Ushauri: Nimekuta 'urine pregnancy test' kwenye kimkoba cha binti yangu

Ushauri: Nimekuta 'urine pregnancy test' kwenye kimkoba cha binti yangu

Una ndugu wa kike,i mean dada zako,mama yako mzazi au wadogo au ma mkubwa? Ongea nao watakusaidia ila kama uliwalea watoto kwa misingi ya ajabu(unawapa uhuru mwingi,pesa ndogo ya matumizi,hujali wanatatizo au hawana,unachelewa kurudi nyumbani) itakua kazi sana kumrudisha mstarini
Nikiyafanya haya Binti atatulia? Nawaza nitakavyomkuza Binti yangu mpaka kichwa kinauma.Mungu anisaidie.
 
Umezidi umbea baba lazma uwe na adabu uwez kufungua mikoba ya mwanao....

Mm uyo dada angu tu au mtoto wa kike siwwz kufungua vitu vyako hata chumban kwake kuingia

Kuweni na adabu

Sent from my SHV-E275S using JamiiForums mobile app
Utoto unakusumbua
 
Mtafute dadako,amchukue akampime,

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Ndio mkuu,samaki mkunje angali mbichi,mlee binti yako mbelen kadri uwezavyo ila baadae usijejilaumu kwa uzembe(kuna mabint wengine wamelelewa kimaadili ila kampan za marafiki zikawaharibu)
Nikiyafanya haya Binti atatulia? Nawaza nitakavyomkuza Binti yangu mpaka kichwa kinauma.Mungu anisaidie.
 
Lakini wanaume jamani, sasa mtoto wa miaka 14 unaweza vipi kumuomba penzi?
Mie nakushauri uachane na mila za kikwetu eti baba hawezi kuongea na mtoto wake wa kike, nakushauri upunguze hasira, ongea naye, mwambie madhara ya kufanya ngono utotoni tena ngono zembe, kama una mifano ya watu waliokufa kwa ukimwi mwambie, pia mwambie kuhusu rais alivyosema watoto wakipata mimba wasiendelee na shule, ila yote kwa yote ongea naye "friendly" tawala hasira zako.
Mi nahisi Kitu kama hiki kikitokea kwa Binti yangu sijui nitakuwa kwenye hali gani.
 
Ni kweli. Mzazi yoyote anayesema usimfatilie mtoto namshangaa. Halafu akiharibika unaanza kumlaumu mtoto wakati wewe mwenyewe mzazi ni tatizo. Wangu namlinda aisee..ni wa kike. Haendi sehemu bila mimi, bahati nzuri nina nafasi akiwa likizo nipo nae 24/7, ana miaka 13 sasa hivi..akifikisha 17 ndo nitamlegezea kidogo ila kwa sasa hapana aisee...
best mom.kudos
 
Labda hiyo test ni ya rafiki yake ... fanya kumfuatilia nyendo zake utajua ukweli. Kidisha private investigator akuletee file lake. Kupandisha pressure kutakumaliza bure .... ukiwa na watoto tegemea lolote ila uwe umewapa guidelines ili usijejilaumu bure kwa kukaa kimy.

Sent from my SM-N910H using JamiiForums mobile app
 
Aisee kwanza pole sana mkuuu kwa yaliyokukuta...
Wewe kama mzazi sioni kosa la wewe kumpekua binti yako ukizingatia bado mdogo na yuko chini ya himaya yako..mana bila kufanya hivyo usingeyajua haya mapema.
Sasa mi nafikiri kwanza ni kumweleza ukweli tuuu wewe mwenyewe ili aweze jua kwamba ilo swala limekukera(kiboko hakiepukiki ila be smart) na ambainishe muhusika ila hii itawezekana kama ni muoga na hajawa kigagula katika hiyo michezo, ikishindikana msongeshe polisi atamtaja tuu...
Hizi habari kwamba sijui jenga nae urafiki sijui fanya nn huu sio wakati wake mana bond ya mtoto na mzazi hujengwa toka akiwa mdogo..huwezi Sema kwenye miaka 14 eti ndo ujenge bond tena kwenye scenario kama hiyo wakati mwenyewe ameshaandaa majibu kukufix...
Kwenda kwa walimu ni muhimu sana,ila sasa je unaushirikiano kiasi gani na hao walimu..mana kama ni mzazi ambaye haujawahi huzulia hata vikao vya wazazi au haujawahi hata kwenda kuulizia maendeleo ya mwanao unafikiri watakuchukuliaje??labda kama ni shule za binafsi lakini huku kwa Magu tulipo sisi na hasira za huuu usawa...tutaipokea hiyo case na kutupia kapuni mana tunakuaona we sio mshirika mzuri wa mambo ya shule ila shida ndo zimekuleta..so take note ya hilo.
Mwisho trace back malezi ya mwanao kwa kipindi amekaa na mama yake yalikuwaje au mama anatabia gani mana mwisho wa siku Tabia za mtoto wa kike 90 zinategemea na tabia ya mama ikoje...



Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
Noted mkuu.
kwa kuniogopa ananiogopa sana kwa sababu ananijua nikimshika inakuwa issue nyingine ila ktk hili nikisema nimshike nadhani serikali inaweza kunifunga na ndo maana naona nisimuulize nimuache dada yangu labda na mama yake waongee nae.
Ila ushauri wako kwa kiasi kikubwa naukubali
Asante mkuu

Najisikia fahari kuwa MTANZANIA
 
Noted mkuu.
kwa kuniogopa ananiogopa sana kwa sababu ananijua nikimshika inakuwa issue nyingine ila ktk hili nikisema nimshike nadhani serikali inaweza kunifunga na ndo maana naona nisimuulize nimuache dada yangu labda na mama yake waongee nae.
Ila ushauri wako kwa kiasi kikubwa naukubali
Asante mkuu

Najisikia fahari kuwa MTANZANIA
Kikubwa ni kupata ukweli wa hyo kitu basi kama watamuliza na akawa mwepesi kusema hapo sawa ila sasa hawa watoto wa siku hizi akili nyingi sana za ujanja ujanja wa mambo yakijinga lakini darasani shidaaaa...
Aisee nikutakie mafanikio mema kwenye kutafuta ufumbuzi wa hilo tatizo...
Ila usisahau mrejesho mana wazazi tupo wengi humu

Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
 
Ndo ukome.... Na wewe uache peku peku kwenye vitu vya bint yako ukikuta naniii!?
Hizi akili ni sawa na za ostrich, yani ostrich akiona adui akaogopa huficha kichwa chake kwakuwa hamuoni adui ufikiri pia adui hamuoni yeye.
Sasa usipofuatilia watoto hasa mtoto mdogo kama huyo hata miaka 16 bado ukajua madudu na madhaifu yake ukamkanya mapema, akija haribikiwa utamlaumu nani?
Uzungu mwingi na eti privacy ndio tunaharibu familia zetu.
 
Afu hizi smart phones mnawapa watoto ni balaa, mtoto anamaliza form 4 unampa smart phone anakutana na STUNTER kadhaa wa kitaa utafurahi na roho yako, mtoto anatumiwa picha mtu anayonywa k, afu yuko kwenye balehe utafurahi na roho yako
Alafu na vile sisi wakina STUNTER tunavyozipenda sketi za shule... Mbona atafurahi na roho yake...
 
Amekosa Upendo wa baba ameamua atafute sehemu nyingine. Kuwa karibu na binti yako ndugu!

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Shida ya jamii nyingi za kiafrica wanadhani mlezi ni mama tu, hata wewe baba unapaswa kukaa na binti yako na kuongea nae bila aibu wala kificho,
i'm so grateful for my dady since we were young amekua akitueleza mimi na ma bros each and everything bila kificho wala kona kona, lol
na sasa tupo imara (sifa jipe mwenyewe, lol)

Bro ongea na mwanao, usimuogope wala kumuonea aibu, she is your douta, huna haja ya kuput a blame kwa her mom.
#BabaZungumzaNaMwanao#

Sent from my siemens kidole juu using JamiiForum mobile app
 
Back
Top Bottom