Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Kuna mambo ni madogo lakini yanakera sana hasa uvutaji sigara hadharani. kama tukiwa serious jambo hili linaweza kumalizwa ndani ya muda mfupi sana.mimi namuunga mkono kwasababu anataka kuleta ustaarabu! siyo kila mahali unakuta mtu anavuta misigara yake.

Ama kuhusu mashoga, dawa ni nyepesi tu ni kuweka adhabu kali kwa wateja wao wakikamatwa walipishwe shs mil kadhaa wakishindwa wafanye kazi ya kusafisha mitaro michafu na kusaidia kuzoa taka kwa muda wa miezi mitatu.
Sigara sawa lakini sio swala la ushoga. Hilo ni swala la Mungu na sio swala la Makonda. Kuna watu wameumbwa hivyo. Sikutaka kuamini lakini ndiyo hivyo. Lazima tukubali na lazima lipokelewe kidini pia.
 
Wana JF.

Ni mwaka sasa tangu mpambanaji mashuhuri Mh. Paulo Makonda ataje orodha ndefu ya wanaotuhumiwa kuendesha mihadharati. Wengi wamekamatwa na kufikikishwa mbele ya sheria. Kuna wengine walikiri wakaachwa kuna wengine wanakabiliana na kesi zao. Kuna wengine orodha ya tatu ambayo tuliadiwa haikutajwa kutokana na kuteuliwa kwa mhusika mkuu wa kupambana na mihadharati. Kuna wengine waliitwa na kamati fulani na kuojiwa lakini hatukupata matokeo kwani ilikuwa faragha muno.

Lakini cha muhimu zaidi kuna watu walitajwa sana na Mange Kimambi hii list haikuguswa wala kuchukuliwa hatua mpaka sasa. Wengi wao walikuwa wamekimbilia SouthAfrica sasa wamerudi wanakula bata kwa sana. Wengine waliwahi kutuhumiwa na Mwakyembe lakini hadi leo wapo mitaani. Wengine ni wabunge mpaka sasa. Je, hii vita imeisha? Mbona sasa mateja wameanza kuongezeka kwa kasi. Ukienda mwananyamala wapo wengi wanaoomba kutibiwa. Sasa kama yameisha si ndio tiba tayari. Pengine tuangalie tena upya wa uswahiba uliopo kati ya viongozi waliopo na wauza ngada ndio kinaweza kuwa kikwazo kipya. Ukienda posta utaambiwa unga ndio kwanza umepanda bei kwani waletaji wanatumia njia ile ile ila gharama ya kuvusha kubwa.
Hilo sasa sio swala la Makonda. Mwulizeni Rais na watu alio wateua. Makonda alionyesha kifua mka gomba mkamnyang'anya madaraka. Sasa hangaikeni na mnao waita smart guys wa kutatua matatizo ya madawa ya kulevya.

Acheni unafiki na fitina. Hamkutaka seriously hilo jambo kutatuliwa. Mngetaka Makonda angeweza kwa namna fulani. Alichotakiwa kuwa nacho ni support yetu na vifaa vya kutosha kutoka serikalini.
 
Kumbe makonda ana mayai? Means ana Ovary...eti!
Elimu ya chekechea hiyo. Nashangaa ubunge wake ameupata vipi?

Hata haibu hatuna watu wazimaa tuna waacha standard seven Leavers kututungia sheria? Mbona vichekesho?
 
Wanasema eti Makonda anaingilia uhuru/anavunja faragha, nadhani kila kiongozi anayempinga Makonda ajitafakari sana.

Kwa sababu suala la kuwa na mtoto siyo faragha tena. Kama mimba haikuweza kufichwa na kuwa faragha sembuse mtoto ambaye ni kiumbe hai anatembea???

Usitawi wa jamii kupitia Waziri Ummy hawafanyi kazi yao!
Ndiyo mambo Rais kila wakati anaimba. Ni watu wasio jua wajibu wao. Sielewi kwa nini hao watu wako huko.
 
Hilo sasa sio swala la Makonda. Mwulizeni Rais na watu alio wateua. Makonda alionyesha kifua mka gomba mkamnyang'anya madaraka. Sasa hangaikeni na mnao waita smart guys wa kutatua matatizo ya madawa ya kulevya.

Acheni unafiki na fitina. Hamkutaka seriously hilo jambo kutatuliwa. Mngetaka Makonda angeweza kwa namna fulani. Alichotakiwa kuwa nacho ni support yetu na vifaa vya kutosha kutoka serikalini.
Hahahhh kuna watu buaaaana
Huyu bashite mwenye kufanya kila jambo kisiasa zaidi hawezi kufanikiwa
He is not serious yeye kama yeye. Anafanya yote kujinufaisha kibiashara na kisiasa bahati mbaya au nzuri anafanikiwa kujijenga kibiashara lakini kujibomoa kunakuja akitoka madarakani aliowadhulumu watakula sahani moja.
Wasifanye mambo kwa mihemko visasi wafanye kwa weledi watafanikiwa.
 
Ndugu yangu umeandika kwahisia sn ili kutetea upuuzi! mfumo pekee wa kuwakomboa kina mama na jamii nzima ni uislam pekee hivyo mfumo wowote utakaotumika ni batili na ni dhuluma kwa wanadamu,sasa unasema mke mmoja mme mmoja kwa mifumo ya kikafir hlf yasitokee madhara ya watoto wa mtaan tunaishi ktk kipindi wanawake na mabint wanatembea uchi na wanadhurula hovyo ambapo uhuru ndo sera ya mfumo ,sasa kwann uzinifu usiendelee na hatmaye madhara tunayaona kwenye matelevisheni kwahy sifu utakavyosifu hakuna suluhisho mpaka tutakaporejea kwa ALLAH!

Kweli Allah alikuumba wewe na nguo. Kajiangalie kwenye kioo utaona kazi ya Allah.
 
Asilimia kubwa ya viongozi wa Tanzania ni useless, wakiona mwenzao anafanya jambo la maana wao watataka kukosoa tu ili wapate kusikika mitaani na kusifiwa kwani jamii kubwa ya watanzania wanapenda sana kusilikiliza ujinga na kufanya kuwa habari mpya ya mjini. Bado tuna kazi sana ya kuelekea 2020, wacha tu Mh. rais atunyooshe ili ujinga ufutike kabisa. Nyerere alijitahidi kutufuta ujinga na ukatoweka kiasi fulani hivi.....kina Mwinyi, Mkapa, Kikwete wakaturudishia kwa kutuaminisha ujinga usio na kichwa wala miguu na mpaka leo hii unaona vijana wetu wanavaa milegezo, wanasuka nywele, kuvaa hereni na kupaka liptick eti ndiyo wanaona ujanja.
Umenena mambo safi sana. Mtanzamo wako unauiana na wangu. Tatizo ni wakuu walio pita baada ya Nyerere. Asante sana Mungu akubariki! Magufuli na Msaidizi wake Paul Makonda ndiyo wenye kazi ya kusafisha uchafu walio uacha Marais hao. [emoji120] Mungu awalaani huko waliko. Hasa Kikwete.
 
Hilo sasa sio swala la Makonda. Mwulizeni Rais na watu alio wateua. Makonda alionyesha kifua mka gomba mkamnyang'anya madaraka. Sasa hangaikeni na mnao waita smart guys wa kutatua matatizo ya madawa ya kulevya.

Acheni unafiki na fitina. Hamkutaka seriously hilo jambo kutatuliwa. Mngetaka Makonda angeweza kwa namna fulani. Alichotakiwa kuwa nacho ni support yetu na vifaa vya kutosha kutoka serikalini.
Acha kutetea ujinga wewe!!!

Majority ya aliokuwa amewataja Makonda hawakukutwa na ushahidi baada ya kwenda kupekuliwa! Na ni Makonda ndie alisababisha kwa sababu haiwezekani mtu umtaje hadharani halafu ukampekue cku 2 baadae na utarajie kukuta ushahidi!!

Waliofikishwa mahakamani ni mateja! Acha ushabiki na mahaba niue kwenye serious issues! Uliza wanaofuatilia haya mambo wakujuze!

And FYI, Charles Kitwanga aliendesha vita yenye matokeo mazuri mara 5 ya Makonda! Drugs war inaendeshwa kimya kimya na sio kwa mayowe yanayosababisha wahusika wafiche ushahidi!

Uliza jinsi alivyokuwa amekamatwa Shikuba pale airport in 2014.

Baada ya kuruka viunzi kila wakati; toka US hadi Dar na kisha kukimbilia South Africa... bado wanaume wakawa wanamfuatilia kimya kimya! Na kote huko alikuwa anabadilisha majina na passport lakini akaja kudakwa hapo airport kama mtoto mdogo!

Sasa kwa staili ya Makonda; ile siku intelligence imesema Shikuba ametoka SA na anaelekea Dar; basi si ajabu angeenda kuita media na kutangaza "tumepata taarifa lile giant la drugs linatarajia kuja Dar na kwahiyo nimeviagiza vyombo vya usalama vikae tayari!"

Sasa kwa staili hiyo unadhani angekamatwa?!

Uliza alivyokuwa amekamatwa Maureen Lyumba huko Lindi au wale Wachungaji fake wa Kinaijeria ambao walikamatwa Tegeta!

Wote hao walikamatwa kimya kimya na ni big dealers! Lakini kwa approach ya Makonda; asingekamatwa hata mmoja!
 
Huyu Mkuu wa Mkoa wa Dar Mhe. Paul Makonda alimaarufu DAB(Daudi Albert Bashite) inaonekana ana matatizo ya Kisaikolojia. Wataalamu wa Saikolojia wanasema ukikuta mtu anafanya mambo fulani kwenye jamii kwa kutaka umaarufu tena kwa kuumiza wengine basi ujue ana matatizo makubwa. Ukifuatilia mtu kama huyu utakuta aidha amelelewa na mzazi wa upande mmoja tu(KE/ME) au Wazazi wake Baba na Mama walikuwa hawaelewani(ugomvi wa kila siku.kutengana n.k) na pengine alikulia mitaani(kama mtoto wa mtaani, ombaomba, kibaka n.k.)

Mtu kama huyu akija kubahatika kupata nafasi ya madaraka makubwa basi ATATUMIA MADARAKA HAYO KULIPIZA AU VISASI....! Wataalamu wa Saikolojia watakubaliana na mimi kuwa vitendo anavyofanya RC Makonda vinadhihirisha hali hiyo. Sina uhakika sana kama Mhe. Makonda alipata malezi stahili ya Baba na Mama na kama alisomeshwa kwa kiwango cha elimu kinachostahili katika jamii ili kufikia ngazi aliyopo sasa...!!

Tangu RC Makonda aingie Madarakani kama DC na baadaye RC amekuwa ni kiongozi mwenye vituko na staili ya aina yake ya kuongoza mbayo naamini haipo hata kwenye misahafu ya Uongozi.Kwanza ikumbukwe huyu Paulo Makonda alimpiga Waziri Mkuu mstahafu Joseph Sinde Warioba wakatiwa mchakato wa Bunge la Katiba mpya...kabla hajawa hata DC. Baaada ya kuwa DC na baadaye RC watu wameshuhudia akija na mambo ya kushangaza kama siyo ya kushtua. K wa uchache tu alianza na Madawa ya Kulenya akiwataja watu maarufu na Mashuhuri ili kuwadhalilisha akiwalenga hasa wapinzani(Vyama vya siasa na CCM yenyewe) zoezi ambalo mpaka leo limeacha MAKOVU MAKUBWA SANA MIONGONI MWA WATANZANIA,

Hivi majuzi kama kawaida yake alibuka na hoja ya KINA NA WATOTO WALIOTELEKEZWA NA WANAUME akiwalenga hasa WANAUME walioko upinzani ili kuwadhalilisha...... bila shaka tumeona kina EDWARD LOWASSA(Waziri Mkuu mstahafu) akitajwa mbele ya Kamera kumbe ni longolongo. Bunge kwa kupitia Wabunge lilihoji uhalali wa RC Makonda kudhalilisha watu kwa mambo ya FARAGHA akiwatangaza LIVE ili apate umaarufu...!!!Pamoja na kupingwa kwa Makonda bado huyu RC ameendelea KUKOMAA mpaka sasa. ikumbukwe kuwa maeneo yote anayojaribu kuibua vituko ni maeneo ambayo yana Wizara

Pamoja na kuathrika kisaikoljia kwa Makonda inaonekana ana kiburi cha kuzaliwa, kibri na jeuri iliyopitiliza....kwamba haogopi yeyote au chochote na amewaambia Waheshimiwa Wabunge kuwa haogOpi kushtakiwa...!!Huu ni ujasiri wa ajabu sana. Kwamba mtu mmoja anavunja Katina sheria na muhimili kama Bunge unapingana naye lakini bado Makonda anaendelea kuvutana kutumisha misuli dhidi ya muhimili.....!!Lazima Kuna shida au tatizo mahali fulani. Yawezekana kabisa kuna nguvu kubwa nyuma yake inayompa jeuri, kibri na majivuno....!!!Rais JPM kuna siku alimpongeza mbele ya hadhra kwa kumwambia AENDELEE KUCHAPA KAZI PAMOJA NA SHUTUMA NA LAWAMA TOKA KWA WATZ. Leo hii amekuja tena na habari ya KUPIMA TEZI DUME NYUMBA KWA NYUMBA...Hivi kama Makonda anataka kupima Tezi Dume Wizara ya Afya chini ya Dada Ummi Mwalimu wako wapi???Hivi Makonda haoni aibu kwa kuwaingilia Viongozi wa maeneo hayo bila utaratibu na kwa ujumla wake anavuruga mfumo na utaratibu mzima wa UTAWALA BORA???

Huu ni wakati wa Rais Magufuli kumpumzisha huyu mtu kwenye nafasi hii ya Ukuu wa Mkoa maana imetosha. Hatuwezi kuendelea kuongoza kwa mtindo huu ambao haupo popote kwenye kazi zinazomhusu Mkuu wa Mkoa. RC Makonda alishawahi kumtuhumu hata IGP mbele ya Wazri Mkuu na akaachwa hivihivi tu. Kwa tabia hii kuna siku atamwambia huyu Mtauzi wake kuwa amekosea hivo hastahili kuwa Rais wa nchi hii. Kama ni mzazi una mtoto kibaka, akiiba analeta nyumbani mnakula kuna siku atakuibia Baba au Mama nyumbani na mtaishia kulaumiana tu....!!!
 
Mkuu jiandae kutumia mkojo, kutoa vyeti vya kuzaliwa vya babu, baba na vya kwako pamoja na vya bibi na mama yako.
 
Kuna mambo ni madogo lakini yanakera sana hasa uvutaji sigara hadharani. kama tukiwa serious jambo hili linaweza kumalizwa ndani ya muda mfupi sana.mimi namuunga mkono kwasababu anataka kuleta ustaarabu! siyo kila mahali unakuta mtu anavuta misigara yake.

Ama kuhusu mashoga, dawa ni nyepesi tu ni kuweka adhabu kali kwa wateja wao wakikamatwa walipishwe shs mil kadhaa wakishindwa wafanye kazi ya kusafisha mitaro michafu na kusaidia kuzoa taka kwa muda wa miezi mitatu.
Mambo mengine msijifanye kuwa nyinyi ni miungu. Kuna watu wameumbika kuwa hivyo. Kama una bisha, umejiuliza kwa nini kuna baadhi ya wanawake wana ndevu? Au kwa nini kuna watu wamezaliwa na sehemu zote mbili za uchi? Msiwe mna sema au kuandika vitu ambavyo binadam hana uwezo navyo.

Binadam tuna maumbile ya aina tofauti. Mungu katuumba hivyo. Wewe kama huwezi kufanya ushoga basi kuwa tolerant kwa hao wenye uwezo huo. Ni maumbile waliyo pewa na mungu vile vile.
 
MKOA HUU BWANA. SAFARII HII UMEPATA KIONGOZI MKALI KWERI KWERI narudia mkali kweRI kweRI . nakumbuka mdogo wangu mmoja anasema walikuwa na mwalimu mmoja WA NIDHAMU alikuwa anaitwa BOB MIKWARA alikuwa anatoka ofisini kwake anasimama assembly akiwa juu na wanafunzi wake chini anatoa matamko kwa sauti kali sana akitokwa na mate,jasho na mishipa ya kichwa kumsimama. halafu anarudi ofisini kwake anapiga selfie anarushia mtandaoni huku ameweka miguu juu ya meza ndo inakuwa imepita hiyo mpaka Jumatatu ijayo tena.
haya mawazo ya Wadau mbali mbali kuhusiana na Matamko mbali mbali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa DSM.

.SIPINGANI NA MAKONDA KUHUSU MAAGIZO YA JANA Dar Es Salaam LAKINI NINA "VIJIWAZO VYANGU KIDOGO":
●Mkuu kasema watu wasiwafollow mashoga (facebook, instagram, tweeter n.k) na adhabu baada wiki itafuata, JE MBONA NYIE MNAGUSANA NAO NA PICHA MNAPIGA NAO? JIKAMATENI KWANZA!!!!!!
●Suala la kukataza uvutaji shisha na sigara uko sahihi mkuu, LAKINI MBONA UNATAFUTA "KIKI" KWENYE MAMBO MADOGO WAKATI NDUGU ZENU WANATESEKA NA MADAWA YA KULEVYA KILA UCHAO? KATI YA SHISHA, SIGARA NA COCAINE/HEROINE KIPI UNADHANI KINATEKETEZA NGUVU KAZI YA TAIFA?
■■Pamoja na nia yako njema chief Makonda hebu anza na mambo makubwa haswa hili la madawa ya kulevya maana inaaminika kuwa hilo ‪#‎HALIGUSIKI‬
: MH MAKONDA:
■Umetenga maeneo ya kuvutia sigara (smoking zones) kama ilivyo ktk miji mingine mfano Nairobi Mombasa n.k?
■Vp suala la usafiri bure kwa walimu kwenye daladala liliishia wapi?
■Ishu ya ombaomba imeishia wapi?
■Madada poa je?
Kuhusu madawa ya kulevya si mlimpiga majungu hadi Bungeni mpaka Rais kumyang'anya uwezo wa kulitekeleza hilo kwa kuunda taasisi maalumu inayo shughulikia swala hilo? Leo inakuwaje kwamba RC Makonda anahusishwa na swala hilo?
 
we pia n kilaza,hiyo kampeni ya bashite lengo kuu n kuchafua kina lowasa na kututoa ktk mjadala wa wizi wenu,ndio maana yule Dada
aliwaumbua,mnaomuunga mkono muigizaji bashit akili zenu zitakuwa zipo kwenye utumbo mpana


Kama wewe si mjinga ni nini sasa, hapa unahisi tu kwa habari za kuambiwa kijiweni. Kama Lowassa HANA mtoto nje ya ndoa ya nini aogope? Na kama ni wake kwani ni kosa kumpa matunzo, si ni damu yake?
 
Back
Top Bottom