Habari wakuu.
Kama mnavyoona hali ya kisiasa inavyoendelea nchini, na hasa ktk jiji la Dsm, matamko na maamuzi ya kila wakati na yanayoonekana kuwakera watu wengi kama yanavyoendelea ktk DAR MPYA, ni dhahiri kuwa mkuu wa mkoa anajijengea maadui katika mambo hasa mawili yasiyo ya msingi sana.
1. Kitendo cha kuwakamata watu wanaotoa kero zao.
2. Kitendo cha kuwatumbua watu ilhali hujawapa nafasi ya kujielezea zaidi.
3. Kitendo cha kuwatoa nishai watu wazima kwa maneno yasiyofaa.
4. Maamuzi anayofikiria kuyafanya ya kufuta na kuwafukuza kazi watu wa idara ya kilimo kwa madai kwamba kwa Dar, wanakula mishahara ya bure.
Kwanini nimesema awe anasali sana au atafute mganga mzuri sana?
Binafsi simfahamu na wala sina mpango huo, zaidi kujua kwmb ni RC wa Dar. Inshort ni kwmb SIIJUI IMANI YAKE, kama anamwamini Mungu zaidi au anaamini nguvu za giza zaidi. Either of the two, itasaidia kujua achague kusali sn au mganga mzuri.
Ni ukweli ulio wazi kwamba aliyoyafanya na anayoendelea kuyafanya yamemwongezea idadi kubwa sn ya maadui, ambao hajui nguvu zao. Anaowakamata au kuwazingua na kuwavunjia heshima, wengi ni watu wazima wenye familia zao. Hatujui wanajisikiaje na kama wanapanga kumkomoa, ni kwa style gani. Hao anaopanga kuwafuta na kuwafukuza kazi, ni watu wenye familia na dependants wa kutosha. Wanawaza nn juu yake, nobody knows...!!!
Sisemi kwamba aache anachokifanya, NO. Ila aangalie the best and positive way to deal with challenges. Na hana sababu ya kutafuta kupendwa na public au kufurahisha public ktk mikutano yake kwa kuwadhihaki watendaji wanaotakiwa kujibu maswali.
MY TAKE IS:
KIUKWELI unaumiza wengi. Na binadamu tunatofautiana ku-handle makwazo, na sisi binadamu wapo wenye visasi. Na ikumbukwe kwamba kuna different styles za REVENGE kutegemeana na imani ya mtu, mazingira aliyepo mtu, ushawishi alionao mtu kwa wakati husika, pamoja na malezi aliyokulia mtu. So, DO EITHER OF THE TWO, DEPENDING ON YOUR FAITH...!!!
Nawasilisha...!!