Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Makonda tunaona anahangaika na usafi, nk. lakini hatujasikia akizungumzia suala la kuupanga mji wa DSM.

mji wetu umekuwa sehemu nyingine nyumba hazina mitaa, gari la zima moto halifiki sehemu husika tunaomba afuatiliesuala la mipango miji ili kuanzia sasa tuseme Tanzania BASI kujenga kiholela nyumba bila mitaa/barabara.

Tunaomba aongee na maafisa ardhi ardhi yote ya Dar ipimwe, Kila mmiliki wa ardhi apewe hati yake na wenye umiliki wa mashamba au kiwanja wapewe hati zao na taratibu za kuuza viwanja kwa wale wenye mashamba...jiji letu liwe safi.

Naimani kuwa kupimwa kwa ardhi kutaepusha Migogoro mingi ya ardhi Dar na Tanzania kwa ujumla na viwanja kuuzwa mara mbili mbili..

Pia hii itasaidia kwani pia Katika upimaji wa ardhi baadhi ya maofisa si wasafi, wanafanya kupima ardhi ni mtaji wao...utaenda kusema una ardhi yako unataka upimiwe, wewe umenunua shi. M5 wao watakuambia wanakupimia kwa M6....bora ardhi yote ipimwe....Mtu akijenga nyumba ziwe na Namba kama walivyofanya nyumba za Sinza...Itawezesha pia Kupata adress ya nyumba husika iwapo mtu anataka kufika sehemu fulani...

Naimani kama maeneo ya Sinza sasa mtu akiagizwa anaweza ambiwa Nenda Mtaa Fulani nyumba namba fulani...Ila sehemu zingine za Dar hakuna hiyo....utapita uchochoro hadi unaweza tokea msalani mwa mtu.

Wale wanaonunua Mashamba kisha wanauza wawe na umiliki wa mashamba yao kisheria na akija uza umiliki ule anahamisha kisheria...
 




Kwanza ningependa kukupongeza kwa juhudi zako za kutaka kuliboresha jiji letu hili la Dar. Nimekuwa nikifuatilia juhudi zako tangu ulipokuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni. Naamini jitihada zako za kutaka kuboresha wilaya ya Kinondoni ndizo zilizomfanya Raisi akuongezee majukumu kutokana na kuona jinsi unavyochapa kazi.

Kwa muda sasa nimekuwa nikiona unaibuka kila siku na matamko ambayo baadhi ya matamko hayo hayajafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa mfano suala la ombaomba. Kwa ushauri wangu kabla ya kutoa matamko naomba ufanye utafiti mdogo kwanza na kujiridhisha na kuweka mpango kazi wa namna ya kutatua tatizo kabla ya na kutoa tamko kwamba hutaki jambo fulani katika mkoa wako. Kuna vita vingine hutaviweza zaidi ya kujifedhehesha.

Kwa ushauri wangu naomba uweke vipaumbele katika mambo yafuatayo.

=Kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati katika shule zetu

=Kuongeza na kuboresha maabara katika shule zetu

=Kujenga maktaba katika shule na maeneo mbalimbali kwa kuanzia ngazi ya kata na kuhakikisha kunapatikana huduma za inteneti na magazeti ya kila ziku hapa unaweza kuzishirikisha kata kutenga maeneo kwa ajili ya kujengwa kwa maktaba hizo ili kuhimiza watu kujisomea na kuongeza maarifa na sio kupiga soga vibarazani na kunywa kahawa

=Kuhakikisha jiji linakuwa safi kwa kuweka sheria ndogo ndogo kali zitakazowabana wachafuzi wa mazingira na ili kulitekeleza hili unaweza kupata uzoefu kutoka kwa viongozi wa mji wa Moshi

=Kupiga marufuku mifuko ya plastiki kutumika hapa jijini na badala yake wenye viwanda hivyo kulazimishwa kuzalisha mifuko ya karatasi kwa ajili ya matumizi au kushirikiana na SIDO kuja na njia mbadala ya mifuko ya karatasi ambapo ubunifu huo unaweza kuwezesha vikundi vidogo vidogo vya vijana na kina mama..

=Kutengeneza maeneo ya vivutio kwa watalii wanaokuja katika jiji letu kwani wengi hupita tu kwa sababu hakuna vivutio. Hili unaweza kuwashirikisha wabunifu na wakandarasi wetu na kutenga maeneo ambayo yana historia na kuyaboresha kwa kiwango ambacho kitavuta wataalii wengi kutumia siku kadhaa katika jiji letu kwa mfano kama mji mkongwe wa Zanzibar, na Makumbusho ni eneo mojawapo ambalo linaweza kuboreshwea zaidi.

=Kuweka utaratibu mzuri wa boda boda, kwa sasa bodaboda pamoja na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Dar lakini zimekuwa ni chanzo kikuu cha ajali hapa jijini na vijana wengi wamekufa au kupoteza viungo na hivyo kutishia nguvu kazi hapa nchini. Tusipoweka utaratibu na kutoa elimu kwa waendesha bodaboda na madereva kuheshimu sheria za barabarani na kuweka sheria kali kwa watakaokiuka miaka kumi ijayo nchi hii itakuwa na ukosefu wa nguvu kazi.

=Tenga maeneo mengi kwa ajili ya vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi na maeneo haya yakabidhiwe VETA ili vijana ambao wameshindwa kuendelea na masomo wapate fursa nyingine ya kujifunza masomo ya ufundi lakini pia ni vyema kukitengwa maeneo ya mafundi wetu kwa mfano mafundi wa magari kuwe na eneo lao, mafundi seremala wae na maeneo yao kama vile Keko, mafundi wa kuchomea vyuma wawe na maeneo yao ili wenye kuhitaji huduma hizo wawe wanajua zinapatikana wapi na kuondoa hizi vurugu mitaani

=Rejesha viwanja vya michezo vilivyovamiwa na hakikisha swala la viwanja vya michezo linapewa kipaumbele, na michezo isiwe ya aina moja, ongeza wigo wa michezo mbalimbali ili na sisi tuweze kushiriki michezo ya olimpiki.

=Mabango na matangazo yawekewe utaratibu maalum siyo kila mtu akiwa na tangazo lake anapita mitaani na kuchafua kuta za watu itungwe sheria kuondoa tatizo hilo n ahata haya makampuni ya matangazo nayo pia yawekewe utaratibu maalum kuondoa mabango mengi mitaani na kufanya jiji lisionekane nadhifu.

=Wanaohubiri usiku kucha na kelele za mziki kwenye mabaa katika makazi ya watu zipigwe marufuku na kila Pub kama watataka kupiga mziki kwa sauti ya juu basi lazima wawe na ukumbi usioruhu sauti kutoka nje.

=Njoo na njia mbadala ya kuhimiza matumizi ya baiskeli kwa wale wanaofanya kazi maeneo ya karibu na hili litafanikiwa kwa wakandarasi wetu kubuni njia ya waendeshao baiskeli ili kuepuka bughdha kwa watembeao kwa miguu. Mpango huu unaweza kuanza na zile barabara ndefu kama Tegeta mpaka Posta, Gongo la Mboto mpaka Posta, Mbagala mpaka Posta.

Mimi naamini kama ukiweka vipaumbele kwenye mambo hayo machache kati ya mengi ambayo sijayazungumzia utaacha historia katika jiji hili na utakumbukwa na vizazi vijavyo.

Unaweza kuitisha mdahalo kwa wakazi wa jiji hili ili kupitia mdahalo huo uweze kuibua mbinu mbalimbali za kuboresha jiji letu. Naamini wakaazi wa jiji hili hawafurahishwi na hali jinsi ilivyo kwa sasa na wangependa hali iwe nzuri zaidi kwa kuondoa kero nilizozitaja hapo juu, iwapo utawaalika kwenye mdahalo watakupa ushirikiano.

Nakutakia kila la kheri katika majukumu yako ya kila siku.

Ni mimi Mzee Mtambuzi.


HII tabia ya kumuvuzisha Thread hii siipendi kabisa...Kila thread ina vionjo vyake hata kama ushauri Unafanana au Jambo linafanana....Points ni tofauti (Same Jubject but different Contents)
Thread ikihamisha inaenda kuwa kama comments tuu...wakati unataka iwe ndio KUU..
Kwani ni daftari hili unahofia litajaa..?
 
MNYONGE mnyongeni haki yake mpeni. Paul Makonda anastahili pongezi kubwa na za dhati kabisa kwa mkakati wake wa kujenga Dar es Salaam mpya ambapo amekuwa akifanya ziara jijini humo akisikiliza kero za wananchi na kuzitolea majibu papo hapo kwa kutumia wataalamu wake. Hapa ndiyo tunaona hasa ile ‘spirit’ ya hapa kazi tu.

Tumezoea kuona wanasiasa wanaowawakilisha wananchi katika vyombo mbalimbali, ikiwemo bunge na halmashauri ndio wanaofanya vikao hivi kwa lengo la kupokea na kupeleka kero hizo kunakohusika. Katika hali ya kawaida, mwanasiasa hatoi utatuzi wa kero hizo mwenyewe.

Lakini mkakati wa Makonda umetengeneza njia ya mkato ya kushughulikia kero za wananchi. Makonda kama kiongozi wa serikali (executive branch) kwa msaada wa wataalamu wake anaweza kutoa majibu ya kero papo hapo.

Kinachofurahisha zaidi ni kuona kuwa Makonda amekuwa mkweli. Tofauti na wanasiasa ambao panapotakiwa jibu kuwa ‘hapana’ atasema ‘tutaangalia..’ na hivyo kuwapa imani ya uongo wananchi, Makonda amekuwa haogopi kusema hapana, kama nilivyoshuhudia akimjibu mmoja wa wakazi wa maeneo ya mabondeni aliyekuwa akitetea kuwa eneo analokaa hamna mafuriko, wakati taarifa za kitaalamu zinasema ni hatarishi.

Ukimuangalia Makonda, unatamani wakuu wote wa mikoa na wilaya wangekuwa na ‘spirit’ na mikakati ya ubunifu wa kazi kama yake. Labda wanafanya hayatangazwi maana wakati mwingine wakuu wa mikoa na wilaya wa mijini wanakuwa na faida ya kuwa karibu na vyombo vya habari.

Wapo wanaomkosoa Makonda akiwemo mtu mmoja ambaye kupitia ukurasa wake wa Facebook alihoji umuhimu wa zoezi hili wakati kipindi cha kampeni CCM walinadi ilani ikimaanisha kuwa tayari wanayajua matatizo ya wananchi. Kwa maoni yake alidai kwenda kwa wananchi kuwauliza kero zao tena ni kupoteza muda na badala yake ingefaa tu kufuatilia utekelezaji wa ilani iliyowapatia kura.

Nadhani aliyeandika vile alisukumwa na hisia za kisiasa zaidi maana tunajua kuwa licha ya uwepo wa ilani, ni wajibu wa wawakilishi wa watu (wabunge na madiwani) kukutana na wananchi kusikiliza kero zao na kuwasemea. Tofauti hapa ni kuwa aliyefanya hivyo ni mkuu wa mkoa.

Pili, haihitaji akili nyingi kujua kuwa changamoto za wananchi zinabadilika. Yaliyokuwa yakiwakwaza jana siyo yale yanayowakwaza leo au yameongezeka au yamepungua. Hata mpango wa miaka mitano, huwa unapitiwa kila mwaka na kuboreshwa. Vilevile, zipo kero nyingi za watu binafsi ndogondogo za udhaifu wa kiutendaji ambazo zinahitaji kushughulikiwa.

Mifumo imekufa?

Lakini, licha ya hayo yote niliyotaja katika kusifia, ukisikiliza malalamiko mengi ya wananchi yaliyokuwa yanatolewa tangu zoezi hili lianze utagundua kuwa kuna udhaifu katika mifumo yetu ya utoaji haki na huduma mbalimbali.

Nina maana kwamba, kujitokeza kwa watu wengi wenye malalamiko binafsi, wanaoshitaki kudhulumiwa mali zao kama viwanja, nyumba na kadhalika inaonesha kuwa mifumo yetu bado si rafiki vya kutosha kiasi cha kuwawezesha wanyonge kufikisha malalamiko yao na kushughulikiwa hadi kupatikana suluhisho la hai.

Vinginevyo, kungekuwa na hiyo mifumo rafiki na inayofanya kazi bila mizengwe na rushwa, kusingekuwa na watu wenye malalamiko binafsi ambayo yangeweza kutatuliwa na vyombo husika katika utaratibu wa kawaida ndani ya mfumo uliowekwa, na badala yake tungesikia zaidi kero za jumla za wananchi wa eneo husika, kama ukosefu wa maji, umeme, usalama mdogo na kadhalika.

Sababu ya mfumo na utaratibu wa kufikisha na kushughulikia malalamiko kutofanya kazi ipasavyo zinaweza kuwa ni nyingi, ikiwemo rushwa, uzembe, uchache wa watumishi ukilinganisha na mzigo wa kazi na kadhalika.

Lakini pia kwa upande mwingine, huenda wa kulaumiwa siyo watumishi. Huenda wananchi hawana elimu ya kutosha juu ya namna ya kufikisha malalamiko yao kwa maana hawajui waapi pa kwenda. Kwa hiyo ipo haja ya elimu halmashauri kuwa na vipindi vya redio, TV na makala za gazeti na mitandaoni za kuelimisha namna ya kufikisha malalamiko na pia namna ya kuhakikisha yanashughulikiwa ikiwemo njia za kukata rufaa vyombo vya juu.

Huwezi jua, huenda Mkuu wa Mkoa mwingine asiwe na utaratibu kama wa Makonda wa kufanya mikutano ya kusikiliza malalamiko, na ikiwa hivyo maana yake wananchi wataishia wakinung’unika serikali mbaya.

Ushauri kwa Makonda

Katika utekelezaji wa mpango huu wa ziara za kuibua kero na hatimaye kujenga Dar es Salaam mpya, nina ushuari mdogo kwa Makonda. Si ushauri mpya lakini nauleta kwa msisitzo maalumu.

Ziara hizi za ujenzi wa Dar es Salaam mpya zitumike kung’amua matatizo ya kimfumo yatakayowaongoza nyingi viongozi kurekebisha sheria, kanuni na taratibu za kiutawala na kisekta katika kuboresha utoaji huduma kwa jamii.

Nilimsikitikia sana yule mwenyekiti aliyeswekwa ndani kwa sababu ya kutotumia risiti halali. Karibu wenyeviti wengi wamekuwa wanafanya hivyo. Kuandikishiana mikataba ya mauziano ya vitu ni biashara kubwa hapa jijini na wenyeviti wamekuwa wakichukua asilimia 10 ya kila dili.

Sasa basi, kimaliza ziara yenu rudini ofisini, andikeni waraka na miongozi mbalimbali na muigawanye kwa wanaostahili iwe miongozo. Kwa namna hiyo ziara hizi zitakuwa zimezaa faida kubwa katika uboreshaji wa utawala bora na huduma za kijamii.
 
Wananchi tunachotaka ni bei nafuu na na inayoeleweka. Hakuna kitu kinaboa kama kupoteza muda una bargain nauli ya taxi mwisho wa aoku mnashindwana. Madereva taxi acha wanyoshwe tu na Uber wapate akili waanze fanya biashara aystematic. Inakuwaje watu wawili wakucharge rate tofauti kwa kwenda sehemu moja, it makes no sense kwa kweli.
Uber waachwe wafanye biashara yao, huwezi kutaka linda wafanyabiashara wa ndani kwa kutaka mbembesha mzigo mwananchi wa kawaida.
Maana mwisho wa siku Uber hawajaja na taxi zao hapa, taxi zitumikazo ni za hapa hapa kwetu.
 
Inaweza kuwa pongezi,maoni,ushauri,dukuduku,pendekezo nk kuhusu mh Makonda na utendaji wake.

Me namwombea mungu ampe hekima na busara, hilo tu
 
Ajiuzulu kwa kuwa mkuu wa mkoa wa kwanza kuiingiza Dar shule zaidi ya tano katika kumi zilizofanya vibaya mtihani wa Taifa kidato cha kwanza
 
Asifuate what's trending ktk harakati..za kupambana na powder ktk nchi zilizoendelea siyo mbaya Si kajitoa mhanga.
Asijekuwa an epic fail huko mbeleni...
[HASHTAG]#personalpointofview[/HASHTAG]
 
Kaza buti, tunachosubiri ni utaje mapapa wa mapapa ya madawa ya kulevya.

Usipotaja na mie nitakuona BOMU.
 
Nampenda makonda napenda utendaji kazi wake ila naona kma mambo mengi anafeli sju kwanini alianza na waali usafir wabure sjui iliishia wapi akaja namba na anuani kila nyumba sjui illishia wapi akaja na mti wangu dar sjui imeishia wapi akaja na mashoga sjui meishia wapi akaja na dar mpya sjui inaendelaje akaja na shisha sijajua mafanikio yake zaidi ya kuskia kina siro wakihongwa na mengine mengi tu sasa hii kubwa lao madawa ya kulevya nayo sjui itakuaje manake naona kina msukuma wameanza kumpa za uso
 
Ndugu Makonda kutokana na maneno yanayopatikana kwenye maandiko kuwa, toa kwanza boriti ndani ya jicho lako ndipo utoe kibanzi kwenye jicho la mwenzio, sasa ni wakati muafaka wa kuelezea umma juu ya tuhuma mbalimbali zinzotolewa dhidi yako!
..Kuhusu hili suala la mapambano ya madawa ya kulevya inasemekana kuwa kuna watu umewaficha umedeal na vile vidagaa, kwamba safari yako ya marekani na Paris, fedha ulitoa wapi? Na kuhusu mali zako, tolea ufafanuzi.
Inasemekana pia umempangishia Masogange aliyekuwa msafirishaji wa ngda na hata kutiwa mbaroni..! Je ni kweli na ukaribu wenu unatokana na nini na kwa nini hukimtaja kwenye list yako ya watumiaji!
Tueleze pia suala la shisha ulilokuwa ukilisemea kwa ukali limefikia wapi, umekamata watuhumiwa wangapi na hatua zipi zimekwisha chukuliwa!
Mashoga nao wamekushinda, hakuna update yoyote tunayoipata kwamba mashoga kadhaa wamekamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki!
...Bila kusahau tupe maendeleo ya miti yako!
 
Ndugu Makonda kutokana na maneno yanayopatikana kwenye maandiko kuwa, toa kwanza boriti ndani ya jicho lako ndipo utoe kibanzi kwenye jicho la mwenzio, sasa ni wakati muafaka wa kuelezea umma juu ya tuhuma mbalimbali zinzotolewa dhidi yako!
..Kuhusu hili suala la mapambano ya madawa ya kulevya inasemekana kuwa kuna watu umewaficha umedeal na vile vidagaa, kwamba safari yako ya marekani na Paris, fedha ulitoa wapi? Na kuhusu mali zako, tolea ufafanuzi.
Inasemekana pia umempangishia Masogange aliyekuwa msafirishaji wa ngda na hata kutiwa mbaroni..! Je ni kweli na ukaribu wenu unatokana na nini na kwa nini hukimtaja kwenye list yako ya watumiaji!
Tueleze pia suala la shisha ulilokuwa ukilisemea kwa ukali limefikia wapi, umekamata watuhumiwa wangapi na hatua zipi zimekwisha chukuliwa!
Mashoga nao wamekushinda, hakuna update yoyote tunayoipata kwamba mashoga kadhaa wamekamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki!
...Bila kusahau tupe maendeleo ya miti yako!
Hapo kazi tu yote yatakaasawa tu mdogomdogo ndugu makonda kaza kiatu
 
Akija kukujibu au wakijitokeza wa kumsaidia kujibu nisitue nipo sebuleni naangalia movie.
 
Back
Top Bottom