Ushauri kuhusu mawazo yangu kabla sijampa kazi msanifu majengo

rabadaki

Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
23
Reaction score
37
Habari ndugu wana Jamii Forums,
Nipo kwenye mchakato wa kumtafuta msanifu majengo anichoree ramani ya nyumba ya kuishi familia ghorofa moja ndogo simple isiyo na makorokoro mengi maana kiwanja ni kidogo.

Nyumba yangu ya kwanza, msanifu majengo mweledi kabisa alitumika na bado chumba ninacholala na cha mtoto wa kiume vipo uelekeo ambao mchana hakulaliki sababu ya jua. Alikosea location ya public toilet matokeo yake public toilet ipo karibu (korido uelekeo) kabisaaa na masterbedeoom yangu i.e. no privacy!. Kulikuwa na makosa mengine pia lakini tuyaache.

Mawazo yangu ni kuwa ukubwa wa sehemu mbalimbali kwa wastani utakuwa kama nilivyoainisha hapo chini kwenye ukubwa huu nimezingatia kuwa mbele nipate sehemu ya kupark magari na pia kukaa na wanaume wenzangu hasa upande wa uelekeo wa dining-nitapanda miti kwa ajili yakivuli Upande wa uelekeo wa jiko kutakuwa na nafsi ya gari kupita.

Nimesketch ramani hapo chini ambapo nimeweka mawazo yangu namna ninaona mpangilio wa vyumba/ukubwa uwe ikiwa na maana pindi nitakapo mpa msanifu majengo hayo ndo yatakuwa mawazo yangu nitakayomwambia bila shaka najua atanishauri vingine vingi tu maana yeye ndo mtaalamu lakini nimetaka nisiwe kipofu. Nikiri toka mwanzo:
1. Kuwa napenda sana usiri huwa sipendi kabisaa mgeni anapoingia kwenye nyumba yangu aone mpangilio wa vyumba anapoenda public toilet.
2. Sikutaka kabisaa kuweka vyumba vya kulala/jiko upande wenye jua mchana/jioni maana kwa sasa mpangilio huo unanitesa sana mimi na wanangu yaani mchana/jioni kulala mtihani. Upande wenye jua mchana nimeplan kuwe na dining, public toilet, ngazi za kupandia ghorofani, laundry na prayer/office/study maana ni locations ambazo watu hawakai muda mrefu wakati jua linapiga uelekeo huo. Kwenye study/prayer/office room nitaweka A/C. Watoto watasomea vyumbani.
3. Kiwanja ni chembamba kina urefu 25 upana 15.5 na ni flat kabisaa.
4. Idea ya open kitchen mpishi mkuu kaikataa so ndo maana kitchen ipo kizamani!!!
5. Nitajenga chumba cha nje kidogo incase mgeni wa kiume kaja.

Kwa unyenyekevu mkubwa sana na kwa moyo wa shukrani natanguliza shukrani zangu za dhati kwa wote mtakaoguswa kunishauri. Mungu awabariki sana kwa kutoa muda na maarifa yenu kunisaidia ili nisirudie tena makosa yaliyofanyika kwenye nyumba ya kwanza. Ahsanteni sana.
Wastani wa dimensions za vyumba katika mita kumbuka ramani ina vipimo katika sentimeta
Ground
1.Kibaraza mbele ya nyumba mita 1.5 x 3.5
2.Sebule mita 6.5 x 4.3
3.Dining mita 3.5 x 4.3
4.Kibaraza mbele ya jiko mita 5.6 x 1
3.Kitchen mita 4 x 3.3
4.Store mita 3.3 x 1.6
5.Laundry 4.4 x 3.2
6.Public toilet 1.4 x 4
7.Ngazi za kupandia ghorofani upana mita 1.4/1.3 urefu itategemea na ushauri/design ya mchoraji ila choo public lazima kikae chini ya ngazi za kupandia ghorofani na lazima kikae ukutani ili kiwe na dirisha na tolet sink itokelezee ukutani kurahisiha flow ya taka.
8. Master bedroom ya mgeni wa kike/dada wa kazi mita 4.2 x mita 4.6

1st FLOOR
1.Master bedroom wazazi mita 4 x 5.1
2.Choo master wazazi mita 1.3 x 5.5

3.Masterbedroom watoto wa kike 5.5 x 4.18
4.Choo master watoto wa kike mita 2 x 4.1

5.Master bedroom mtoto wa kiume mita 4 x 5.5 i.e. kuna SQM kidogo sana zitapungua sababu ya kona kwenye mlango wa chumba cha watoto wa kike.
6.Choo master bedroom mtoto wa kiume 1.3 x 5.5

4. Small study/office/prayer room mita 4 x 2.1
5.korido ya ngazi za kupandia/kushukia ghorofani ukubwa utategemea design
6. Balcony mbele ya nymba mita 1.7 (japo itaongeza to 2) x 3.5 kwa sasa kuna mkanganyiko wa vipimo but that's rough idea.

ramani.jpg
 
Kuna nyumba moja nilienda kurekebisha kitu , ile ramani ya ile nyumba inausiri mno, unaingikia hapa unatokea pale kurudi hujui upite wapi, kwa ufupi haikaririki.
Nimependa hapo uliposema unapenda usiri , sio kila mtu anajua master ile pale unaingia hapa unatokea pale.

Rmani nzuri ila pata mtaamu kuna vya kuweka sawa na kubadilisha bila kuathiri matakwa yako.
 
Chukua ushauri huo
  1. Kama una hela za kutosha tumia mtindo wa contemporary kwenye kusanifu ramani then kupaua hii nyumba yako elewa na zingatia neno kama una hela maana contemporary inahitaji hela ili isivuje na inahitaji Engineer/Technician/Fundi maiko anayejua kuzijenga sio ilimradi uokote tu fundi kisa urahisi wa bei utarudi tena hapa kuomba ushauri.
  2. Kama utapaua kwa mtindo usio contemporary basi tafuta fundi mzuri yaan pro. Ndo aipaue hii nyumba maana haina konakona kwa nje hivyo kuna hatari ya fundi kama sio mzoefu akaipaua ka shule ya kata na ikachukiza maana ramani yako imekaa ka box la maziwa ya asas.
  3. Hakikisha unamuona plumber pro. kabla hujampa msanifu akuchoree akushauri kwenye ramani hii hii kuhusu plumbing drawings/designing kwa mfano ili ghorofani mpate maji yenye pressure ya kutosha inabidi ujue tanki la maji litawekwa wapi usije fikiri hiyo ni issue ya Architect.
  4. Kabla hujafanya decision kuhusu kuweka grill windows then madirisha aluminium hebu nenda site siku moja wakati usio na jua uone if arrangement ya madirisha iko okay na hamna giza kumbuka raman yako kwa ndan ina konakon hii ina madhara kuleta giza mchana.
  5. Chumba cha wazazi kipo upande wa jikon ujiandae na kelele za mpishi/wapishi na za watu wengine mfano wauza mboga. Kingine upande ulipoweka hii master BR. yako wakat unamdo nkeo ka ni nchana bachi ntu wa jikoni atasikia labda ka nkeo si ntu wa kupiga makelele hata ukindo usiku ntoto wa kiume atajua mama yake leo anakula nkuyenge.
  6. Ramani yako inaonyesha upande wa jikoni kutakuwa na chemba nyingi na nadhani septic tank itakaa upande huohuo hivyo patakuwa busy kudeal na taka ushauri kuwa; makini sana umpate plumber pro. ili akutengenezee mfumo wa kueleweka na usiwe mbahili wa kununua vifaa bora maana ukikosea hapo daily upande wa jikoni utakuwa unaishi na harufu mbaya za vima na jokoim (soma from right) naona umemtag huyu plumber hydrogen atakusaidia zaid. Niliwahi kuona fundi mmoja akimshauri mtu ambapo chemba zilikaa kinyume upande mwingine na zilipotakiwa kuwa lengo ilikuwa kuondoa hiyo athari niliyosema hapo sijui kama hii ilifaa au vipi.
  7. We na nkeo mtakapokuwa wazee definitely mtapenda sana kukaa chumba cha chini ila bado mnaweza funga zile lift za kituruki au kichina kwa hiyo design vizuri hizo ngazi tokea sasa ili baadae au now ziweze kuakomodate ufungaji wa hizo lift.
Otherwise hii ramani sio mbaya kihivyo na ukizingatia imechorwa na mtu asiye Architect hongera.
 
Huo upande wenye jiko bila shaka ndo upande ambao wakati wote utakuwa na kelele za watu mbalimbali mfano mkeo na mashosti zake, watoto wako, dada wa kazi watu wanaoingia na kutoka mfano majirani, wauza vitu wa mtaani automatically hii inapelekea wewe ukiwa kwenye room yako ghorofani kupigiwa makelele yes umekwepa jua but ujiandae na kelele kwa kuwa kiwanja chako ni chembamba nashindwa namna ya kukushauri uweke wapi chumba chako but Architect wako atakushauri zaidi.
 
Habari ndugu wana Jamii Forums,
Nipo kwenye mchakato wa kumtafuta msanifu majengo anichoree ramani ya nyumba ya kuishi familia ghorofa moja ndogo simple isiyo na makorokoro mengi maana kiwanja ni kidogo.

Nyumba yangu ya kwanza, msanifu majengo mweledi kabisa alitumika na bado chumba ninacholala na cha mtoto wa kiume vipo uelekeo ambao mchana hakulaliki sababu ya jua. Alikosea location ya public toilet matokeo yake public toilet ipo karibu (korido uelekeo) kabisaaa na masterbedeoom yangu i.e. no privacy!. Kulikuwa na makosa mengine pia lakini tuyaache.

Mawazo yangu ni kuwa ukubwa wa sehemu mbalimbali kwa wastani utakuwa kama nilivyoainisha hapo chini kwenye ukubwa huu nimezingatia kuwa mbele nipate sehemu ya kupark magari na pia kukaa na wanaume wenzangu hasa upande wa uelekeo wa dining-nitapanda miti kwa ajili yakivuli Upande wa uelekeo wa jiko kutakuwa na nafsi ya gari kupita.

Nimesketch ramani hapo chini ambapo nimeweka mawazo yangu namna ninaona mpangilio wa vyumba/ukubwa uwe ikiwa na maana pindi nitakapo mpa msanifu majengo hayo ndo yatakuwa mawazo yangu nitakayomwambia bila shaka najua atanishauri vingine vingi tu maana yeye ndo mtaalamu lakini nimetaka nisiwe kipofu. Nikiri toka mwanzo:
1. Kuwa napenda sana usiri huwa sipendi kabisaa mgeni anapoingia kwenye nyumba yangu aone mpangilio wa vyumba anapoenda public toilet.
2. Sikutaka kabisaa kuweka vyumba vya kulala/jiko upande wenye jua mchana/jioni maana kwa sasa mpangilio huo unanitesa sana mimi na wanangu yaani mchana/jioni kulala mtihani. Upande wenye jua mchana nimeplan kuwe na dining, public toilet, ngazi za kupandia ghorofani, laundry na prayer/office/study maana ni locations ambazo watu hawakai muda mrefu wakati jua linapiga uelekeo huo. Kwenye study/prayer/office room nitaweka A/C. Watoto watasomea vyumbani.
3. Kiwanja ni chembamba kina urefu 25 upana 15.5 na ni flat kabisaa.
4. Idea ya open kitchen mpishi mkuu kaikataa so ndo maana kitchen ipo kizamani!!!
5. Nitajenga chumba cha nje kidogo incase mgeni wa kiume kaja.

Wafuatao naombeni ushauri wenu sehemu za kuboresha kwenye haya mawazo yangu. Naomba niwatag wafuatao maana huwa mnawasaidia sana watu wenye uhitaji wa ushauri kuhusu ramani za nyumba. Please! Haina maana kama sijaweka jina usinishauri please!
Hechy Essy , greater than , HENRY14 , Scale , Glenn , Bemendazole , conductor , Njuka II, Equation x funzadume, ARV AH architectural , Nile_house_designs ,Mnyiramba OKW BOBAN SUNZU Qs Cathbert Frank mtanganyika plumber hydrogen

Kwa unyenyekevu mkubwa sana na kwa moyo wa shukrani natanguliza shukrani zangu za dhati kwa wote mtakaoguswa kunishauri. Mungu awabariki sana kwa kutoa muda na maarifa yenu kunisaidia ili nisirudie tena makosa yaliyofanyika kwenye nyumba ya kwanza. Ahsanteni sana.

Wastani wa dimensions za vyumba katika mita kumbuka ramani ina vipimo katika sentimeta
Ground
1.Kibaraza mbele ya nyumba mita 1.5 x 3.5
2.Sebule mita 6.5 x 4.3
3.Dining mita 3.5 x 4.3
4.Kibaraza mbele ya jiko mita 5.6 x 1
3.Kitchen mita 4 x 3.3
4.Store mita 3.3 x 1.6
5.Laundry 4.4 x 3.2
6.Public toilet 1.4 x 4
7.Ngazi za kupandia ghorofani upana mita 1.4/1.3 urefu itategemea na ushauri/design ya mchoraji ila choo public lazima kikae chini ya ngazi za kupandia ghorofani na lazima kikae ukutani ili kiwe na dirisha na tolet sink itokelezee ukutani kurahisiha flow ya taka.
8. Master bedroom ya mgeni wa kike/dada wa kazi mita 4.2 x mita 4.6

1st FLOOR
1.Master bedroom wazazi mita 4 x 5.1
2.Choo master wazazi mita 1.3 x 5.5

3.Masterbedroom watoto wa kike 5.5 x 4.18
4.Choo master watoto wa kike mita 2 x 4.1

5.Master bedroom mtoto wa kiume mita 4 x 5.5 i.e. kuna SQM kidogo sana zitapungua sababu ya kona kwenye mlango wa chumba cha watoto wa kike.
6.Choo master bedroom mtoto wa kiume 1.3 x 5.5

4. Small study/office/prayer room mita 4 x 2.1
5.korido ya ngazi za kupandia/kushukia ghorofani ukubwa utategemea design
6. Balcony mbele ya nymba mita 1.7 (japo itaongeza to 2) x 3.5 kwa sasa kuna mkanganyiko wa vipimo but that's rough idea.

View attachment 2950029
Awali ya yote,Heri ya Pasaka
Pongezi kwa kuweza kuunganisha na kuwasilisha mawazo yako katika mchoro,big up.
Ila kuna vitu kadhaa havijaa kaa sawa, ntaviorodhesha vichache tu.

MAIN ENTRY/MLANGO MKUU
1.Umeuweka Dinning : watu wanakula wengine waingie ama kutoka...
2.Mda wa kula viti vinarudi nyuma, nafasi ya kupita inakuwa ndogo.
3.Kupitia hapo unampa mtu nafasi ya kuona vyumba vitatu kwa wakati mmoja mpaka kufika kukaa sebureni, no privacy hapo.

CIRCULATION/MZUNGUKO WA WATU
1.Mpangilio wako unaweka mkanganyiko kwenye movement.
2.Kuingia tu ndani,njia zimegawanyika, Kile kichumba cha Jokofu nacho kinaleta mkanganyiko,mtu anapinda kona unnecessary.
3.Kwenye hali ya hatari kutoka Ghorofani mpaka kufika mlangoni itakuwa kimbembe

NGAZI
1.Ngazi inatakiwa ikae sehem rahisi kwa mtu kui-access,
2.Kwenye floor ya pili ngazi inakula nafasi yote ya korido.

COLUMNS
1.Kwasasa haujaweka nguzo hata moja,
2.Tarajia mabadiliko kadhaa pindi mapendekezo ya nguzo na beams yakihusishwa

MADIRISHA
1.Kuna madirisha kadhaa ni madogo kuliko ilivyopaswa
2.Madirisha kadhaa hayaja zingatia suala la mwanga ndani ya jengo.

Kwasasa ni hayo tu.
 
Wachoraji ni wengi ila wanaozingatia misingi ya uchoraji ni wachache, kabla hujampa mtu kazi ya kuchora muombe akupatie sample hata sketch tu za kazi alizofanya ili ujiridhishe kwanza.

Kuhusu directions za vyumba, sebule, jiko n.k nilivielezea kwenye uzi wangu (sikumbuki ni comment no ngapi, ngoja nikusaidie kuitafuta nikuletee)

Kwa ramani ya ghorofa ni vizuri ukatafuta engineer ambaye anaweza kuchora michoro ya architectural na structural pia, vinginevyo ndio utakuta architect amedesign hivi na engineer nae akamcrash architect kwamba haikupaswa kuwa hivi (wakati huo architect umeshamlipa pesa yake, na ukimuomba arekebishe anadai pesa nyingine ya usumbufu)

Mimi yangu ni hayo mkuu, na ninashukuru sana kwa kunitag katika uzi wako
 
Hechy Essy shukran sana mkuu kwa ushauri sure utakuwa umenisaidia sana ukiniletea hii "Kuhusu directions za vyumba, sebule, jiko n.k"
 
Awali ya yote,Heri ya Pasaka
Pongezi kwa kuweza kuunganisha na kuwasilisha mawazo yako katika mchoro,big up.
Ila kuna vitu kadhaa havijaa kaa sawa, ntaviorodhesha vichache tu.

MAIN ENTRY/MLANGO MKUU
1.Umeuweka Dinning : watu wanakula wengine waingie ama kutoka...
2.Mda wa kula viti vinarudi nyuma, nafasi ya kupita inakuwa ndogo.
3.Kupitia hapo unampa mtu nafasi ya kuona vyumba vitatu kwa wakati mmoja mpaka kufika kukaa sebureni, no privacy hapo.

CIRCULATION/MZUNGUKO WA WATU
1.Mpangilio wako unaweka mkanganyiko kwenye movement.
2.Kuingia tu ndani,njia zimegawanyika, Kile kichumba cha Jokofu nacho kinaleta mkanganyiko,mtu anapinda kona unnecessary.
3.Kwenye hali ya hatari kutoka Ghorofani mpaka kufika mlangoni itakuwa kimbembe

NGAZI
1.Ngazi inatakiwa ikae sehem rahisi kwa mtu kui-access,
2.Kwenye floor ya pili ngazi inakula nafasi yote ya korido.

COLUMNS
1.Kwasasa haujaweka nguzo hata moja,
2.Tarajia mabadiliko kadhaa pindi mapendekezo ya nguzo na beams yakihusishwa

MADIRISHA
1.Kuna madirisha kadhaa ni madogo kuliko ilivyopaswa
2.Madirisha kadhaa hayaja zingatia suala la mwanga ndani ya jengo.

Kwasasa ni hayo tu.
greater than ahsante sana kwa ushauri wako mkuu shukran
 
Huo upande wenye jiko bila shaka ndo upande ambao wakati wote utakuwa na kelele za watu mbalimbali mfano mkeo na mashosti zake, watoto wako, dada wa kazi watu wanaoingia na kutoka mfano majirani, wauza vitu wa mtaani automatically hii inapelekea wewe ukiwa kwenye room yako ghorofani kupigiwa makelele yes umekwepa jua but ujiandae na kelele kwa kuwa kiwanja chako ni chembamba nashindwa namna ya kukushauri uweke wapi chumba chako but Architect wako atakushauri zaidi.
hayacola ahsante sana una point nafikiria kuhamisha jiko liwe pale kwenye laundry room.
 
Chukua ushauri huo
  1. Kama una hela za kutosha tumia mtindo wa contemporary kwenye kusanifu ramani then kupaua hii nyumba yako elewa na zingatia neno kama una hela maana contemporary inahitaji hela ili isivuje na inahitaji Engineer/Technician/Fundi maiko anayejua kuzijenga sio ilimradi uokote tu fundi kisa urahisi wa bei utarudi tena hapa kuomba ushauri.
  2. Kama utapaua kwa mtindo usio contemporary basi tafuta fundi mzuri yaan pro. Ndo aipaue hii nyumba maana haina konakona kwa nje hivyo kuna hatari ya fundi kama sio mzoefu akaipaua ka shule ya kata na ikachukiza maana ramani yako imekaa ka box la maziwa ya asas.
  3. Hakikisha unamuona plumber pro. kabla hujampa msanifu akuchoree akushauri kwenye ramani hii hii kuhusu plumbing drawings/designing kwa mfano ili ghorofani mpate maji yenye pressure ya kutosha inabidi ujue tanki la maji litawekwa wapi usije fikiri hiyo ni issue ya Architect.
  4. Kabla hujafanya decision kuhusu kuweka grill windows then madirisha aluminium hebu nenda site siku moja wakati usio na jua uone if arrangement ya madirisha iko okay na hamna giza kumbuka raman yako kwa ndan ina konakon hii ina madhara kuleta giza mchana.
  5. Chumba cha wazazi kipo upande wa jikon ujiandae na kelele za mpishi/wapishi na za watu wengine mfano wauza mboga. Kingine upande ulipoweka hii master BR. yako wakat unamdo nkeo ka ni nchana bachi ntu wa jikoni atasikia labda ka nkeo si ntu wa kupiga makelele hata ukindo usiku ntoto wa kiume atajua mama yake leo anakula nkuyenge.
  6. Ramani yako inaonyesha upande wa jikoni kutakuwa na chemba nyingi na nadhani septic tank itakaa upande huohuo hivyo patakuwa busy kudeal na taka ushauri kuwa; makini sana umpate plumber pro. ili akutengenezee mfumo wa kueleweka na usiwe mbahili wa kununua vifaa bora maana ukikosea hapo daily upande wa jikoni utakuwa unaishi na harufu mbaya za vima na jokoim (soma from right) naona umemtag huyu plumber hydrogen atakusaidia zaid. Niliwahi kuona fundi mmoja akimshauri mtu ambapo chemba zilikaa kinyume upande mwingine na zilipotakiwa kuwa lengo ilikuwa kuondoa hiyo athari niliyosema hapo sijui kama hii ilifaa au vipi.
  7. We na nkeo mtakapokuwa wazee definitely mtapenda sana kukaa chumba cha chini ila bado mnaweza funga zile lift za kituruki au kichina kwa hiyo design vizuri hizo ngazi tokea sasa ili baadae au now ziweze kuakomodate ufungaji wa hizo lift.
Otherwise hii ramani sio mbaya kihivyo na ukizingatia imechorwa na mtu asiye Architect hongera.
salari shukran sana mkuu kwa ushauri wako mkuu
 
Habari ndugu wana Jamii Forums,
Nipo kwenye mchakato wa kumtafuta msanifu majengo anichoree ramani ya nyumba ya kuishi familia ghorofa moja ndogo simple isiyo na makorokoro mengi maana kiwanja ni kidogo.

Nyumba yangu ya kwanza, msanifu majengo mweledi kabisa alitumika na bado chumba ninacholala na cha mtoto wa kiume vipo uelekeo ambao mchana hakulaliki sababu ya jua. Alikosea location ya public toilet matokeo yake public toilet ipo karibu (korido uelekeo) kabisaaa na masterbedeoom yangu i.e. no privacy!. Kulikuwa na makosa mengine pia lakini tuyaache.

Mawazo yangu ni kuwa ukubwa wa sehemu mbalimbali kwa wastani utakuwa kama nilivyoainisha hapo chini kwenye ukubwa huu nimezingatia kuwa mbele nipate sehemu ya kupark magari na pia kukaa na wanaume wenzangu hasa upande wa uelekeo wa dining-nitapanda miti kwa ajili yakivuli Upande wa uelekeo wa jiko kutakuwa na nafsi ya gari kupita.

Nimesketch ramani hapo chini ambapo nimeweka mawazo yangu namna ninaona mpangilio wa vyumba/ukubwa uwe ikiwa na maana pindi nitakapo mpa msanifu majengo hayo ndo yatakuwa mawazo yangu nitakayomwambia bila shaka najua atanishauri vingine vingi tu maana yeye ndo mtaalamu lakini nimetaka nisiwe kipofu. Nikiri toka mwanzo:
1. Kuwa napenda sana usiri huwa sipendi kabisaa mgeni anapoingia kwenye nyumba yangu aone mpangilio wa vyumba anapoenda public toilet.
2. Sikutaka kabisaa kuweka vyumba vya kulala/jiko upande wenye jua mchana/jioni maana kwa sasa mpangilio huo unanitesa sana mimi na wanangu yaani mchana/jioni kulala mtihani. Upande wenye jua mchana nimeplan kuwe na dining, public toilet, ngazi za kupandia ghorofani, laundry na prayer/office/study maana ni locations ambazo watu hawakai muda mrefu wakati jua linapiga uelekeo huo. Kwenye study/prayer/office room nitaweka A/C. Watoto watasomea vyumbani.
3. Kiwanja ni chembamba kina urefu 25 upana 15.5 na ni flat kabisaa.
4. Idea ya open kitchen mpishi mkuu kaikataa so ndo maana kitchen ipo kizamani!!!
5. Nitajenga chumba cha nje kidogo incase mgeni wa kiume kaja.

Kwa unyenyekevu mkubwa sana na kwa moyo wa shukrani natanguliza shukrani zangu za dhati kwa wote mtakaoguswa kunishauri. Mungu awabariki sana kwa kutoa muda na maarifa yenu kunisaidia ili nisirudie tena makosa yaliyofanyika kwenye nyumba ya kwanza. Ahsanteni sana.
Wastani wa dimensions za vyumba katika mita kumbuka ramani ina vipimo katika sentimeta
Ground
1.Kibaraza mbele ya nyumba mita 1.5 x 3.5
2.Sebule mita 6.5 x 4.3
3.Dining mita 3.5 x 4.3
4.Kibaraza mbele ya jiko mita 5.6 x 1
3.Kitchen mita 4 x 3.3
4.Store mita 3.3 x 1.6
5.Laundry 4.4 x 3.2
6.Public toilet 1.4 x 4
7.Ngazi za kupandia ghorofani upana mita 1.4/1.3 urefu itategemea na ushauri/design ya mchoraji ila choo public lazima kikae chini ya ngazi za kupandia ghorofani na lazima kikae ukutani ili kiwe na dirisha na tolet sink itokelezee ukutani kurahisiha flow ya taka.
8. Master bedroom ya mgeni wa kike/dada wa kazi mita 4.2 x mita 4.6

1st FLOOR
1.Master bedroom wazazi mita 4 x 5.1
2.Choo master wazazi mita 1.3 x 5.5

3.Masterbedroom watoto wa kike 5.5 x 4.18
4.Choo master watoto wa kike mita 2 x 4.1

5.Master bedroom mtoto wa kiume mita 4 x 5.5 i.e. kuna SQM kidogo sana zitapungua sababu ya kona kwenye mlango wa chumba cha watoto wa kike.
6.Choo master bedroom mtoto wa kiume 1.3 x 5.5

4. Small study/office/prayer room mita 4 x 2.1
5.korido ya ngazi za kupandia/kushukia ghorofani ukubwa utategemea design
6. Balcony mbele ya nymba mita 1.7 (japo itaongeza to 2) x 3.5 kwa sasa kuna mkanganyiko wa vipimo but that's rough idea.

View attachment 2950029
Awali ya yote nikupongeze na kukushukuru Kwa kuwa mjenzi mwenye akili na busara umekuwa mtu wa maana sana kwa kutoa design conceptualization ya unacho hitaji.

Pili, pole sana kwa changamoto uliyo ipata na unayo ipitia kwa sasa.
Nafikiri it is our time as Professionals to walk through your ideas and to challenge it and to modify and to advise. And finally to come up with drawings.

Naamini hakuna kinacho shindikana katika ujenzi ilhali akili imepewa ruhusa ya kufikiri. We need some time to think and work for it.

Kwa kuwa hili ni jukwaa huru hebu na sisi kama Limbu Nation Builders tuwe katika Mwendo wa ideas zako then we’ll share the story.

I’m really proud of you, kwasababu wewe ni miongoni mwa wajenzi wachache kuwahi kutokea nchini Kwani unajua unacho taka, I believe your ideas plus ours tutapata kitu bora sana.

Ninakuahidi kuja na implementations za mawazo yako very soon.

0621003092 (it is my WhatsApp number)
 
Attachments

  • B5D5F4DA-0BE2-45DE-9F10-D0044C589B85.png
    B5D5F4DA-0BE2-45DE-9F10-D0044C589B85.png
    716.1 KB · Views: 29
Mimi sio mtaalamu wa majengo kwa namna yoyote ile ila kuna vitu siku kipenda kwenye mchoro wako.
Kwenye vyumba vya watoto wa kiume na wakike, pia master.

Kwanini watoto wa kike na wakiume wasiwe na vyoo na sehemu ya kuoga tofauti?

Sifahamu wana umri gani, lakini mimi binafsi napenda hizo sehemu zijitegemee, wakikua wakubwa kuna kuwa hakuna usiri kwao wote.

Pia wakikua ki umri wakaondoka, au hata kama ni wageni au hao hao watoto wakija/wakirudi nyumbani kwa wazazi kutembea watahitaji usiri pia.

Hivyo mi naona huo muingiliano wa vyoo na bafu ungetafuta namna uka weka mipaka ya kudumu.

Na kuhusu Master kuwa na muingiliano na vyumba vya watoto sioni kama ni sawa, hasa wanapo anza kupevuka, hawahitaji hata kuhisi huko kwa wazazi kuna nini kinafanyika.

Ukijenga wangali wadogo unakuwa unawaza usalama wao hivyo unataka uwe na sehemu ya haraka kuwatizama, lakini wakikua ki umri hawahitaji muingiliano huo, na kama unajenga nyumba zetu hizi za kudumu yani tofari na cement au concrete inakuwa siyo rahisi kubadirisha muundo huko mbeleni.

Ungekuwa unajenga nyumba za mbao kam za ulaya, ungeweza kuacha ilivyo baadaye uka ziba au kubadili muundo.

Huo ni mtizamo wangu, kwamba Master ikae mbali na vyumba vya watoto,. Kwasababu hawataishi nawe milele, na wakiondoka matumizi yatabadirika vitakuwa vya wageni, ndugu rafiki au wao hao wakija kukutembelea wakiwa watu wazima.
 
Back
Top Bottom