Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Changanya na zako maamy
 
Aweke vyeti mezani,hata alie machozi ya samaki hatutamwelewa,mbona simple tu ni kuweka vyeti tu.
 
Nimeamini, watanzania wengi mnaishi kwa kutegemea hela za wauza madawa ya kulevya, ndio maana Makonda kuanzisha vita ya dawa ya kulevya imewauma sana, maana mnaona mwisho wenu umefika.

Sasa ni hivi, vita ya madawa ya kulevya ipo palepale, hata mkipindisha ukweli vipi, na kututoa kwenye line ya kupambana na dawa za kulevya kwa kelele nyingi kiasi gani za maisha binafsi ya Makonda, mkatafute tu biashara halali mfanye, msitumalizie vizazi vyetu.

Vita ipo palepale

 
Reactions: Ame
Mimi nahesabu siku tu.
 
vita vya madawa sio kichaka cha kuficha vilaza wanaotumia vyeti vya wengine
kamanda sianga ndie amepewa hilo jukumu....na hatujawahi kusikia mtu akimshambulia sianga ktk majukumu yake.
huyo kiumbe anatakiwa tu ajibu tuhuma zinazomkabili.asihusishe tuhuma hizi na vita vya madawa ya kulevya.
 
Hata hivyo vyeti vyake havimuathiri mtu yeyote lakini madawa ya kulevya yanamaloza vijana
 
Hizi akili nyingine za kuku shida sana. Huu ni zaidi ya ubashite.

Kuombwa kutoa vyeti vyake kama kiongozi wa wananchi inahusiana vipi na madawa ya kulevya?!!
 
Tanzania tu ndio nchi pekee ambapo mtu kulia ni rahisi kuliko kuonyesha vyeti
 
Huyu Bwana hana jinsi ya kufunika ufidhuli huu!
Mamlaka yake ya ajira imeaibika sana!
Hana cheti huyo!
Saa hii haogopi kupoteza ajira Bali anaogopa jinai!
 
Mkuu wetu wa jiji la Dar tunakuomba usikatishwe tamaa na wahuni wachache wanaotumia mitandao kukuchafua kwa sababu za kitoto kabisa.Tulio wengi tuko nyuma yako.
 
Mkuu wetu wa jiji la Dar tunakuomba usikatishwe tamaa na wahuni wachache wanaotumia mitandao kukuchafua kwa sababu za kitoto kabisa.Tulio wengi tuko nyuma yako.
Sema mimi. Mlio wengi na nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…