Ushauri: Nimepewa RB kwa kosa la kufanya fujo kanisani

Ushauri: Nimepewa RB kwa kosa la kufanya fujo kanisani

Haya makanisa kuna namna huwa sielewi na hapo nachelea kusema shem ni mjinga kiasi hicho wenda hata yeye hajui nini anafanya kwa sasa. kuna bro wetu Mmoja alikuwa mkatolik mzuri kabisaa na misingi yake ya dini ilikuwa thabiti mpaka pale alipoalikwa na rafiki yake kuwa aende kuudhuria kongamano kanisani kwao. Toka hapo yeye na familia vilitengana lasmi hakutaka tena kusikia juu ya familia, Mazaa alikuwa kampambania kazi flani Serikalin na tayar ilikuwa hatua ya mwisho ilikuwa ni yeye tuu kwenda kuripot na kuanza kazi lakin alikataa kabisaa kuwa hataki kazi. Toka 2010 mpaka leo yupo yupo tuu amebaki kuugua magonjwa yasiyo elezeweka kila kukicha
 
Wasaalam?
Ipo hivi juzi asubuhi Jumapili niliingia nyumbani nilikuwa SA kwa mambo ya kikazi, kufika nyumbani nilimkuta binti yangu wa kwanza pamoja na dada wa kazi kumuuliza mama yako yuko wapi? Akasema ameenda kanisani, nikamuuliza mbona hajaenda na watoto(watoto ni mapacha wana miezi 4) wakashindwa kunipa jibu nikapiga kimya nikaenda kupumzika kutokana na uchovu.

Imefika saa 7 mchana nikashtushwa na kelele za watoto walikuwa wanalia mno nahisi walikuwa wanataka kunyonya kuangalia makopo ya maziwa yameisha nikatoa pesa wakaenda kununua lakini nilipiga marufuku matumizi ya maziwa ya kopo.

Nimebuy time mpaka saa 10 jioni kimya mtu hajarudi nikipiga simu inaita tu haipokelewi, nikashikwa na gadhabu sana nikachukua watoto nikawatupia kwenye gari safari mpaka kanisani kwa wife.
Nimefika kanisani nimemkuta wife yupo madhabauni anaombea watu nikachukua watoto nikawaweka pale pale madhabauni nikamwambia awanyonyeshe watoto wana njaa, akagoma akasema nimemfanyia vitendo vya aibu!!

Ghafla mchungaji mkuu akaja akauliza kuna nini? Mimi nikamwambia mchungaji hayakuhusu nataka watoto wanyonye niondoke nao nyie endeleeni na ibada zenu,mchungaji akadakia akasema ibada ya leo inahitaji utulivu ndio maana tulitangaza watoto wote wabaki majumbani.

Nikamvuta kinguvu wife nikaondoka nae nikamwambia Leo ndio mwanzo na mwisho kusali katika makanisa ya kiroho kama hauwezi kusali roman Catholic pumzika nyumbani tu.

Nimepigiwa simu sasa hivi natakiwa kituo cha polisi kwa kosa la kufanya fujo kanisani na kufanya shambulio la kimwili dhidi ya wife, niende au nisiende? Kwa sababu kesho asubuhi inabidi niende Bujumbura kikazi.

Asante
Nenda kaka,na uombe rehema ya Mungu kwa kufanya fujo madhabahuni. Kumbuka madhabahu haichezewi. Hapo alikuwa kanisani,imagine huyo mkeo angekuwa yuko kwenye kikao na mkuu wa nchi ungempelekea watoto hapo? Angekuwa daktari yuko theatere ungempelekea?
Angekuwa amekwama safarini ama amelazwa wodini ungempelekea watoto hapo?
 
Wanawake bhana na dinii sijui huwa kuna shida ganiii...yuko radhi akatoe mil 2 kanisani kesho akuombe hela ya naulii very pathetic...ovyooo sanaa jitahdi kuwaelimisha hasa haya makanisa ya kirohooo ni balaaa tupu
 
Sasa huyo mtumishi wa Mungu ( Mchungaji) Anawafundisha nini wafuasi wake juu ya msamaha?
Maana hapa alitakiwa awaweke sawa mke na mme na maisha ya wanandoa hawa yaendelee vyema.
Sasa yeye analeta mambo ya polisi, kweli aendelee kuaminika kama mtumishi wa Mungu?
 
Wasaalam?
Ipo hivi juzi asubuhi Jumapili niliingia nyumbani nilikuwa SA kwa mambo ya kikazi, kufika nyumbani nilimkuta binti yangu wa kwanza pamoja na dada wa kazi kumuuliza mama yako yuko wapi? Akasema ameenda kanisani, nikamuuliza mbona hajaenda na watoto(watoto ni mapacha wana miezi 4) wakashindwa kunipa jibu nikapiga kimya nikaenda kupumzika kutokana na uchovu.

Imefika saa 7 mchana nikashtushwa na kelele za watoto walikuwa wanalia mno nahisi walikuwa wanataka kunyonya kuangalia makopo ya maziwa yameisha nikatoa pesa wakaenda kununua lakini nilipiga marufuku matumizi ya maziwa ya kopo.

Nimebuy time mpaka saa 10 jioni kimya mtu hajarudi nikipiga simu inaita tu haipokelewi, nikashikwa na gadhabu sana nikachukua watoto nikawatupia kwenye gari safari mpaka kanisani kwa wife.
Nimefika kanisani nimemkuta wife yupo madhabauni anaombea watu nikachukua watoto nikawaweka pale pale madhabauni nikamwambia awanyonyeshe watoto wana njaa, akagoma akasema nimemfanyia vitendo vya aibu!!

Ghafla mchungaji mkuu akaja akauliza kuna nini? Mimi nikamwambia mchungaji hayakuhusu nataka watoto wanyonye niondoke nao nyie endeleeni na ibada zenu,mchungaji akadakia akasema ibada ya leo inahitaji utulivu ndio maana tulitangaza watoto wote wabaki majumbani.

Nikamvuta kinguvu wife nikaondoka nae nikamwambia Leo ndio mwanzo na mwisho kusali katika makanisa ya kiroho kama hauwezi kusali roman Catholic pumzika nyumbani tu.

Nimepigiwa simu sasa hivi natakiwa kituo cha polisi kwa kosa la kufanya fujo kanisani na kufanya shambulio la kimwili dhidi ya wife, niende au nisiende? Kwa sababu kesho asubuhi inabidi niende Bujumbura kikazi.

Asante
La kuenda police kwangu ni dogo kibwa zaidi kapime DNA kama hao mapacha wa kwako au wamtumishi wa buana au kondo wenzie, police neenda aombe kulala cell huyu mke asipo onekana police kukutoa,ujue huna mke hapo.
 
Mme bwege kabisa wewe, yaani ningekuwa ni mimi tayari ningekuwa nimeshabebwa na polisi.

Hapo huna mke, mkeo hana akili hata 1

Nenda polisi haraka waambie una safari mhimu ya kikazi wape chao kama kawaida polisi kuingia ni BURE.

USIPOENDA POLISI WATAKUONA UNADHARAU NA JAMBO LIKAWA KUBWA WAKATI NI DOGO TU

Usiende tena kwenye hilo kanisa la wajinga
 
Kitendo cha wewe kupewa RB ya kuitwa Polisi kwa kufanya shambulio la kimwili kwa wife wako kina maanisha kua Wife wako pia ameridhia wewe kuitwa Polisi/Kushtakiwa,

Hii inanipa tafsiri kua,mkeo anawasikiliza/anawaheshimu zaidi hao watu wa huko Kanisani kuliko wewe coz kabla ya Kanisa kufikia maamuzi ya kukushtaki ni lazima walishauriana na mkeo,

Anza kudeal na mkeo kwanza na solution ni kukazia hapo hapo kua asiende tena huko kwenye hilo Kanisa.
BIASHARA ZA KANISA ZINAANZA KWA KUSHIKA FAHAMU NA AKILI ZA WAUMINI.
KITU PEKEE ANACHO ELEWA NI KILE ANACHO ELEZWA NA MWENYE KANISA!
NINA HAKIKA WALIO OA WANAWAKE WAUMINI WA HIZO KANISA MAGUMU MENGI WANAYAPITIA.
 
Ni tatizo mkuu tena tatizo zaidi lipo kwa ndugu yetu huyu kuchagua mwanamke asie jielewe
Sahihi kabisa,kama Mama ameweza kutelekeza watoto wake wachanga na kuona kuwaombea watu wengine ni bora zaidi kuliko watoto wake,hii ina maanisha kua huyo Mwanamke akili yake na heshima yake na utu wake,vyote amevihamishia huko Kanisani,

Kama amekosa imani/huruma/mapenzi kwa watoto wake wachanga,unafikiri ana mapenzi tena na mumewe?

Hapo cha kufanya ni kukazia tu achague Kanisa au ndoa.
 
Mwache huyo mwanamke chap
Ndoa ya Kikristo ni kifo tu kinatenganisha sio mtu kubadili dini .Mkewe hata angebadili dini kuwa muislamu ndoa ya Kikristo hairuhusu aachwe mke kubadili dini hakumpi Haki ya talaka .Haipo hiyo
 
Just imagine mwanamke yuko kanisani hana hata habari na watoto wake wachanga. I see! Mshauri mkeo amepotea njia.
Alitakiwa aripoti polisi na afungue kesi ya mke kutelekeza watoto alichofanya ni uhuni hakikubaliki kisheria
 
Nenda kaka,na uombe rehema ya Mungu kwa kufanya fujo madhabahuni. Kumbuka madhabahu haichezewi. Hapo alikuwa kanisani,imagine huyo mkeo angekuwa yuko kwenye kikao na mkuu wa nchi ungempelekea watoto hapo? Angekuwa daktari yuko theatere ungempelekea?
Angekuwa amekwama safarini ama amelazwa wodini ungempelekea watoto hapo?
Uko sahihi mwanaume huyo bichwani akili Hana kajaa ujinga mtupu Wacha aende akakutane na polisi kule Kuna dawati la jinsia wanajua Sheria Hadi basi hizo za matatizo ya familia watamnyoosha Hadi akome akitoka hapo atakuwa mtii wa Sheria bila shuruti Kila akitaka kufanya kitu atajiuliza kwanza Sheria za nchi zimekaaje kwenye hili
 
Back
Top Bottom