Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ndugu yangu yangu kutaja majina makubwa juu ya dawa yanahitaji kianza nawatumiaji iliwatoe data za wanaowauzia ndio kwenda kwa wakubwa
 
Tatizo lililopo Nape na wengine wanaangalia 2020, ila Makonda haangalii hilo maana hao wanaowatuhumu ndio hao hao walopiga kampeni kama MAMA ONGEA NA MWANAO... WEMA SEPETU na Samia wake... Mama Samia Mungu anakuona ujue muokoe wema aisee maana kawa maarufu utafikiri hakuna wengine walokwidwa[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Ajibu hizi tuhuma, ukimya wake unatia shaka kama kweli ni muadilifu!
Ni kweli alimpangisha Masogange bingwa wa kusafirisha ngada..??
 
Kama Watanzania hapa tulipofika tunahitaji kutafakari kwa kina kama utendaji wa viongozi wetu wa awamu hii ya tano unaleta matumaini. Katika kipindi kifupi tumeshuhudia utendaji unaotia shaka katika mihimili yote mitatu ya dola na hii peke yake inatoa indiketa ya tunakoelekea. Hivyo swali linalohitaji jibu la haraka bila kuchelewa zaidi ni je kwenye safari yetu hii tuko njia sahihi?

Kwa kuanzia, je kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam, Paul Makonda, kiongozi aliyeteuliwa na Rais kuanza kutunishiana misuli na mihimili mingine ya dola ni sahihi? Je vitendo vya wateuliwa wa Rais, kutunishiana misuli na wawakilishi wa wananchi akitishia kuwashughulikia ni sahihi? Lakini linalotishia zaidi ni ukimya wa mteuzi haya yakitendeka unatupa picha gani sisi wananchi.

Leo nimeona nianze tu na kura ya maoni kwa wana JF popote walipo, je vitendo vya Mkuu huyo wa Mkoa kwa ujumla wake ni sahihi? Je unaunga mkono hatua anazozichukua dhidi ya anaowaita watuhumiwa wa makosa mbali mbali? Je jeshi letu la polisi, kazi yao ni kutii amri bila kuzingatia uhalali wake kisheria? Je siku wakiamriwa kumpiga risasi mwakilishi wa wananchi watatii?
 
Weka ushahidi wa kutunishia misuli miimili mingine
 
Nashauri kama sio yeye basi Hata ngazi ya juu watoe maagizo kwa vyombo vya ulinzi na usalama wawachunguze msukuma na Bulaya kwa siri i wajue mienendo yao.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, nakuandikia ujumbe huu mfupi kupitia mtandao huu wa kijamii wa Jamiiforums kutokana na kinachoendelea dhidi yako. Mitandaoni kunaandikwa na kusemwa kuwa unahusika na kutumia cheti ambacho si chako cha kidato cha nne. Wapo wanaofikia hata kukuita jina la Daudi Albert Bashite.

Najua wewe ni kiongozi wa kiserikali: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Najua kuwa Rais alikuwamini kila idara inayokuhusu kabla ya kukuteuwa kuwa katika nafasi hiyo. Najua kuwa Rais anakufuatilia kila uchao kama mteule wake. Najua pia nafasi yako kiuongozi inakupa heshima na hadhi tofauti katika jamii ya watanzania.

Kuambiwa kuwa umetumia cheti cha mtu mwingine kwakuwa wewe ulifeli kwa kupata sifuri (kulingana na Mchungaji Gwajima) ni suala kubwa. Ni suala linalogusa maadili,heshima na hata utendaji wako. Cheti ndicho kinachompa mtu nafasi fulani ya kimaisha katika jamii na ndiyo maana kinapaswa kwanza kuwa cheti chake mwenyewe muhusika.

Kelele nilizozisema hapo juu zikiendelea zitaonekana ni ukweli. Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, nakushauri ufanye hivi. Kama unaamini kuwa unachafuliwa na kutwezwa kwakuwa kinachosemwa si kweli, waburuze mahakamani wote wanaokuchafua na uwadai mabilioni kulingana na heshima na hadhi yako. Tafadhali usitumie vyombo vya dola kwa mambo yako binafsi.

Muda wa kuweka kumbukumbu zako sawa ni huu kwakuwa unapaswa kuuanika ukweli juu ya kinachosemwa. Zinatumika media katika suala hili kwakuwa nawe ni mtumiaji mzuri wa media hizo. Nawe tumia media kujisafisha na kutangaza kuwashughulikia kimahakama wote wanaosema hayo, kama wanayoyasema si kweli. Kama ni kweli, endelea kukaa kimya.
 
Kwa mbwembwe za Bashite na anavyopenda kuona Kamera nyingi zinammulika kuliko anavyomulikwa Wema angekuwa tayari keshaita waandishi, tena Press conference angeifanyia ikulu huku akisindikizwa na tabasamu mubashara na madongo ya kusemwa vibaya mpendwa wake na Mh. mkulu. BTW Atajisafisha vipi ikiwa kweli alitaga!?
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, nakuandikia ujumbe huu mfupi kupitia mtandao huu wa kijamii wa Jamiiforums kutokana na kinachoendelea dhidi yako. Mitandaoni kunaandikwa na kusemwa kuwa unahusika na kutumia cheti ambacho si chako cha kidato cha nne. Wapo wanaofikia hata kukuita jina la Daudi Albert Bashite.

Najua wewe ni kiongozi wa kiserikali: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Najua kuwa Rais alikuwamini kila idara inayokuhusu kabla ya kukuteuwa kuwa katika nafasi hiyo. Najua kuwa Rais anakufuatilia kila uchao kama mteule wake. Najua pia nafasi yako kiuongozi inakupa heshima na hadhi tofauti katika jamii ya watanzania.

Kuambiwa kuwa umetumia cheti cha mtu mwingine kwakuwa wewe ulifeli kwa kupata sifuri (kulingana na Mchungaji Gwajima) ni suala kubwa. Ni suala linalogusa maadili,heshima na hata utendaji wako. Cheti ndicho kinachompa mtu nafasi fulani ya kimaisha katika jamii na ndiyo maana kinapaswa kwanza kuwa cheti chake mwenyewe muhusika.

Kelele nilizozisema hapo juu zikiendelea zitaonekana ni ukweli. Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, nakushauri ufanye hivi. Kama unaamini kuwa unachafuliwa na kutwezwa kwakuwa kinachosemwa si kweli, waburuze mahakamani wote wanaokuchafua na uwadai mabilioni kulingana na heshima na hadhi yako. Tafadhali usitumie vyombo vya dola kwa mambo yako binafsi.

Muda wa kuweka kumbukumbu zako sawa ni huu kwakuwa unapaswa kuuanika ukweli juu ya kinachosemwa. Zinatumika media katika suala hili kwakuwa nawe ni mtumiaji mzuri wa media hizo. Nawe tumia media kujisafisha na kutangaza kuwashughulikia kimahakama wote wanaosema hayo, kama wanayoyasema si kweli. Kama ni kweli, endelea kukaa kimya.
Sasa hana vyeti atafanyeje. Alivyo navyo ni vya kununua
 
Back
Top Bottom