USHAURI: Nani asimame kati ya Baba mlezi na Baba mzazi kwenye send off na harusi!!

We ulikuwa mzembe tu
Huna hata katoto ka nje
Sasa una faida gani duniani
 
We ulikuwa mzembe tu
Huna hata katoto ka nje
Sasa una faida gani duniani
Haha mkuu. Ni maadili na kujipangia tu. Sitaki kuacha watoto nje ya mama Furaha wangu. Ndiyo msimamo wangu na nilijiambia kabisa sitazaa nje nikiwa kijana au ndani ya ndoa. Na hii pamoja na nidhamu tuliyojengewa na wazazi wangu (Pumzikeni kwa Amani) lakini niliona kwa ndugu waliozaa nje inakuwa ngumu Sana watoto kuchangamana na wanawake wanalogana na kudhuru Sana watoto wa Wanawake wenzao. Kuzaa nje ni tunakaribisha invisible war kwa familia kwa mambo ya tamaa tu. Kwani ukizaa watoto hata 10 na mke mmoja kuna Shida gani? Ila kila mwanaume ana maamuzi yake jinsi anataka familia yake iwe hasa nidhamu.
 

Aongee na Mama yake, uwe mjadala wao.
 
Respect [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Hii taarifa, wachangiaji wengi ni wale waliopitia hiyo changamoto.
 
Kabla ya kuchangia, unatakiwa kutafakari kwa kina na kumuomba mwenyezi Mungu akupatie busara katika kulikamua.
 
Matunzo alikuwa anatoa kidogo,yamkini ulikuwa ndio uwezo wake.
Hajawahi kukukataa,point ya matunzo ni very weak,suala la kuachana na mama yako pia ni weak,
Lazima ujue watu wanatofautiana,je unajua ni yapi yalikuwa yanamsibu mpaka matunzo yanakuwa kidogo,huyo ni baba yako tu provided alikupa alochokuwa nacho
 
Sijaona sehemu baba alikimbia majukumu,huyo mlezi anavyokwambia nenda kwa baba usidhani ni mjinga,mahari yako haiwezi kumwongezea chochote,ye alifanya sehemu yake kama mlezi,
 

We ndo umenena, hapaswi kujiingiza kwenye migogoro yao, ndoa asimamie baba mzazi ilq izo zawad kubwa ampe baba mlezi, swala la kuuliza apo kama angefariki mwili ungezikwa wapi kama sio kwa baba mzazi? Jamaa afanye kubalance ayo mengine awaachie wenyewe.
 
Mtoto alihitaji kulelewa sio kuzaliwa.
Alizaliwa bila kupenda,akapenda apate malezi Bora.
So hapo baba mlezi ndo muhusika na siye mzazi.

Kwenye swala la kipaumbere apewe baba mlezi ila baba mzazi naye hawapaswi kutengwa uko ni kutafta laana zisizo na ulazima,

kuhusu kipato na kutodumu na mama ake mzazi ayo huwezi kuyaingilia, ayo ni mambo ya wazazi hata uyo anayemuoa uyo binti yanaweza kumkuta waakachana pia.

Hawa wanawake nyie mnajifanya hamuwaujui! Mwanamke anaweza kuachana na wewe anajua kipato chako ni chalaki moja kwa mwezi alafu kwakua kabahatika kupata mtu mwenye kipato zaidi anampeleka mtoto kwenye shure za ghalama za juu then anakumbia lipia nusu kukukomesha ukikataa kua huwezi kuafford anamjaza mtoto maneno kua baba ako hataki usome and etc,

so ayo ni kuwaachia wao chamsingi kwenye ndoa ifanye iwe kawaida nenda kwa mzee pata baraka zake hata usipompa ela najua atafurahia kumuozesha mwanae iyo furaha ni barak tosha, then kwenye sherehe ya ndoa ndo mama na baba mlezi waachie wajiachie na mazawad yote wapeni wao apo kila mtu atakua amefurahi kwa nafasi yake na utatoka bila kuacha huadui na ndoa itakua ya baraka zaidi.
 
Vitu vingine bwana watu wanapenda kufanya viwe complicated tu Sasa apo mnajiuliza nini ? ebu kamsome jeffy huyu tajiri wa Amazon na mkasa wake yeye pamoja na baba yake mzazi unadhani kwa ile hela alionayo ameshindwa kumsaka baba yake mzazi eti kisa tu alimzaa? Huyu baba mlezi ndo amefanya kufika hapo alipo Sasa acheni mambo mengi sendoff iwe Dsm tu
 
Sherehe ya kumuaga binti anaeolewa anaagwa na anaoishi nao.
Sherehe ya sendoff itafanywa na aliokua anakaa nao. Huwezi kwenda sehemu hawakujui unawaambia wakuage na hawajawahi kukaa na wewe. Hapa sendoff ifanywe na mama wa binti na aliokua akikaa nao.
Mahali inaweza kutolewa kokote but kwa Baba mzazi wa mtoto itakua vyema ili kuunganisha ukoo na familia hizi mbili za Baba na Baba mlezi na mtoto husika.
Unahitaji kujua ukoo wako na wa mwenza wako kabla ya kuoana na Baba mzazi atajua vyema kuepusha ndugu kuoana.
Huenda Baba mzazi alikua hafanyi vyema katika makuzi yako lakini hadhi yake kama Baba mzazi inabaki palepale, suala la ukaribu wenu linategemea na ninyi wenyewe.
 
Ili kuondoa sintofahamu Aachane na mambo ya sendoff afunge tuu harusi na mume wake mtarajiwa . Tatizo mabinti kupenda show off ndio inachangia kuongeza haya mambo ya sintofahamu
 
Sijaona sehemu baba alikimbia majukumu,huyo mlezi anavyokwambia nenda kwa baba usidhani ni mjinga,mahari yako haiwezi kumwongezea chochote,ye alifanya sehemu yake kama mlezi,
Sio mimi ni rafiki yangu inamuhusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…