Wana JF,
RC Makonda ni rafiki yangu sana tena wa karibu, siwezi thibitisha hizi tuhuma na unapoona rafiki yako matatizo au ana tuhuma lazima uwe karibu na yeye uangalie jinsi gani utamsaidia kwa mawazo, umfariji na umsaidie pale unapoweza, sasa basi namshauri kama ifuatavyo:
1. Kama kweli tuhuma zina ukweli ndani yake na ana uhakika kinachosemwa ni ukweli mtupu basi afute kiapo alichokifanya mahakamani kuhusu majina na abaki na majina yake yote original, hili alifanye kimya kimya.
2. Atafute center ambayo atafanya mtihani wa marudio ya form 4 au afanye mtihani wa QT baadae ajiandikishe kufanya mtihani wa form 4 atajitahidi ata pass nina uhakika. Hapa lazima atumie majina yake original bila ya kupoteza hata jina moja
3. Atafute chuo aanze na certificate kwa kutumia majina yake original bila ya kuacha hata moja, achukue diploma na badae degree. Kama ataona aibu akasome nje ya nchi pesa anazo inawezekana sio kusomeshwa tena maana haitaji.
[HASHTAG]#Tatizo[/HASHTAG] lililopo kwa sasa ni lipi
Kwasasa hawezi kupata kazi yoyote ile na popote pale hapa nchini labda ajiajiri maana swala hili hakuna mkuu wa shirika au taasisi au ofisi ambayo haina taarifa au mwajiri hajui media na magazeti yameandika ukizingatia ndio kila mtu hupata kujua nchi inavyoendelea na kupata taarifa mbalimbali, kwa hiyo tatizo hili ni kubwa sana, labda ajiajiri au afanye biashara.
Nasema haya kwakuwa umri wake bado unamruhusu, pesa alizopata na madaraka alishawahi kuwa nayo isimpe kiburi kuwa huko ni chini la hasha, kwanza itamsaidia hata akionekana miaka hiyo ijayo atakuwa na ujasiri wa kuonesha vyeti vyenye majina yake original ambavyo ukiambatanisha na barua ya mwenyekiti wa kijiji alikozaliwa lazima atakuwa na heshima yake na hatakuwa wa mchezo mchezo.
Sina ushauri zaidi ya huu, vinginevyo atakuwa si kitu maana atakuwa ai mtu wa kukaa na watu na kuwa na ujasiri, ataona aibu kuwa kila mtu anamfahamu hata mtoto mdogo.
Kila mtu ana udhaifu wake na kuna makosa ambayo wengi tumeshawahi kuyafanya ila tuliomba kusamehewa na tulikubali kujirekebisha mabaya tuliyo yafanya tuli tubu na tuliomba msaada ili tuondokane na hadha au aibu.
Msinielewe vibaya huu ni ushauri wangu binafsi kama rafiki wa karibu sana. Mashambulizi sitaki muwe wastarabu maana kama kuna kosa alilolifanya yanamhusu mwenyewe.