Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

wewe lazima utakuwa mbunge wa ulanga
Haha, duh aisee, unenihukumu bana. Sio kihivyo, unajuwa sio watali wote wanapenda kwenda kwenye sehemu za kifahari. Ukiipanga vizuri tandale inaweza kujiingizia kipato kama sehemu nyingine. Inabidi kufikiri nje ya box.
 
Haha, duh aisee, unenihukumu bana. Sio kihivyo, unajuwa sio watali wote wanapenda kwenda kwenye sehemu za kifahari. Ukiipanga vizuri tandale inaweza kujiingizia kipato kama sehemu nyingine. Inabidi kufikiri nje ya box.
SIO WEWE ULISEMA SANAMU YA BISIMINI IONDOLEWE IWEKWE YA DIAMOND KWELI? MAANA SI KWA MAHABA HAYO ULIYONAYO KWA DIAMOND
 
Wanabodi leo wacha nimpe sifa zake kijana mwenzangu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Huyu jamaa ni shida aisee yapaswa aandaliwe Tuzo kwa ajili ya kutambua mchango wake na kuweza kuwa mfano wa kuigwa na baadhi ya viongozi wengine.

Huyu jamaa ni jasiri kwanza haogopi na wala hamtetemekei mtu, hili unaweza lithibitisha kipindi hata akiwa hana cheo namna alivyoweza kumtolea uvivu Mh. EL jamaa alitamka live live tena mchana kweupe bila uoga kuwa jamaa hafai kuwa Rais wa nchi hii kwa vile ni mwizi na kwa kipindi kile kusema ukweli ilikua ngumu sana kwa mtu wa kawaida tu kuweza kumkurupukia bwana EL lakini jamaa alithubutu.

Swala la pili, huyu jamaa ni mbunifu wa kiwango chake alianza kipindi akiwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mkakati wa kuitisha vikao na wananchi wake na kusikiliza kero zao na kuzitatua papo kwa papo zile zinazowezekana na kuahidi kuzitatua zile zinazohitaji muda kidogo. Hapa hata wale wafanyakazi waliokuwa chini yake waliiona jamba jamba maana kama kero ilikua ikihusu idara yako ilitakiwa ujieleze ni kwa nn tatizo hilo lipo na wewe hujalifanyia kazi.
Wapo waliopoteza ugali wao na wengine waliongeza umakini zaidi katika utendaji kazi. System hii imeendelea hata kipindi hiki akiwa Mkuu wa mkoa anakutana na wananchi wake na kutatua kero zao.

Swala la tatu ni katika ulinzi wa amani ya jiji la Dar es Salaam. Hapa kweli napo ukibisha kuwa jamaa hajafanya kazi utakuwa na matatizo yako binafsi, Dar si Dar ya vibaka tena kama enzi za nyuma hii ni kutokana na kudhibiti vilivyo mianya mingi ya kuzalisha vibaka, watuta unga, bangi, wanywa viroba, wakaa maskani sasa nadra sana kuwaona na hawa wote walikuwa chanzo cha uhalifu ktk hili jiji.
Issue za ujambazi zimepungua sana kama si kuisha kabisa maandamano uchwara ya wenzetu hakuna kabisa, vi mikutano visivyo na kichwa wala miguu hapa Dar es Salaam vimeyeyuka ama kweli huyu ni kiongozi anayestahili cheo zaidi ya alichonacho.

Swala la nne, uthubutu, jamaa anauthubutu wa kufanya kile anachokiamini kuwa ni sahihi na kinawezekana sema anakwamishwa na wanafiki wachache wa kujifanya wapinzani. Jamaa alisimamia issue ya madawa watu wakamdhihaki sana pongezi zangu ziende kwa Rais mpendwa Mheahimiwa sana John. P Magufuli kwa kumuunga mkono, alipambana na ma Giant yaliyokuwa yanaogopeka nchi hii ma drug dealers makubwa bila woga wa kupoteza uhai wake. Tukumbuke kuna viongozi wakubwa walishindwa hata kuthubutu kutaja majina tu ya wauza madawa lakini jamaa aliweza tena na kuwahita wakahojiwa.
Wengine walileta mbwembwe nadhani kila mtu anajua kilichoendelea.

Uwezeshaji wa wasanii, kupiganoa haki za wasanii ili waweze kunufaika na kazi zao, kupigania haki za wafanyakazi wa kada mbalimbali mfano waalimu kupanda daladala bure, kugawa viwanja kwa wafanyakazi, kuja na mkakati wa kuwa na eneo moja la wafanya biashara za magari (Yard) ili kuwarahisishia wauzaji wa wanunuzi, utunzaji wa mazingira kwa kuanzisha kampeni ya kupanda miti. Kwa haya machache na mengine huyu kijana anastahili pongezi.

Popote ulipo kijana mwenzangu hongera sana na endelea kuchapa kazi usiwasikilize wanafiki wanaokukatisha tamaa kumbuka kelele za chura haziwezi mnyima tembo kunywa maji, na hata ungefanya nini usitegemee binadamu wote watakusifia ndio binadamu tulivyoumbwa ila ipo siku watu watakukumbuka, rejea Rais kikwete watu walimuita dhaifu ila haohao sasa hivi wanamsifia.
Fanya kazi kadri ya uwezo aliokujalia mwenyezi Mungu yeye ndio atakaekulipa kwa yale unayotufanyia wana Dar es Salaam na sio sisi.
 
Jamaa kwa uthubutu tu anao tena wa kiwango cha juu sana.kwa point hiyo amejitahidi sana lakini madhaifu yake makubwa ambayo yanafanya watu waseme huku mitaani ni namna ambavyo ana wa treat wafanyakazi katika halaiki bila kujali heshima zetu za kiafrica nadhani hilo ndilo ambalo watu wengi hawapendi.

Ni kweli kila mtu anamadhaifu katika kutimiza majukumu yake na hakuna ambaye yuko perfect 100% lakini hiyo hali ya kudhalilishana mbele ya umma wengi kweli hawapendezwi na hali hiyo.
 
Jambo la kusikitisha ni kwamba watanzania wengi tumekuwa wajinga na washamba wakubwa wa kisiasa. Utendaji wa Paul ukiwa na akili timamu utagundua namna anavyojutuma kwa moyo, Kwasababu halazimishwi.. tazama wenzake walivyolala.

Inasikitisha sana kuona watanzania walidai wauza madawa wanaogopwa, kazi ikaanzia kwa watumiaji ili tubaini nini kipo mbele watanzania wakaleta mambo ya vyama tena hadi kwenye sumu hii inayoua watoto wetu. Huu ni upovu, ushamba au ujinga?
 
kwanza rekebisha jina
anaitwa daudi albert bashite wa kolomije
jina paul makonda ni la wizi,alifoji vyeti baada ya kupata zero form four pale pamba secondary mwanza
nafikiri nimeweka rekodi sawa
Acha kuropoka mkuu kuhusu jambo usilolifahamu
 
Back
Top Bottom