Ushauri: Chakula Bure mashuleni kirudishwe ili kuboresha uelewa wa wanafunzi

Upo sahihi njaa ndo inasababisha watoto wakike wajitongozeshe kwa walimu ili kutibu njaa

Kiufupi njaa watu wanaichukulia Ila Mtu mwenye hawezi kuwa na msimamo.
 
Upo sahihi njaa ndo inasababisha watoto wakike wajitongozeshe kwa walimu ili kutibu njaa

Kiufupi njaa watu wanaichukulia Ila Mtu mwenye hawezi kuwa na msimamo.
Ikiwa mtu mzima hawezi anatatizwa na njaa ikipita masaa 6 tu,

Iweje mtoto mdogo shule ya msingi tena akisoma somo la HISABATI?

Serikali iliangalie hili, huu ni unyanyasaji!!
 
Wanasiasa hawana mpango na vitu visivyo kua na maslahi ya moja kwamoja katika harakati zao za kisiasa,waache kununua magoli wakalishe watu ambao hata kura hawapigi.
 
Wanasiasa hawana mpango na vitu visivyo kua na maslahi ya moja kwamoja katika harakati zao za kisiasa,waache kununua magoli wakalishe watu ambao hata kura hawapigi.
Shule haipasi kuwa kama gereza.

Maana hata gereza Huwa wanakula. Mtoto mdogo apewe HAKI yake ya kula na kuishi.
 
Hii ndo ilikuwa Sera ya Rais wangu Hashimu Rungwe, wadanganyika wakampuuza na kuchagua tozo, bei kubwa za mafuta na mgao wa umeme.
Kweli Mtanzania hawezi kuwa na mbele hata kama YESU akirudi.
 
Hii ndo ilikuwa Sera ya Rais wangu Hashimu Rungwe, wadanganyika wakampuuza na kuchagua tozo, bei kubwa za mafuta na mgao wa umeme.
Kweli Mtanzania hawezi kuwa na mbele hata kama YESU akirudi.
Kuna mahindi yapo katika maghala ya Serikali,

Na Bado wanashindwa kuhakikisha Kila mtoto anapata hata kikombe Cha uji awapo shuleni, break ya saa nne asubuhi!!
 
Nisaidie mfumo wa kumfanya mtoto wa darasa la nne ajilishe mwenyewe na masomo yakiendelea.
Kulima kibustani cha mbogamboga na kuambiwa tutauza mboga tununue ugali.

Lakini serikali kuongezea mahindi (mfano batch iliyozidi NFRA ipelekwe mashuleni kwa kiasi) ili wapate unga wa kutosha..... tena sio lazima serikali wazazi kuchangia mahindi na maharage.

Mwisho wa siku suala la kutokomeza njaa mashuleni limekuwa jukumu la wote, wanafunzi, wazazi na inapobidi ndo serikali.
 
Unayo HOJA.

Bt unanikumbusha niliwahi tembelea Kijiji kimoja,

Walimu wanawapeleka watoto wa shule ya msingi kubeba tofali za kuchoma za wanakijiji, pesa wanayolipwa walimu wanatia mfukoni,

.Wazazi wakihoji why, wanajibiwa kuwa mtoto anafundishwa kujitengemea.

Na Ilikuwa twice per week.
 
Kwa mfano wako sitakubaliana na hao waalimu. Si sawa.

Maana hapo wametumikishwa kwa faida ya watu wengine. Wamefundishwa utumwa.

Labda kama maelezo yako umeyatia chumvi ili kuamsha hisia.

Hiyo sio sawa

Lakini kama wanafunzi haohao, watabebeshwa tofali ili waijenge maktaba/maabara yao hapo sina pingamizi. Iendane tu na saizi yao. Mdogo sana asibebe. Wa kati kipande na mkubwa tofali eeasy.
 
Wezi wa Mali za umma wengi ndo Wana mawazo kama Yako.
Wavivu wa kufikiri na kutenda ndiyo wenye akili za kimakalio kama zako. We penda tu vya bure,, ni lazima hata shemejiyo kakuchoka toka kitambo sana, bali anakusitiri tu kwa ajili ya uking'ang'anizi wa dada yako.
 
Mbona ninyi mnaiba pesa za umma zilizokopwa?

Hujaona tunavyotembeza mabakuli Nchi mbalimbali ilhali tuna Kila kitu hapa?
 
Kwahiyo unashauri wazazi wawe wanapika vyakula majumbani na kuwapelekea watoto wao mashuleni muda wa break?
Sio wazazi wapike vyakula, bali wawajibike kuchangia gharama za chakula kwa ajili ya lishe ya watoto wao pale wawapo shuleni. Kwani wakiwa nyumbani kwao huwa wanamtegemea nani awape chakula!?
 
Sio wazazi wapike vyakula, bali wawajibike kuchangia gharama za chakula kwa ajili ya lishe ya watoto wao pale wawapo shuleni. Kwani wakiwa nyumbani kwao huwa wanamtegemea nani awape chakula!?
Ubinafsi unakusumbua.

Mwalimu Nyerere mbona aliweza katika utawala wake na ndo kwanza tulikuwa tumetoka kupata uhuru?

Uwezo wa wazazi inatofautiana sana.

Serikali Inatakiwa kuondoa matabaka hayo, wote wawe flat wakipata chakula Cha Serikali mashuleni Nchi nzima.
 
Mbona ninyi mnaiba pesa za umma zilizokopwa?

Hujaona tunavyotembeza mabakuli Nchi mbalimbali ilhali tuna Kila kitu hapa?
My friend, mimi si mtumishi wa umma, nipo sekta binafsi na ninazungusha fursa kibinafsi mwenyewe kama kuku wa kiemyeji. Pengine wewe ndiye upo katika sekta ya umma, ila tu unakosa fursa za kiupigaji.

Kanuni kuu ni mbili tu,
Namba 1: Kuwa mwadilifu katika matendo yako mwenyewe, ndipo utakapo kuwa mudailifu kwa wengine, na fursa nzuri za maisha zitakufuata.
Namba 2: Zingatia kwa dhati kanuni namba 1 hapo juu.
 
KAZI Yako hainihusu,

Naongea na Serikali inayokusanya Kodi Kutoka Kwa wananchi,

Nataka bibi kijijini aliyeachiwa wajukuu yatima , asiye na uwezo wa kuwalisha Milo mitatu,

Angalau Serikali imsaidie kuwapa yatima hao japo kikombe Cha uji wawapo shuleni Ili bibi awatafutie chakula Cha usiku Kwa kuombaomba barabarani.
 
Ni kweli inashangaza mzazi aliyehurumiwa na serikali asitoe ada elfu 30 au 40 shule ya sekondari ya kata eti huyo huyo achangie shuleni gunia 2 za mahindi debe 2 za maharage na hela ya mpishi elfu 80.It doesn't make sense.Kuna watoto wameshindwa kutimiza ndoto zao za kusoma sekondari kwani wazazi wao hawana uwezo wa kumudu hiyo michango.Serikali yetu chini ya mama Samia ilione hili kwenye budget ijayo inshallah
 
Inashangaza sana,

Hasa Kwa mtu mwenye akili timamu mwenye uwezo wa kuchanganua issues Kwa upana wake.
 
Unazaa hovyo na kumtelekeza mama mtoto, na yeye anaenda kumtelekeza mtoto kijijini kwa bibi yake, halafu mtoto unamuita yatima ili asaidiwe na serikali! Wewe ni mhalifu na mbadhilifu wa mali za umma kama vile wengine walivyo.

Yaani hutaki kuwajibika katika kugharamia watoto kwa kisingizio cha hali ngumu ya maisha! Kwa nini usife kabisa ili tujue moja tu, kuwa mojawapo ya rasilimali watu hasara imeondoka katika jamii yetu.

Huenda baadhi ya watoto ombaomba barabarani na wengine waliotelekezwa kwa bibi zao wewe ni mmoja wa baba yao. Leo unatafuta huruma ili weweze kusadiwa kwa hoja dhaifu sana. Ngoja sheria ya utambuzi wa madogo hawa kupitia vipimo vya D.N.A ianze kazi, na utaipata fresh ndugu yangu.
 
Tutakutana 2024/2025.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…