Mbowe, Lissu tunawapa pole za kupigwa risasi na kufilisiwa lakini hii struggle siyo ya watu binafsi sababu kuna watu wamekufa kabisa kwa ajili ya mapambano ya kuitoa CCM. Je hao utawambia nini familia zao? Viongozi wa sasa hawana mbinu, ari wala mikakati ya kiuhalisia wakuitoa CCM. Wakina Mwakubusi wanajaribu kuratibu maandamano na civil disobedience na hiyo ndio lugha CCM wanaelewa na kuogopa. Hivi nyie mnawezaje kuwa waastarabu kwa watu wanaoiba kura mchana kweupe huko Zanzibar na mkaamini watabadilika na kuwa waastarabu? Eti unaongelea vyuo vya Uongozi, Diplomacy una akili kweli wewe? Unapambana na mhuni wa Mbagala kwa technique za Oysterbay.