USHAURI: Nani asimame kati ya Baba mlezi na Baba mzazi kwenye send off na harusi!!

USHAURI: Nani asimame kati ya Baba mlezi na Baba mzazi kwenye send off na harusi!!

Habari wana jf kuna ishu inachanganya huku, kuna harusi miezi 3 ijayo sasa huyu binti anayeolewa anababa yake mzazi ambaye Hakushi naye alikuwa anaishi na mama yake wa mzazi wa kumzaaa na baba wa kufikia, Sasa kwenye malezi Baba wa kufikia ndo alikuwa ana muhudumia kila kitu na alikuwa anaishi kwake lakini Baba yake ambaye alikuwa na ndoa nyingine kahusikia kwenye malezi kiasi kidogo sana tena sana, na kwenda kwa Baba mzazi alikuwa ni likizo tuu kama 2 weeks anarudi kwa mama na baba wa kufikia.

Sasa kapata kigugumizi kuhusu wapi apeleke mchumba wake apeleke posa na pia wapi mahari ikatolewe pamoja na wapi afanyie send-off wake kwa Baba yake mzazi au malezi?

Baba mlezi kamwambia kuwa aende kule kwa Baba yake mzazi iringa. Ila binti anaona Baba yake mzazi hakuusika hata kwenye malezi alimuacha kwa mama yake akiwa na umri wa mwaka 1 na yeye kuoa mwanamke mwimgine. Kuna kipindi akimuomba hata pesa kidogo mzee anazungusha maneno tuu.

Sasa send off ifanyike iringa au dsm anapoishi na mzazi mlezi?
Na kama dsm nani aiandae sherehe hio?
Na kuna zawadi anataka kuotoa ya Alphard gari kwa Baba mlezi coz alimlea kama mwanae wa kumzaa bila kubagua na hata baada ya kumaliza chuo alimsaidoa kumtafutia kazi na pesa kidogo alimpa.
Na ikifanyika iringa zaiwadi ya gari ampe mlezi kule iringa.

KAONGEA NA WATU WENGI WAMEMWAMBIA KUWA AMSHILIKISHE TUU BABA MZAZI NA SIO BABA MLEZI. ITAONEKANA NI AIBU.
Zawadi iende kwa yoyote yule,ila suala zima la jambo hili basi lifikishwe kwenye chimbuko lake{Kwa Baba Mzazi} huko ndipo mizimu ya Kinyalu,wajinga na makabila ya chimbuko la iringa, kwenye milima ya kitonga akafanyiwe na Tambiko ili ndoa isiwe ndoano, suala zima la zawadi aangalie mapenzi yake yanaenda wapi.Wahenga tuliposema DAMU NZITO KULIKO MAJI basi muwe waelewa,

Ushauri wangu ndio huo,huu USASA/MODERNITY usitm tuzuzue tusije kuchanganyikiwa baadae,tuyaseme haya bado mapema sio mpaka toa itake kuvunjika ndipo mje mhitaji msaada humu tutakuchangia mawazo ya kukuponda ndipo MADA ZA KATAA NDOA zitarudi kwa kasi.

Sent from my V2204 using JamiiForums mobile app
 
Tuanze kwanza kwanini akukimbie?😂unaona? Una matatizo wewe
Ndani kina vimbwanga vingi ndugu yangu acha tu nilimpa kila kitu na yy akanipa kila kitu lakini sasa maraaa paap tukachana mpaka saivi sitaki tena kuowa
[Kata ndoa]
 
Tuulize sisi tukuelezee situation nzima mm mke wangu alikimbia na mtoto anampeleka kwao sasa vita ilikuja kwenye kumchukua ndugu zake walingaka kama chui alieguswa mkia
Ndio maana kumbe ulikimbiwa ngoja nikuignore tu mzee
 
Kiuhaisia baba yake mzazi yupo,hiyo zawadi ya gari iende Kwa baba mlezi,ila kwenye eneo la baba mzazi mbingu zinafahamu kuwa baba mzazi ni nani.usiingia kwenye changamoto za wazazi ,yeye afanye kulingana na protocol zinavyohitaji.Baba mzazi asimane mahali pake
Baba mzazi akiwa na akili na uwezo wa kufikiri vizuri hawezi kuruhusu sherehe ifanyike kwake. Mtoto ni wa kwake, uhuru wowote atakao mpa mtoto kuamua katika hili jambo,mtoto atafarijika sana na utakuwa ushindi kwa baba mzazi kumrudisha mwanae kiaina kwake.
Baba mzazi hatakiwi hata kushiriki sherehe japo anatakiwa kuchangia gharama kama tu anampenda mtoto wake na ana ndoto za kuja kuwa karibu nae huko mbeleni.

#maniisiomtotomalezindiomtoto
 
Ndani kina vimbwanga vingi ndugu yangu acha tu nilimpa kila kitu na yy akanipa kila kitu lakini sasa maraaa paap tukachana mpaka saivi sitaki tena kuowa
[Kata ndoa]
Ah sasa ulienda ustawi wa jamii kufatilia swala la custody ya mwanao? Nadhan ungeenda kule mkajadiliana kuwa bado unataka kuwa part ya maisha ya mwanao. Umlee. Umlipie matunzo, umlipie ada. Lazima tu ustawi wangeruhusu uwe unapata muda wa kuwa anakuja kukutembelea au wewe kwenda kumtembelea. Ila swala tu la mtu hafanyi any efforts, anadisappear afu anakuja ukubwani na kudai eti yeye ndo baba mzazi ni upuuzi
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Pumbavu wewe! Uzazi maana yake kuchangia mbegu ndiyo! Mbona mnageuza vitu kijinga? Uzazi ni nini sasa? Anakwambia alimlea kidogo! Ana mzani wa kupima kiasi cha malezi. Aende kwa mzazi wake aachane na laana hizo.
Kwa kuwa na mlezi yupo ashirikiane na mzazi wapokee mahari. Kwisha!!
Pumbavu mwenyewe ngese kweli we lazima utakuwa upinde sio bure. Lazima na wewe umetelekeza mtoto hulei ukitegemea eti biology nyokonyoko, sperm donor mkubwa wewe na bado mkitelekeza watoto jiandaeni kisaikolojia ukubwani.
 
Kwa baba mzazi hakumfai,Kama baba mlezi sio sehemu sahihi,Waende kwa Wajomba zake ,huko ndiko watakakokutana baba mzazi na mlezi.
 
Tumeshachoka kuwashauri kitu kimoja kila siku.

Kwenye complication ya Wazazi swala la mahari linasimamiwa na wajomba, msijitafutie laana ambazo baadaye mtaona mmelogwa kumbe hamna akili.
Mkuu Baba mlezi kamwambia kuwa aende kwa Baba yake mzazi iringa.
Baba mzazi yupo na si ndo kwamba yeye Baba mlezi ndo anataka posa apokee yeye No.
 
Back
Top Bottom