Yako.
 
Kuna vidonda havisikii dawa. Ni mpaka mwili ukatwe ndiyo vinapona.
Huwa nafanya utafiti mashuleni ndugu Hasa shule za kata,

Wanafunzi wanafungiwa Hadi sasa kumi jioni Eti wajisomee , na walimu hawawapi chochote kitu Wala kuwaruhusu warudi makwao kula na kurejea baadae.
 
Ikiwa ilipitia taabu Ukiwa mtoto,

Usilipize Kwa wanao. Huo ni unyanyasaji.

Nakubaliana nawe, mtoto anapaswa kufundishwa kujitengemea pole pole muda wa ziada.

Lakini kumuunguza direct mtoto kwenye uzalishaji Ili ajilishe huo ni unyama.

Ikiwa unatumia pombe, acha ulevi Ili pesa ibaki Kwa ajili ya kuhudumia familia Yako.
Ona sasa madhara yaliyopo

Nini kimekufanya uione kazi kuwa ni taabu(laana), sisi tuliambiwa kazi ni heshima.

Nakushauri kama una watoto soma kitabu cha 'Parenting with Love and Logic'

Unajua hata kama una hela, ukimlea mtoto kikuhudumiwa kila kitu halafu baadaye ukaja kumrithisha hiyo mali. Kimaajabu ataona kuwa hiyo mali ni mzigo mzito!!?

Lakini ukijaribu kumpa kazi ya, kukuhesabia noti hizo (labda ni mdogo) au kufunga mahesabu (mkubwa) chochote kulingana na kiwango ndio utawezesha mali kudumu vizazi na vizazi.

Nenda kachunguze tafiti ni sababu zipi zinaonesha mali hupotea asilimia sabini kufikia kizazi cha tatu cha aliyetoboa!???

Nikusanue tu mojawapo ya kichocheo ni hii kauli 'mimi nilipata tabu, sitaki mwanangu apate shida hata kidogo'
 
Nisaidie mfumo wa kumfanya mtoto wa darasa la nne ajilishe mwenyewe na masomo yakiendelea.
 
Twende haraka kwenye mada.

Mama mwenye Upendo Kwa wanae, Yuko radhi ashinde njaa, ajinyime kununua kipande Cha kanga Ili mtoto wake apate kula chakula na kupata mahitaji muhimu, Watoto mashuleni katika shule za kata ni watoto wa Serikali wawapo mashuleni.

Viongozi wengi wa juu waliopo sasa ni mashuhuda kuwa zamani wanafunzi tulikula mashuleni Bure uji, ugali wa wanga, Hadi maziwa, tulionekana Kwa nje maskini lakini tulipata huduma muhimu ya CHAKULA muhimu shuleni na Elimu ilipaa na kuthaminika sana. Nini kimetokea, mbona mmebadilika ghafula?

Wazazi wanapokabidhi watoto wao Kwa Serikali kupitia shule za kata Ili wapewe Elimu, ni JUKUMU la Serikali kuhakikisha watoto wanapatachochote kitu tumboni Ili masomo yaeleweke na kumrahisishia mwalimu kufundisha Kwa muda wawapo shuleni.

ELIMU Bora inachagizwa na Mazingira Bora ya kufundishia kama madarasa, walimu wenye Viwango Bora, Madawati, nk nk

Uwezo wa kulisha wanafunzi wetu tunao, Nia tunayo? Ari tunayo kuhakikisha watoto wanapata chakula Bure mashuleni.?

Kuna watoto shule za msingi na sekondari wanatembea zaidi ya 5km kwenda na kurudi shuleni, na hurudi jioni saa kumi Hadi 12 jioni bila kula chochote shuleni, kusoma imekuwa ADHABU?

Nikisema Serikali itoe chakula Bure mashuleni, haimaanishi Bure, wazazi wanalipa Kodi serikalini Kwa njia mbalimbali.

Pia wazazi wengi Hasa wazazi wakulima wanalima chakula na kikiuza katika maghala ya Serikali.

Hivyo pakiwepo Nia thabiti, tunaweza kuhakikisha tunaanza japo na UJI mashuleni, wanafunzi wapate japo kikombe kimoja.

Shule Zina Utaratibu wa kuwafungia watoto mashuleni Hadi jioni saa kumi bila kula chochote.

Nauliza, hivi mtoto wa MKULIMA aliyetoka nyumbani bila kula chochote nyumbani wazazi wakienda shambani kulima, anawezaje kuelewa nasomo darasani bila kula chochote ?

Narudia tena, Serikali haitapata HASARA yoyote kuhakikisha wanafunzi wanapata japo kikombe Cha uji mashuleni Nchi nzima.

Kiongozi wetu mkuu wa sasa ni mama na mwenye vichengerwa kadhaa, tafadhali unaweza kukumbukwa hata Kwa hili jambo dogo lenye mchango mkubwa sana mbeleni.

Angalizo: Katika chaguzi zijazo msipokuja na HOJA nzito na muhimu kama Chakula mashuleni, maji safi, Nishati ya umeme shule za vijijini Kwa wanafunzi kujisomea usiku,sahauni kuchaguliwa.

Karibuni, Amen.
Haya mambo ya watu kupewa ama kutolewa vitu vya bure na serikali ndiyo hasa kichocheo cha lindi la umaskini katika jamii nyingi za Kiafrika ikiwemo za Kitanzania. Ni lazima sheria za ustawi wa jamii zibane ili watu wepuke kuzaana hovyo.

Yaani inaingia akilini watu wazaliane hovyo na kukwepa kuwajibika, halafu jukumu la malezi ikiwemo gharama za elimu na lishe libebwe na serikali!? Sheria kali zitungwe ili kila atakayezalisha mtoto awajibike moja kwa moja kwa gharama zote muhimu za malezi ya mtoto.

Ifike wakati sheria zitamke wazi kuwa kama mtu hana uwezo wa kugharamia malezi ya mtoto, basi hana haki kuzalisha ama kuzaa. Kinyume chake afanye kazi za jamii bure ili fedha zipatikane kwa ajili ya malezi ya mtoto ama watoto wake.

Yaani watu wanapenda sana kunyemba na kunyembwa kama stahere za kizinifu tu. Lakini mtoto akizaliwa kwa makusudi kabisa wanakwepa kuwajibika! Shame on them!
 
Kwahiyo unashauri wazazi wawe wanapika vyakula majumbani na kuwapelekea watoto wao mashuleni muda wa break?
 
Haya mambo ya watu kupewa ama kutolewa vitu vya bure na serikali ndiyo hasa kichocheo cha lindi la umaskini katika jamii nyingi za Kiafrika ikiwemo za Kitanzania. Ni lazima sheria za ustawi wa jamii zibane ili watu wepuke kuzaana hovyo.

Yaani inaingia akilini watu wazaliane hovyo na kukwepa kuwajibika, halafu jukumu la malezi ikiwemo gharama za elimu na lishe libebwe na serikali!? Sheria kali zitungwe ili kila atakayezalisha mtoto awajibike moja kwa moja kwa gharama zote muhimu za malezi ya mtoto.

Ifike wakati sheria zitamke wazi kuwa kama mtu hana uwezo wa kugharamia malezi ya mtoto, basi hana haki kuzalisha ama kuzaa. Kinyume chake afanye kazi za jamii bure ili fedha zipatikane kwa ajili ya malezi ya mtoto ama watoto wake.

Yaani watu wanapenda sana kunyemba na kunyembwa kama stahere za kizinifu tu. Lakini mtoto akizaliwa kwa makusudi kabisa wanakwepa kuwajibika! Shame on them!
Wezi wa Mali za umma wengi ndo Wana mawazo kama Yako.
 
Back
Top Bottom