Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

makonda/bashite ana kiwango kidogo sana cha kuelewa mambo sijui alisoma wapi huyu mtu. ila mkuu umechambua vizur lakini hawezi kukuelewa
 
Ama hakika Wewe ndiye Mkuu wa Mkoa ambaye yawezekana tokea wawepo Adam na Hawa hapajawahi kuwa na Mkuu wa Mkoa anayejituma kama Wewe hasa Kiutendaji / Kiuwajibikaji ( hasa kwa kuja na matamko ) na nahisi pengine hata huko Mbinguni tukienda na kukuta kuna Mikoa unaweza pia ukaukwaa huu huu Ukuu wako wa Mkoa.

Mimi nawashangaa sana Waswahili jinsi ambavyo hawakuelewi hasa katika mambo yako mengi ambayo huwa unayafanya hasa kwa Mkoa huu wa Dar es Salaam ila bahati nzuri Mimi GENTAMYCINE huwa nakuelewa vyema halafu haraka mno.

Yafuatayo ndiyo mema na maono ambayo mara kwa mara humtokea Binadamu mmoja tu aitwae Paul C. Makonda:

  1. Kati ya tatizo la Usafiri kwa Wanafunzi na Wanawake kuachika na Kuzalishwa na Waume zao Kwa Makonda suala la Wanawake hao ndilo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
  2. Kati ya tatizo la Uchafu katika Jiji la Dar es Salaam na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
  3. Kati ya tatizo la Vibaka katika Jiji la Dar es Salaam na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
  4. Kati ya tatizo la Mfumko wa Bei katika Bidhaa hasa kwa Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
  5. Kati ya tatizo la Maji kukatika hovyo katika Jiji la Dar es Salaam na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
  6. Kati ya tatizo kubwa la Foleni katika Jiji la Dar es Salaam ambalo ' Kiuchumi ' linaigharimu sana nchi na Wanawake kuachika na kuzalishwa na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
  7. Kati ya tatizo kubwa la Wafanyabishara ndogondogo ' Wamachinga ' kunyanyasika na kusumbuliwa na Askari wa Jiji la Dar es Salaam hadi na Watu wa TRA huku na Wao wakiwa wanasaidia Kukuza Uchumi wa nchi na pato lake na Wanawake kuzalishwa na kuachika na Waume zao kwa Makonda suala la Wanawake hao ndiyo Kipaumbele chake Kikuu kwa sasa.
Makonda Wewe piga Kazi tu ' Baba ' kwani uko vizuri sana na tunakukubali hasa Mimi kwani nakumbuka tokea ' Uteuliwe ' kuwa Mkuu wetu wa Mkoa ulishatutolea zaidi ya ' matamko ' kama 20 hivi na kuonyesha kuwa uko vizuri Kiutendaji na aliyekuteua hakukosea kabisa mpaka muda huu umeshaikamilisha 2 huku hiyo 18 iliyobaki ikikungojea Kwanza umalizane na hawa Wanawake waliozalishwa na kuachika na Waume zao.

Mimi nakuelewa mno ila nashangaa sijui kwanini Waswahili hawakuelewi au sijui wana Wivu tu nawe!

Nawasilisha.
umemuelewa vizuri sana,sijui kama ataelewa kama umemuelewa
 
Mkuu GENTAMYCINE Naungana na wewe kabisaa mkuu wa mkoa wetu mpendwa katika bwana mtume na nabii Paul C.Makonda anafanya kazi kubwa sana sijui kwa nini wengine hawataki kumkubali kama mimi na wewe tunavyomkubali, mkuu wachache watakuelewa wengine tuwapuuze tu mradi limetokea jina makonda wanapaniki
Umetumwaaa
 
Makonda njoo uone watu utendaji wako haukidhi vigezo Papaa GENTAMYCINE na wengine wenye akili wanakuona sasa unapotoka kwa kuanzisha hoja ambazo hauzimalizi na umekua wewe wa matamko tu na sio ubunifu kiutendaji. lakini tunakuelewa sana Makonda wetu
 
Precisely.

Mkuu Genta andishi bora kabisa hili kwenye post yako namba moja. Sasa utashangaa mtu ambaye ana matamko 20, mawili tu kayi ya hayo ndio yametekekezwa akijisifu ni mchapa kazi na huku akijigamba kwamba 2020 akigombea atashinda kwa kishindo. na kweli uchaguzi ukifanyika zinatokea figisu za kufa mtu kama mabox ya kura kutolewa ndani ya chumba na kurejeshwa yakiwa na kura kisha yeye kutangazwa mshindi halafu wanatokea wati kusema kashinda kwa kishindo baada kuona uchapa kazi wake.
 
Genta uko vizuri upstairs. Ila sina uhakika kama utaeleweka km ULIVODHAMIRIA! Kwa maoni yangu: Sisi wa Pwani tuna msemo wetu: SIKIO HALIZIDI KICHWA!
 
Kwa mwandiko huu hata mimi bwana makonda namuelewa sana.
[emoji2][emoji23][emoji2][emoji23][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Fasihi ndio mpango mzima, mm naungana na waliokuelewa. Genta nimekuelewa sana. Hakika uko vizuri. Lakin huko mbele za haki asitarajie kupewa hayo madaraka maana sidhan kule kama yohana atakuwepo.
 
Back
Top Bottom