Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,415
- 29,584
Tatizo kubwa la viongozi wetu wengi hapa Tanzania, na hasa RC Makonda, ni kwamba wanatumia nguvu nyingi katika mambo ambayo ni ya kawaida sana (routine things), ambayo wasaidizi wao ndio wanapaswa kuyafanya. Nimeliona hili hata kwa Raisi, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa nk.
Wanasahau kwamba wao nafasi zao ni mtazamo mbali (strategic positions) kuliko haya mambo madogo madogo ya kila siku. Kiongozi mkubwa anayeweka nguvu zaidi katika mambo madogo madogo hafai kuwa kiongozi. Sawa na Meneja Mkuu kufuatilia mambo kama nani leo kachelewa kufika kazini. Wakati fulani Waziri mmoja alifanya hili!
Sasa nina changamoto moja kwa RC Makonda. Hili suala la Dar es Salaam kufurika maji kila mvua ikinyesha, tatizo la muda mrefu sana, linatia aibu sana. Sasa RC Makonda akitaka kweli jumuiya ya Dar es Salaam na hata Tanzania imkumbuke siku zote, basi aache kufukuzana na madiwani na vitatizo vidogo vidogo ambavyo sio size yake, na aweke mkakati na kuusimamia kwamba haitatokea tena kwamba mvua ikinyesha Dar es Salaam basi inageuka kuwa ziwa la maji.