Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Kumbe alikulia kota!? Ndio maana anamdomo.....
 
Mkuu KayScarpetta unayosema ni kweli kwani kwa sasa matamko anayoyatoa hayana impact kubwa kwa jiji letu la Dar katika kulifanya kuwa bora. Yeye kama Mkuu wa mkoa wa Dar anatakiwa kushirikiana na Jiji ili kutekeleza hayo niliyoyasema najua anao uwezo huo kwa nafasi yake aelekeze nguvu zake hapo
Mpimeni tezi dume
 
Swali langu kubwa ni hili:
Who does what?
Ni nani anafanya kipi?
Katika mkoa wenye mji?
Kuna
RC
RAS
DED
MAYOR
Wakuu wa idara zote:
Afya, elimu, kilimo, mifugo, miundo mbinu, mazingira, maji, ustawi wajamii/wazee/watoto/jinsia nk
Then kuna wabunge, madiwani, wenyeviti wa kata na vijiji na
WEO na VEO

Mimi nadhani kazi kubwa ya mkuu wa mkoa ni kuhakikisha kuwa

1. Kuna mgawanyo wa
kazi unaoeleweka
2. Kila kiongozi ama mfanyakazi anajua kuna fedha na vitendea kazi gani
3. Kila moja anajua majukumu yake
4. Kila moja amewezeshwa kutekeleza majukumu yake
5. Kuna ufuatiliaji na usaidizi wa karibu kutoka watu wanaoleweka wenye kujua nidhamu ya kazi.
Matamko mengine yaliyofanywa hayana maana kama wafanyakazi na viongozi hawajawezeshwa.

Kufunga maduka mpaka saa nne wakati watu wamelala na jiji ni chafu
bado haina maana.
Weka sheria na adhabu ya malipo mazingira ya mahali yakikutwa pachafu kama wanavyofanya Moshi.
Kwanini tunashindwa kujifunza kwa wenzetu?
Shimo linakaa barabarani na kuleta ajali kwa zaidi ya mwaka moja lakini hakuna kati ya viongozi wote hao anajua kuwa ni jukumu lake.
Ama barabara haina alama
Ama pomba la maji limepasuka
Ama kifusi cha vumbi kimekaa barabarani kwa mwezi mzima bila kutandazwa
Ama vumbi imetumika badala ya maram katika matengenezo ya barabara fulani
Ama kuna gereji kila mahali badala ya sehemumaalumu na ndiyo maana kuna magonjwa mengi ya kansa nchini
Ama barabara hii ama daraja hili ni mbovu inahitaji matengenezo.
Ama ufuko wabahari ni mchafu ila hatujui anayehusika
Au kuna ngombe na mbuzi wanachafua mazingira mitaani lakini hakuna mwenye usemi
Barabara nyingi Dar hazina majina na vitongoji na vijiji vingi Dar havina majina lakini hatujui anayehusika!

Ebu tuache kusifia kwanza
Haya mambo ya msingi yafanyike kabla ya makubwa yasiyowezekana!
RC siyo Mungu lakini ashirikishe viongozi wake ili kilamoja afanye wajibu wake, apate sifa zake
Badala ya RC kusema morning mpaka evening kuwa huu ni mkoa wangu! Mkoa wangu!
Tunachotaka ni mambo muhimu yakae sawa!
Amen!
 
Mambo mengine msijifanye kuwa nyinyi ni miungu. Kuna watu wameumbika kuwa hivyo. Kama una bisha, umejiuliza kwa nini kuna baadhi ya wanawake wana ndevu? Au kwa nini kuna watu wamezaliwa na sehemu zote mbili za uchi? Msiwe mna sema au kuandika vitu ambavyo binadam hana uwezo navyo.

Binadam tuna maumbile ya aina tofauti. Mungu katuumba hivyo. Wewe kama huwezi kufanya ushoga basi kuwa tolerant kwa hao wenye uwezo huo. Ni maumbile waliyo pewa na mungu vile vile.
Punga at work
 
Huyu Mkuu wa Mkoa wa Dar Mhe. Paul Makonda alimaarufu DAB(Daudi Albert Bashite) inaonekana ana matatizo ya Kisaikolojia. Wataalamu wa Saikolojia wanasema ukikuta mtu anafanya mambo fulani kwenye jamii kwa kutaka umaarufu tena kwa kuumiza wengine basi ujue ana matatizo makubwa. Ukifuatilia mtu kama huyu utakuta aidha amelelewa na mzazi wa upande mmoja tu(KE/ME) au Wazazi wake Baba na Mama walikuwa hawaelewani(ugomvi wa kila siku.kutengana n.k) na pengine alikulia mitaani(kama mtoto wa mtaani, ombaomba, kibaka n.k.)

Mtu kama huyu akija kubahatika kupata nafasi ya madaraka makubwa basi ATATUMIA MADARAKA HAYO KULIPIZA AU VISASI....! Wataalamu wa Saikolojia watakubaliana na mimi kuwa vitendo anavyofanya RC Makonda vinadhihirisha hali hiyo. Sina uhakika sana kama Mhe. Makonda alipata malezi stahili ya Baba na Mama na kama alisomeshwa kwa kiwango cha elimu kinachostahili katika jamii ili kufikia ngazi aliyopo sasa...!!

Tangu RC Makonda aingie Madarakani kama DC na baadaye RC amekuwa ni kiongozi mwenye vituko na staili ya aina yake ya kuongoza mbayo naamini haipo hata kwenye misahafu ya Uongozi.Kwanza ikumbukwe huyu Paulo Makonda alimpiga Waziri Mkuu mstahafu Joseph Sinde Warioba wakatiwa mchakato wa Bunge la Katiba mpya...kabla hajawa hata DC. Baaada ya kuwa DC na baadaye RC watu wameshuhudia akija na mambo ya kushangaza kama siyo ya kushtua. K wa uchache tu alianza na Madawa ya Kulenya akiwataja watu maarufu na Mashuhuri ili kuwadhalilisha akiwalenga hasa wapinzani(Vyama vya siasa na CCM yenyewe) zoezi ambalo mpaka leo limeacha MAKOVU MAKUBWA SANA MIONGONI MWA WATANZANIA,

Hivi majuzi kama kawaida yake alibuka na hoja ya KINA NA WATOTO WALIOTELEKEZWA NA WANAUME akiwalenga hasa WANAUME walioko upinzani ili kuwadhalilisha...... bila shaka tumeona kina EDWARD LOWASSA(Waziri Mkuu mstahafu) akitajwa mbele ya Kamera kumbe ni longolongo. Bunge kwa kupitia Wabunge lilihoji uhalali wa RC Makonda kudhalilisha watu kwa mambo ya FARAGHA akiwatangaza LIVE ili apate umaarufu...!!!Pamoja na kupingwa kwa Makonda bado huyu RC ameendelea KUKOMAA mpaka sasa. ikumbukwe kuwa maeneo yote anayojaribu kuibua vituko ni maeneo ambayo yana Wizara

Pamoja na kuathrika kisaikoljia kwa Makonda inaonekana ana kiburi cha kuzaliwa, kibri na jeuri iliyopitiliza....kwamba haogopi yeyote au chochote na amewaambia Waheshimiwa Wabunge kuwa haogOpi kushtakiwa...!!Huu ni ujasiri wa ajabu sana. Kwamba mtu mmoja anavunja Katina sheria na muhimili kama Bunge unapingana naye lakini bado Makonda anaendelea kuvutana kutumisha misuli dhidi ya muhimili.....!!Lazima Kuna shida au tatizo mahali fulani. Yawezekana kabisa kuna nguvu kubwa nyuma yake inayompa jeuri, kibri na majivuno....!!!Rais JPM kuna siku alimpongeza mbele ya hadhra kwa kumwambia AENDELEE KUCHAPA KAZI PAMOJA NA SHUTUMA NA LAWAMA TOKA KWA WATZ. Leo hii amekuja tena na habari ya KUPIMA TEZI DUME NYUMBA KWA NYUMBA...Hivi kama Makonda anataka kupima Tezi Dume Wizara ya Afya chini ya Dada Ummi Mwalimu wako wapi???Hivi Makonda haoni aibu kwa kuwaingilia Viongozi wa maeneo hayo bila utaratibu na kwa ujumla wake anavuruga mfumo na utaratibu mzima wa UTAWALA BORA???

Huu ni wakati wa Rais Magufuli kumpumzisha huyu mtu kwenye nafasi hii ya Ukuu wa Mkoa maana imetosha. Hatuwezi kuendelea kuongoza kwa mtindo huu ambao haupo popote kwenye kazi zinazomhusu Mkuu wa Mkoa. RC Makonda alishawahi kumtuhumu hata IGP mbele ya Wazri Mkuu na akaachwa hivihivi tu. Kwa tabia hii kuna siku atamwambia huyu Mtauzi wake kuwa amekosea hivo hastahili kuwa Rais wa nchi hii. Kama ni mzazi una mtoto kibaka, akiiba analeta nyumbani mnakula kuna siku atakuibia Baba au Mama nyumbani na mtaishia kulaumiana tu....!!!
Taratibu mkuu... Nissan nyeupe zimetapakaa popote zinakufikia lol
 
Mkuu wa mkoa mchapa kazi kuliko wote Mh. Paul Makonda, amefika hatua anajiona naye ni Rais wa sehemu husika kana kwamba anaweza ongea lolote,

Nakupa sifa moja kuu ya Rais Magufuli,

Hapendagi kukosolewa au kuonekana amekosea katika mambo yake, mbaya zaidi ukimkosoa katika tuezi anazofanya, tunayo mifano mingi juu ya hilo.

Kuna kipindi watu walishinikiza utoke katika ukuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwasababu wanazojua wao, lakini aliyekuteua kwa jeuri akasema hawa hawanijui sikutoi na sipangiwi.

Likaja suala la Mnyeti akasema hupangiwi na ukampa kabisa cheo, suala lako Makonda na Nape, Nape alitaka kuonekana anajua sana mpaka kuingilia kuchunguza mtu ambaye kateuliwa na Rais, hakubaki salama.

Sasa naona wewe umeanza kuteleza juu ya Juliana Shonza na kupost post mambo ya kumponda Shonza na kumtetea Diamond, so suala la kuingilia kichwa kichwa ili utamkera mkuu sasa hivi na kufanya aonekane hana busara katika teuzi zake.

Mbaya zaidi haumtukuzi vizuri kama zamani, japo Rais hayupo ili atukuzwe, lakini wewe ndo uliyaanzisha yaendeleze, hata mkipeana mkono, hunyenyekei kama zamani, unampa mkono mmoja, huoni kina Gambo, na Mongella,?

Ndo muone madhara ya kutukuza tukuza watu, Mungu tu ndo hutukuzwa

Ni hayo tu

picha ya Kabla unyenyekevu 100%

View attachment 722594

Picha ya baada hakuna unyenyekevu
View attachment 722595


Hata kwa waziri mkuu
View attachment 726855
 
Nikiwa kama mkaazi wa jiji la dsm naomba wakaazi wenzangu wa jijini na wengine kutoka mingine tujadili je ktk matamko yote ya Makonda ni mangapi yamefanikiwa kwa100%?
 
Nikiwa kama mkaazi wa jiji la dsm naomba wakaazi wenzangu wa jijini na wengine kutoka mingine tujadili je ktk matamko yote ya Makonda ni mangapi yamefanikiwa kwa100%?

Kuvuka dhoruba kali aliyoipata mwaka 2017. Sasa imekuwa historia tu. Maisha yanasonga kama kawa, kama dawa za Bi. Havijawa.
 
Mateja kupungua mitaa ya ufipa waliokuwa wamejaa kuzunguka makao makuu ya chadema.
 
Back
Top Bottom