Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Sijaelewa kwa nini [HASHTAG]#elitegwe[/HASHTAG] umekazana kuutetea upuuzi katika kila uzi uuletao?
 
Kiukweli Mhe Makonda kaonesha njia na kutusaidia kujua kuwa katika jamii yetu kumbe hali ipoje na kama hatutachukua hatua nini kitatokea mbele,hao wanao lalamika wajiulize nini wamefanya katika kutatua shida za wananchi wao katika maeneo yao! yeye amefanya kwa upande wake na wao wafanye nasiyo kumkatisha tamaa
 
Sawa ndio hajafuata utaratiba kama unavyotaka ,je nyinyi mnaojuwa utaratibu kuna juhudi zozote ambazo mmezifanya kuonesha mnataka kuondoa tatizo la wanawake waliotelekezwa?.
 
Wanasema eti Makonda anaingilia uhuru/anavunja faragha, nadhani kila kiongozi anayempinga Makonda ajitafakari sana.

Kwa sababu suala la kuwa na mtoto siyo faragha tena. Kama mimba haikuweza kufichwa na kuwa faragha sembuse mtoto ambaye ni kiumbe hai anatembea???

Usitawi wa jamii kupitia Waziri Ummy hawafanyi kazi yao!
 
Wewe inaonekana mama yako anafanya kazi huko. Watumishi wa ustawi wa jamii kazi yao ni- ku enforce law, na kushauri serikali kama sheria zilizopo zinaendana na muda, ili serikali ione umuhimu wa kufanya amendments. Tunategemea basi hata kuona hata hilo linafanyika kabla hawajaenda kwenye broad programs ambazo zinahitaji fedha nyingi
 
Bashite atakua na mayai ya kware ndio mana hana mtoti
 
Mod One nisaidie kudelete hii post
 
Naomba kufahamishwa: Hivi watetezi wa Makonda wanafahamu kinachopingwa hasa ni nini kwenye hili zoezi?
 
Wana JF.

Ni mwaka sasa tangu mpambanaji mashuhuri Mh. Paulo Makonda ataje orodha ndefu ya wanaotuhumiwa kuendesha mihadharati. Wengi wamekamatwa na kufikikishwa mbele ya sheria. Kuna wengine walikiri wakaachwa kuna wengine wanakabiliana na kesi zao. Kuna wengine orodha ya tatu ambayo tuliadiwa haikutajwa kutokana na kuteuliwa kwa mhusika mkuu wa kupambana na mihadharati. Kuna wengine waliitwa na kamati fulani na kuojiwa lakini hatukupata matokeo kwani ilikuwa faragha muno.

Lakini cha muhimu zaidi kuna watu walitajwa sana na Mange Kimambi hii list haikuguswa wala kuchukuliwa hatua mpaka sasa. Wengi wao walikuwa wamekimbilia SouthAfrica sasa wamerudi wanakula bata kwa sana. Wengine waliwahi kutuhumiwa na Mwakyembe lakini hadi leo wapo mitaani. Wengine ni wabunge mpaka sasa. Je, hii vita imeisha? Mbona sasa mateja wameanza kuongezeka kwa kasi. Ukienda mwananyamala wapo wengi wanaoomba kutibiwa. Sasa kama yameisha si ndio tiba tayari. Pengine tuangalie tena upya wa uswahiba uliopo kati ya viongozi waliopo na wauza ngada ndio kinaweza kuwa kikwazo kipya. Ukienda posta utaambiwa unga ndio kwanza umepanda bei kwani waletaji wanatumia njia ile ile ila gharama ya kuvusha kubwa.
 
Jamaa kafanikiwa sana Kwa kuweza kusurvive ishu yake ya kufoji vyeti.
Suala lake lipo wazi
Watu wamesoma naye mwanza sec akitumie jina la daudi bashite.
Matokeo yake mwanza sec yanajulikana alipata zero.
Hongera sana ZERO IN PAPER ZERO IN BRAIN
Kweli unampa nyama tamu ya ulimi mzee mbaba JIWE
 
Yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Basi. hayo mengine ni kimbelembele chake tu. Yote anayofanya kuna watu wameajiriwa kwa ajili ya hayo. Pia kuna kazi za jiji na halmashauri zake na siyo kazi za mkuu wa mkoa. Watu wanapotosha lakini ukweli ni kwamba watumishi wa umma ngazi ya mkoa wapo chini ya RAS na siyo RC. RC ni siasa tupu na ni cheo cha kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…