Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ila akiacha siasa akafanya kazi kwa ubunifu atafanikiwa, akubali kujishusha kwenye baadhi ya mambo ili kushirikiana na ukawa, ila kwa sasa anafanya siasa wakati sio muda wa kampeni.
 
Anatafuta kuvunja rekodi ya kuwa RC mzigo kuliko wote nchi hii.
Laana ya marehemu Kabwe inamuandama huyo.
Makonda laana ya kabwe itaendelea kumtafuna mpaka siku ambayo na yeye atapelekwa kaburini
 
View attachment 366544
Utasema huyu ana talanta za uongozi kweli?
Mkuu hakuna haja ya kuuliza wakati unaona mtu mwenyewe kashapagawa na hajui nini anafanya. MUCCoBS alidisco kwa kufuata mambo ya kipuuzi kama haya. Yaan utoto hajaacha kabisa ameshindwa kujielewa kwa sasa yeye ni nani
 
Makonda ameshaichoka hiyo kazi ya ukuu wa Mkoa,
Huwezi kuongea mashudu kama hayo alafu bado ukaendelea kuwa mkuu wa Mkoa.
Poleni sana wakazi wa Dar.
Tena hatuna uhakika kesho tukiamka atakuja na lip
Makonda ameshaichoka hiyo kazi ya ukuu wa Mkoa,
Huwezi kuongea mashudu kama hayo alafu bado ukaendelea kuwa mkuu wa Mkoa.
Poleni sana wakazi wa Dar.
Mkuu kuna wakati aliwahi kujibu kwa kauli za mipasho utadhani pashkuna fulani
 




Kwanza ningependa kukupongeza kwa juhudi zako za kutaka kuliboresha jiji letu hili la Dar. Nimekuwa nikifuatilia juhudi zako tangu ulipokuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni. Naamini jitihada zako za kutaka kuboresha wilaya ya Kinondoni ndizo zilizomfanya Raisi akuongezee majukumu kutokana na kuona jinsi unavyochapa kazi.

Kwa muda sasa nimekuwa nikiona unaibuka kila siku na matamko ambayo baadhi ya matamko hayo hayajafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa mfano suala la ombaomba. Kwa ushauri wangu kabla ya kutoa matamko naomba ufanye utafiti mdogo kwanza na kujiridhisha na kuweka mpango kazi wa namna ya kutatua tatizo kabla ya na kutoa tamko kwamba hutaki jambo fulani katika mkoa wako. Kuna vita vingine hutaviweza zaidi ya kujifedhehesha.

Kwa ushauri wangu naomba uweke vipaumbele katika mambo yafuatayo.

=Kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati katika shule zetu

=Kuongeza na kuboresha maabara katika shule zetu

=Kujenga maktaba katika shule na maeneo mbalimbali kwa kuanzia ngazi ya kata na kuhakikisha kunapatikana huduma za inteneti na magazeti ya kila ziku hapa unaweza kuzishirikisha kata kutenga maeneo kwa ajili ya kujengwa kwa maktaba hizo ili kuhimiza watu kujisomea na kuongeza maarifa na sio kupiga soga vibarazani na kunywa kahawa

=Kuhakikisha jiji linakuwa safi kwa kuweka sheria ndogo ndogo kali zitakazowabana wachafuzi wa mazingira na ili kulitekeleza hili unaweza kupata uzoefu kutoka kwa viongozi wa mji wa Moshi

=Kupiga marufuku mifuko ya plastiki kutumika hapa jijini na badala yake wenye viwanda hivyo kulazimishwa kuzalisha mifuko ya karatasi kwa ajili ya matumizi au kushirikiana na SIDO kuja na njia mbadala ya mifuko ya karatasi ambapo ubunifu huo unaweza kuwezesha vikundi vidogo vidogo vya vijana na kina mama..

=Kutengeneza maeneo ya vivutio kwa watalii wanaokuja katika jiji letu kwani wengi hupita tu kwa sababu hakuna vivutio. Hili unaweza kuwashirikisha wabunifu na wakandarasi wetu na kutenga maeneo ambayo yana historia na kuyaboresha kwa kiwango ambacho kitavuta wataalii wengi kutumia siku kadhaa katika jiji letu kwa mfano kama mji mkongwe wa Zanzibar, na Makumbusho ni eneo mojawapo ambalo linaweza kuboreshwea zaidi.

=Kuweka utaratibu mzuri wa boda boda, kwa sasa bodaboda pamoja na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Dar lakini zimekuwa ni chanzo kikuu cha ajali hapa jijini na vijana wengi wamekufa au kupoteza viungo na hivyo kutishia nguvu kazi hapa nchini. Tusipoweka utaratibu na kutoa elimu kwa waendesha bodaboda na madereva kuheshimu sheria za barabarani na kuweka sheria kali kwa watakaokiuka miaka kumi ijayo nchi hii itakuwa na ukosefu wa nguvu kazi.

=Tenga maeneo mengi kwa ajili ya vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi na maeneo haya yakabidhiwe VETA ili vijana ambao wameshindwa kuendelea na masomo wapate fursa nyingine ya kujifunza masomo ya ufundi lakini pia ni vyema kukitengwa maeneo ya mafundi wetu kwa mfano mafundi wa magari kuwe na eneo lao, mafundi seremala wae na maeneo yao kama vile Keko, mafundi wa kuchomea vyuma wawe na maeneo yao ili wenye kuhitaji huduma hizo wawe wanajua zinapatikana wapi na kuondoa hizi vurugu mitaani

=Rejesha viwanja vya michezo vilivyovamiwa na hakikisha swala la viwanja vya michezo linapewa kipaumbele, na michezo isiwe ya aina moja, ongeza wigo wa michezo mbalimbali ili na sisi tuweze kushiriki michezo ya olimpiki.

=Mabango na matangazo yawekewe utaratibu maalum siyo kila mtu akiwa na tangazo lake anapita mitaani na kuchafua kuta za watu itungwe sheria kuondoa tatizo hilo n ahata haya makampuni ya matangazo nayo pia yawekewe utaratibu maalum kuondoa mabango mengi mitaani na kufanya jiji lisionekane nadhifu.

=Wanaohubiri usiku kucha na kelele za mziki kwenye mabaa katika makazi ya watu zipigwe marufuku na kila Pub kama watataka kupiga mziki kwa sauti ya juu basi lazima wawe na ukumbi usioruhu sauti kutoka nje.

=Njoo na njia mbadala ya kuhimiza matumizi ya baiskeli kwa wale wanaofanya kazi maeneo ya karibu na hili litafanikiwa kwa wakandarasi wetu kubuni njia ya waendeshao baiskeli ili kuepuka bughdha kwa watembeao kwa miguu. Mpango huu unaweza kuanza na zile barabara ndefu kama Tegeta mpaka Posta, Gongo la Mboto mpaka Posta, Mbagala mpaka Posta.

Mimi naamini kama ukiweka vipaumbele kwenye mambo hayo machache kati ya mengi ambayo sijayazungumzia utaacha historia katika jiji hili na utakumbukwa na vizazi vijavyo.

Unaweza kuitisha mdahalo kwa wakazi wa jiji hili ili kupitia mdahalo huo uweze kuibua mbinu mbalimbali za kuboresha jiji letu. Naamini wakaazi wa jiji hili hawafurahishwi na hali jinsi ilivyo kwa sasa na wangependa hali iwe nzuri zaidi kwa kuondoa kero nilizozitaja hapo juu, iwapo utawaalika kwenye mdahalo watakupa ushirikiano.

Nakutakia kila la kheri katika majukumu yako ya kila siku.

Ni mimi Mzee Mtambuzi.
Sizan Kama atasoma atakua kashachoka
 
Simbali sana kwa maelekezo....

Ukifika afrikasana kunaa sehemuya kuuzia mafuta opp kuna sehemu ya kuuza chakula usiku wanajaa sanasana..baadayahapo pemben kuna njia inaingia kwandan....

Neenda mbele utakuta uwanja wa wazi kushoto kuna nyumba ya vyumba vinne sebule aijaisha...hiinyumbaa n laana mabinti ndipo wanajazana pale nakuinamishwa nakupigwa sindano ya fasts

Nanpale wanapoona WATU wamejaa wamasai huwaruhusu kufanyia mapenzi kuna gari moja nyeusi inakaaga hapo pembeni Toyota hilux usipojua unawezahisi iko KWENYE parkn ila kams una kapesachako wanakuwashia NA ac kabisa
Sio sehemu MPYA mapolisi ndio wamekuwawakija NA kuondoka kwa siku wamekuwa wakipita NA defender sichini ya NNE nakugeuka aijulikani wansongea nn NA huyo mmasai

Nafiki mh polepole NA were mnaweza let's mabadiliko amamkakaondoa kabisa AMA kakawekewea ulinzi watoto wadogo wamekuwa wakiwainamisha mama xao bila aibu hip sehemu......

Watatulia watoto
 
Mpwa umesikika isipokuwa kazi zimeingiliana.....sasa nchi nzima inajiandaa na mikakati na mipango ya kuzuia UKUTA........nadhani baada kuubomoa UKUTA wanaweza wakaishughulikia kero yako....
 
14068311_2099862966906522_5756918632513164890_n.jpg

•••
Tujengee vibanda jamii hii / kila mahali kuanzia karume yote kila pahala ambapo panaruhusu kwa jiji zima,vipatie namba maalumu/
at least vipatikane vibanda mil 2 dar yote vitakavyokuwa katika mpangilio maalum/
kwanini Nairobi watushinde?
•vibanda mil 2 ×10000/- kila kibanda kwa mwezi!,je jiji litaingiza kiasi gani?/ kwa mwezi.
**kukusanya matrilions sometime haiitaji maguvu mengi,ukizingatia Ajira hakuna /
 
Mh makonda kwanza na kupongeza kwa mikakati yako ya kuliendesha jiji lenye watu milioni 6 na ushehe tunaomba siku moja pita barabara ya kigogo mwisho uje uone daraja limeziba tangia mafuriko

Mapaka leo haliko vizuri pia suala usafi bado ni 2% tu ya magizo yako watu wanatupa taka taka kwenye daraja

Serekali ya mtaa ipo lakini hakuna kinachofanyika hivi watapataje zawadi zako za magari mapya
 
Mh makonda nakuchosha,,hongera kwa ujenzi wa taifa, Mimi so mpenzi wako ila napenda unavoshughulika na matatizo ya wana dar,,ushauri shuka chini chini huku kwetu,,sector binafsi zinatuumiza sana,mshahara ni midogo ssana masa ya ziada na siku za sikukuu hatulipwi,,tunaomba ufuatilie we we mwenyewe,vyama vya wafanyakazi haviruhusiwi huku,,ni kwenye mahotel na restaurant and bar/ night club,,plz ukituma watu wako wanapewa wanapewa Chai,,they say coffee,cupuccino and chicken chips basi wanarudi wanasema pako OK,pakuanzia anzia hapo Morogoro store kuna marestaurant kibao
 
1475047297117.jpg


Utendaji kazí wa mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda umekuwa ukiwavutia watu kwa kuwa amekuwa akibaini changamoto zinazoikabili mkoa wetu na amekuwa akija na namna mbalimbali ili kuhakikisha mji unakuwa katika hadhi ya jiji la kimataifa

Makonda amekuwa akibuni njia tofauti ili kuhakikisha eneo analokabidhiwa kiutawala anatekeleza majukumu ndio halí iliyomfanya hata apandishwe cheo mambo makubwa aliyofanya akiwa DC aliwakutanisha vijana wenye vipaji vyao ambao wengi wao mpaka sasa wanatumia ile fursa kujinufaisha pia nakumbuka alivyokabiliana na migogoro ya ardhi ya kinondoni

"HONGERA MAKONDA"

1-Upimaji bure wa magonjwa mbalimbali
2-Suala la Madawati
3-Utambuzi wa Raia na kazí zao
4-uvaaji wa kofia ngumu kwa abiria na. Bodaboda
5-kuhamasisha wananchi kuhusu Ushiriki wa suala la usafi
6-Kampeni ya Dar yangu, Mti wangu
7;Utambuzi wa bodaboda kwa kieletronic

NINGEFURAHI;Ningefurahi zaidi kuona Viongozi kama MAMEYA wanamuunga mkono ili wananchi wa Dar tupate maendeleo na kuwa na DSM mpya.
 
View attachment 408201

Utendaji kazí wa mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda umekuwa ukiwavutia watu kwa kuwa amekuwa akibaini changamoto zinazoikabili mkoa wetu na amekuwa akija na namna mbalimbali ili kuhakikisha mji unakuwa katika hadhi ya jiji la kimataifa

Makonda amekuwa akibuni njia tofauti ili kuhakikisha eneo analokabidhiwa kiutawala anatekeleza majukumu ndio halí iliyomfanya hata apandishwe cheo mambo makubwa aliyofanya akiwa DC aliwakutanisha vijana wenye vipaji vyao ambao wengi wao mpaka sasa wanatumia ile fursa kujinufaisha pia nakumbuka alivyokabiliana na migogoro ya ardhi ya kinondoni

"HONGERA MAKONDA"

1-Upimaji bure wa magonjwa mbalimbali
2-Suala la Madawati
3-Utambuzi wa Raia na kazí zao
4-uvaaji wa kofia ngumu kwa abiria na. Bodaboda
5-kuhamasisha wananchi kuhusu Ushiriki wa suala la usafi
6-Kampeni ya Dar yangu, Mti wangu
7;Utambuzi wa bodaboda kwa kieletronic

NINGEFURAHI;Ningefurahi zaidi kuona Viongozi kama MAMEYA wanamuunga mkono ili wananchi wa Dar tupate maendeleo na kuwa na DSM mpya.
Hata yeye inabidi awaunge mkono wenzake sio yeye tu kuingwa. Gurudumu la maendeleo ni jukumu letu sote
 
Back
Top Bottom