Wadau kinachoendelea katika jiji letu kuu hatukielewi
Mkuu wa mkoa huu ni dhahiri kuwa ameshindwa kazi aliyopewa na mh Rais
Mkoa wa Dar umekuwa na matukio ya ajabu ajabu ,watu kutekwa ovyo,si wanasiasa,si wafanyabiashara,si wanamuziki,si watoto,sasa kila aina ya mtu anaweza kutekwa Dar na mkuu wa mkoa yupo tu ofisini
Mkuu wa mkoa hata kusimamia Udart umeshindwa wananchi wanateseka unakula keki ofisini,yaani mkuu wa mkoa yupo active kwenye mambo ya wasanii kuliko mambo ya umma
Mkuu wa mkoa Paul Makonda ajitathimini kama anafaa kuwepo kwenye hiyo nafasi au mh Rais amhamishie mkoa mwingine au amuachishe kazi