Ushauri: Niende Serikalini au nibaki private sector


Nakazia hoja: Labda kwa kumwongezea uzoefu; mm nimefanya kazi na Shirika la kazi duniani (ILO) mshahara mnono (ni x 3 mshahara serikalini) na hakuna kuchelewesha malipo, usafiri ni personal driving i.e. unakabidhiwa gari L.C hard top mali ya ILO uitumie kwa mujibu wa taratibu zao lakini ilifika mahali nikaOpt kuondoka kutokana na udhalilishaji; yan mtu mweusi unaonekana kama hujui kitu, huna lolote, ni umaskini wako tu ndo umekuleta hapa......
 
Sasa sijui unabisha nini
Sijakubaliana na wazo lako eti huko unazurura...... Huko kuna upimaji wa kiwango cha ufanisi wa kazi na unakuwa chini ya mkuu wa Idara (immediate boss wako) atakayekusimamia kuona unatekeleza majukumu uliyopangiwa kwa mujibu wa Job description yako. Zaidi tena, ni lazima uandike Taarifa ya kazi i.e. kile ulichokifanya kwa mwezi mzima. Hakuna uzururaji kivile ila sikatai Utegaji upo.
 
Kuna classmate wangu alipataga kazi halmashauri mwaka 2023 ila hakwenda kwa kigezo cha kuwa private amekaa baada ya miezu kumi na moja akaona mambo ya private hayaendi akaenda kulia utumishi kuwa alikuwa anaumwa sana ndo maana hakwenda kuripoti, utumishi wakampa barua. Na yeye aliluwa amepangiwa Tabora pia
 
Tabora nzega ni pazuri tu pia kwa kufanya maisha na swala la kuanza upya sio issue babe mizigo yako yote uje uendeleze ulipoishia
Labda kama una miladi huko dar ambayo unaona ikija nayo nzega itakufa bas bas huko huko ila kama unazungumzia vitu vya kawaida tu toka huko njoo tabira kwa speed ya ngiri bro
Chance hii haitakuja mara mbili Mechanical tupo wengi tu tunaotaman kupata kazi serikalini ww umepata gap ishi nalo
Waza tu baada ya contract yako kuishaje utarenew na ikitokea usiporenew itakuaje
Jitafakari mkuu nenda kachukue barua yako.
 
Private job security ndogo, pressure kubwa sana, na unatumika ipasavyo kwa kile unacholipwa. BTW sikiliza moyo wako
 
Private company hapana ni fitna watu wanarogana kuja jamaa alikuwa quality control kwenye hyo company ya mwanzoni niliyokuwa nafanyia kazi alikuwa na permanent contract jamaa alikuwa na msimamo sana kwakuwa yeye ni qc basi alikuwa kuna baadhi ya products ana zi reject walikuja kumuundia zengwe wakaja wakamsainisha new contract ambayo alikuwa analipwa mara mbili ya mshahara wake masikini hakusoma terms of contract basi akasaini kumbe ule mkataba mpya una sehemu una terminate mkataba wake wa permanent na aliopewa mpya ni wa mwaka mmoja yeye kaangalia hela tu mwaka ulivyoisha wakamla kichwa jamaa hakwenda mahakamani wala wapi akasema namwachia mungu ila alipoondoka akatuambia kuweni makini ikitokea kazi ombeni kweli niliondoka na wenzangu wengine bila mkataba kuisha baada ya kupata kazi sehemu nyingine mpaka leo mtu akiwa analingalisha eti serikalini na private kwasababu ya pesa naona hana tofauti na mwanamke anayeangalia mwanaume mwenye pesa wakati anataka kuolewa.
 
Private job security ndogo, pressure kubwa sana, na unatumika ipasavyo kwa kile unacholipwa. BTW sikiliza moyo wako
Pia Private mambo yanabadilika, kuna kipindi kampuni profit inashuka, na hapo ndo utaona punguza punguza ya kampuni...kwa ushauri wangu nenda Serikalini. Ila nenda pia ukajiendeleze kielimu na maarifa. Mafanikio ni mchakato
 
Aisee! Kumbe ww pia unao uzoefu na hao watu. Kwa bahati mbaya au tuseme kwa kutokujua, vijana wengi baadhi yao wanaangalia hapa karibu na kiasi cha hela atakachopata ndani ya muda mfupi na kusahau kwamba siku zinakimbia mno na mabadiliko ni mengi. Hao watu hawaangalii makunyanzi. Private Sector siku za mwanzoni utaona kama umefanikisha lakini baadaye wanakubadilikia.
Asante kwa kushare uzoefu wako. Huyo bwana 2in1 kama atatulia na kuzisoma comment kwa umakini atakuwa amejifunza kitu hapo.
 
1.Niliomba taasisi kubwa ya serikali mzee na ningepata huko nisingejishauri kwa chochote ningeenda sema nilikosa nafasi jina likabaki kwenye database ndio wamenipangia huko halmashauri sahv ambapo sikuombea ajira nimepangiwa tu
2.Mechanical Engineer
Mdogo wangu nikwambie ukweli tu.
Kama hiyo kazi ya serikali ingekuwa ni kwenye taasisi kama EWURA,TANAPA,BOT,TPDC ,TAZAMA hapo sawa ningekushauri uende serikalini lakini kwa hiyo kazi ya halmashauri ni kwenda kujitia umaskini tu na kibaya zaidi kwa hiyo fani yako hautajifunza chochote cha maana zaidi ya kuwa na maneno mengi kama dalali.
Kwa hiyo fani yako ukienda halmashauri utaenda kuwa fundi magari kwenye gereji yao ambayo huwa haipo active kivile maana gari zao zingine huwa wanazipeleka Temesa kwa ajili ya matengenezo.
Mwisho wa siku ndoto yako itakuwa tu uwe Supervisor wa gereji uanze kugombania cheo na wazee wakupige kipapai achana napo huko hakufai kabisa endelea kufanya private ili uwe smart kwenye kazi zako
 
Serikalini ni Job security tu,hasara yake ni kuwa unabweteka kuona kuwa bado una muda mrefu kazini,pili kuna mambo ya transfer za mara kwa mara,hapo Private ukikomaa kwakuwa pia mindset yako inasema "chochote kinaweza tokea at anytime" unaweza kukuta ndani ya muda mfupi umefanya mambo ya kutisha...
 
Serikalini tangu kuingie ma E GOVERNMENT serikali sio unyama siku hizi baki private utanishukuru
 
Umesema vizuri ila cjui unazizungumzia Halmashauri za kipindi kipi. Kwa sasa hivi 2025; Halmashauri kumechangamka sio kama enzi zile. Kwa Taaluma ya mtoa mada, huko Halmashauri wajibu wake ni pamoja na kumshauri mkubwa wake kuidhinisha manunuzi ya vipuri vya mitambo lakini pia zipo fursa nyingine nyingi zenye malipo a.k.a mbali na mshahara. Halafu kuna muda mwingi wa "kujiongeza" (personal projects). Changamoto iliyopo Halmashauri ni pale mwanzoni kabla mtu hujayasoma mazingira na kugundua ramani au pale mtu esp.new comers wanapoangukia mikononi mwa makomredi njaa pangu pakavu tia mchuzi.
 
Mkuu iko hivi private ni kwa ajili ya watu smart na competitive ambao wanajiupdate kila wakati ili kutengeneza impressive CV kuwavutia waajili wapya watakaokuchukua kwa dau refu zaidi.
Kama unajijua una kichwa kizito na mzito kujiupdate upstairs basi baki serikalini ili muwe kila mwaka mnaandamana kudai increament ya elfu 50 na uvae nguo za kuchakaa,soli ya kiatu iliyorika chini.
Ila watu wenye confidence huwa wanaingia private wanasaini mkataba wa mwaka mmoja au miwili na kabla mkataba haujaisha wanaandaa mazingira ya kupata kampuni mpya na kabla kampuni haijakutema unawatema wewe unarukia kampuni nyingine kwa maslahi makubwa zaidi.
Mfano mzuri mimi hapa tangu nimalize chuo imepita miaka 12 na nimefanya kazi kwenye kampuni 6 hadi sasa hivi nimechoka kuajiriwa nataka kujistaafisha mwenyewe nifanye mambo yangu binafsi wakati mtu wa serikalini atangoja hadi afike miaka 60 ndio anashtuka kuwa hatakiwi tena kazini.
 
Kaza hapohapo.. Kufanya kazi Halmashauri ni kipengele, labda uende huko kisha ukatafute namna ya kuhama.

My take.:
Endelea kupambana tu na hapo Private.
 
Serikalini kuna high job security but zero exposer na hakuna kukua.


Private exposer kubwa na kukua .

So ikiwa unahitaji kukaa sehemu waweza fikiria mambo Kama hayo.
Exposure kwenye mambo yapi na kukua kivipi??,huko kote watu wa kuwa na wanapata Exposure itategemena na mahali ulipo.
 
Ni kweli mimi baada ya kumaliza chuo niliwahi kufanya kazi halmashauri kama internship japo ni miaka mingi.
Nikayasoma mazingira nilichogundua ni kweli kuna watu wananufaika kwenye miradi ila si wote ni Mkurugenzi na Chief Engineer watu wa chini hawashirikishwi labda utaambulia hela ndogondogo za nauli ukitumwa ukabebe materials,so baada ya kuona hali hiyo nikaachana napo nikaendelea na mambo yangu mengine.
 
Umenena sawasawa. Umesema: "...private ni kwa ajili ya watu smart na competitive ambao wanajiupdate kila wakati ili kutengeneza impressive CV kuwavutia waajili wapya watakaokuchukua kwa dau refu zaidi."
1. Unadhani wasomi walioko kitaa sio smart na competitive halafu hawana CV zinazovutia? Kumbuka mshahara Private mara nyingi huwa ni negotiable.
2. Private Sector wanao mtandao wa mawasiliano baina yao. Ukiomba kazi huwa wanakufanyia usaili na kama huna "connection au mtu wa kukupigia debe" wanalo swali lao lile Ni kwa nini uliacha kazi huko na unataka kuja huku? Na je huku nako si utaacha kazi kama ulivyoacho kule? Badadaye hufuatilia utendaji wako na tabia yako huko ulikoacha kazi. Wakigundua madhaifu yako e.g. ww hapo udhaifu wako ni kutokutulia kazini i.e. ww ni mwindaji mashuhuri wa big salaries (Salary monger). Wanaweza wasikuchukue au wakaweka dau la chini ili ukatae kazi mwenyewe.
3. Sijakuelewa unaposema Kuji-update unamaanisha nini. Kusoma au Kupata mshahara mpya wa juu zaidi? Kama ni kusoma mbona hata hata ukiwa Halmashauri hukatazwi kujiupdate? Lakini uwe na sponsers vinginevyo unaishia Urusi frontline vs Ukraine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…