Ushauri: Nimepewa RB kwa kosa la kufanya fujo kanisani

MREJESHO.
Nimeripoti police nimewekwa selo kwa dakika 30 mama mkwe amekuja ameniwekea dhamana nimetoka.
Cha ajabu muda huu nimerudi nyumbani nimemkuta dada wa kazi tu.. kuuliza naambiwa ameenda kanisani yeye na watoto wote .

Kusikia kwa kenge mpaka damu zimtoke ngoja niende kwanza Bujumbura.
Asante

Humu tuliongea wengine kuwa Polisi lazima wakukomalie na kuwa lazima utawekwa ndani nenda na wadhamini wengine wakakujaza ujinga humu wakabeza Yako wapi ndani umeenda .Polisi wa Sasa wanajua Sheria sio utani

Mke Yuko sahihi kuondoka Kwa usalama wake na wanawe
Kuondoka na watoto ni ushahidi kuwa anajali wanawe angekuwa hajali asingeondoka nao angekuachia

Ngoma bado mbichi kwako kisheria subiri mziki wake mahakamani uko nje Kwa dhamana kesi Iko palepale ni ya kanisa dhidi Yako sio ya mkeo dhidi Yako.Unalo hilo
 
Mke akikuweka ndani unatakiwa kuachana naye only that
Mke hahusiki kwenye hiyo kesi ni kanisa linamshtaki Kwa kufanya fujo kanisani na kumtoa muumini wao Kwa nguvu bila kufuata taratibu za kisheria za ukamataji mtu Kwa kuwa na RB ya polisi na kuiwakilisha Kwa viongozi wa mtaa na mjumbe na kuongozana nao kwenye ukamataji na kuiwakilisha hiyo RB Kwa uongozi wa Kanisa ili waridhie kama Sheria zinavyotaka
 
Humu tuliongea wengine kuwa Polisi lazima wakukomalie na kuwa lazima utawekwa ndani nenda na wadhamini wengine wakakujaza ujinga humu wakabeza Yako wapi ndani umeenda .Polisi wa Sasa wanajua Sheria sio utani

Mke Yuko sahihi kuondoka Kwa usalama wake na wanawe
Kuondoka na watoto ni ushahidi kuwa anajali wanawe angekuwa hajali asingeondoka nao angekuachia

Ngoma bado mbichi kwako kisheria subiri mziki wake mahakamani uko nje Kwa dhamana kesi Iko palepale ni ya kanisa dhidi Yako sio ya mkeo dhidi Yako.Unalo hilo
Kwani mjomba wewe ndio mchungaji? Mbona unaonekana una uchungu sana?
 
Uko sahihi mwanaume huyo bichwani akili Hana kajaa ujinga mtupu Wacha aende akakutane na polisi kule Kuna dawati la jinsia wanajua Sheria Hadi basi hizo za matatizo ya familia watamnyoosha Hadi akome akitoka hapo atakuwa mtii wa Sheria bila shuruti Kila akitaka kufanya kitu atajiuliza kwanza Sheria za nchi zimekaaje kwenye hili
sheria ya nchi watoto wangu wateseke na njaa kwa ajili ya mchungaji? kweli? yeye kawashikiria muda wote huo kwa sheria gani? hivi hizi changamoto mnazijua vizuri jinsi zinavyochelewesha maendeleo kisa wachungaji? hebu acheni hiyo bana hawa jamaa wanazamisha ndoa za watu na kuwafanya wanawake wasiwajibike kwenye familia!
 
Wakati wa Magufuli watu wamechukuliwa kwenye nyumba za ibada, Hapo hata Mimi ningefanya hivyo as long as sijamzuia mchungaji kufanya KAZI yake Mimi nimemchukua Mke wangu, Mke kakiuka haki za watoto.
Mke akikiuuka Haki za watoto nenda Polisi dawati la Haki za jinsia kafungue jalada la kesi watakupa RB na wao ndio watashughulika na hiyo kesi usithubutu kujichukulia Sheria mkononi utakiona Cha mtema Kuni tii Sheria bila shuruti.Zingatia Sheria sio mihemuko ya kidini utaumia
 
Kwani mjomba wewe ndio mchungaji? Mbona unaonekana una uchungu sana?
Nasisitiza uzingatiaji Sheria na kutii Sheria ukizingatia na kutii Sheria huwezi Pata shida popote kama huyo mume Hadi kawekwa ndani Kwa kitu Cha kijinga kabisa Mke katelekeza watoto nenda Polisi kafungue jalada achukuliwe hatua mahakamani kama ikithibitisha ni kweli sio huo ujinga kafanya huyo mwanaume kuvamia mke kanisani na kufanya fujo watu wanasali zao wawe wakristo au waislamu
 
sheria ya nchi watoto wangu wateseke na njaa kwa ajili ya mchungaji? kweli? yeye kawashikiria muda wote huo kwa sheria gani? hivi hizi changamoto mnazijua vizuri jinsi zinavyochelewesha maendeleo kisa wachungaji? hebu acheni hiyo bana hawa jamaa wanazamisha ndoa za watu na kuwafanya wanawake wasiwajibike kwenye familia!
Fungua jalada polisi kuwa mke anatesa watoto ,polisi wapeleke mahakamani tuhuma zikathibitishwe na mahakama na kutoa hukumu usijichukulie Sheria mkononi

Tii Sheria bila shuruti na usipende mambo ya kisheria kujiamulia mwenyewe .Ona Sasa huyo mume Hadi kawekwa rumande katolewa Kwa dhamana Kwa ujinga wake wa kutozingatia sheria
 
Mimi alikuwa anabeba boxer zangu anaenda nazo kanisani akaanza kusali kwa kufoka foka usiku nikamchimba bonge la beat nikamuambia sitaki tena kumuona kwenye makanisa ya kufoka foka na akirudia sitaki tena kuungana nae kwenye hii ndoa
 
Hiyo sababu kwenye ndoa za Kikristo haimo kama sababu ya kuvunja ndoa haimo labda muwe hamkufunga ndoa ya Kikristo na hukuelewa Mafundisho ya ndoa za Kikristo kuwa ndoa huvunjika pale tu mmoja wa wanandoa akifa kuwa ni kifo tu ndicho kitatenganisha sio ohh mke kajiunga kanisa la wanafoka foka kama mwanamziki diamond au mziki wa kizazi kipya inaelekea Mafundisho ya ndoa hukuelewa wewe
 
Mkeo achague kati ya kanisa na ndoa yake. Una vita kubwa sana mbele yako kati ya wewe na mkeo + kanisa. Kuhusu polisi malizana nao kiume. Haya makanisa ya koroho yanavunja ndoa nyingi mno.
 
Mke akiwa kakosea mume afungue jarada polisi na polisi wapeleke kesi mahakamani kesi iamuriwe huko. Haiwezekani kuwa na kangaroo court mume anaibuka tu na kutuhumu kuwa ohh mke kanitelekeza au katelekeza watoto

Ifike mahali utawala wa sheria uzingatiwe Asante Kwa Hilo kanisa lililofungua kesi dhidi ya huyo mume ili mbivu na mbichi zikajulikane mahakamani

Kila kanisa au msikiti ukipata changamoto kama huyo mume kafanya wburuze
 
MREJESHO.
Nimeripoti police nimewekwa selo kwa dakika 30 mama mkwe amekuja ameniwekea dhamana nimetoka.
Cha ajabu muda huu nimerudi nyumbani nimemkuta dada wa kazi tu.. kuuliza naambiwa ameenda kanisani yeye na watoto wote .

Kusikia kwa kenge mpaka damu zimtoke ngoja niende kwanza Bujumbura.
Asante
Kuna kitu cha ziada anakifuata huko Kanisani zaidi ya hiyo ibada,mfukuze aende kwao kisha chukua maamuzi ambayo wewe utaona yanafaa zaidi kwa upande wako.
 
Aende kwao wapi ndoa ni kuoana Kila mtu ana Haki sawa kwenye ndoa ya Kikristo kwao wapi ? Mfano wazazi wote kama walifariki miaka mingi anaenda kwao wapi mjinga wewe?

Hapo ndio kwao aondoke Kwa sababu ipi? Ndoa ya Kikristo inatambua kifo tu ndio kivunja ndoa sio hizo porojo za huyo mumewe
 
Unanishambulia kwa lipi mpaka kuniita mjinga? Unaanzisha ligi ambayo nina uhakika hutaiweza,ngoja nikuangalie tu kwanza.
 
Mke hahusiki kwenye hiyo kesi ni kanisa linamshtaki Kwa kufanya fujo kanisani na kumtoa muumini wao Kwa nguvu bila kufuata taratibu za kisheria za ukamataji mtu Kwa kuwa na RB ya polisi na kuiwakilisha Kwa viongozi wa mtaa na mjumbe na kuongozana nao kwenye ukamataji na kuiwakilisha hiyo RB Kwa uongozi wa Kanisa ili waridhie kama Sheria zinavyotaka
Mwanamke anatakiwa kumlinda mume wake Kwa namna yeyote ile
 
Kanisa ni sehemu ya jumuiya.ya watu huwezi ibuka tu unaenda kamata mtu huko ndani wako kwenye taratibu zao za ibada unaingia tu hujali na kukamata watu na kuburuza nje Kuna taratibu za kisheria za kuzingatiwa
Huyo mwanaume hakuzingatia hakuhitajiki kibali Cha mke kuwa anaridhia au la ataburuzwa Hadi mahakamani hata mke akisema siridhii mume apelekwe mahakamani haihusu mapenzi Yao huko huko Sheria ni Sheria kavunja Sheria atakutana na msumeno wa Sheria mke sio jaji au mahakama
Sawa Sasa wewe mchungaji unaona sawa kwa MwanaMke kuacha watoto wachanga kwenda kushinda kabisa??? Kwanini hukuwa shauri wake na mabinti zao nje muda fulania anatoka kunyonyesha anarudi Tena na Ibada...

Haya Sasa kaondoka Tena na huku nyumbani hajatengeneza hapo Kuna Ibada kweli???????
 
Humu tuliongea wengine kuwa Polisi lazima wakukomalie na kuwa lazima utawekwa ndani nenda na wadhamini wengine wakakujaza ujinga humu wakabeza Yako wapi ndani umeenda .Polisi wa Sasa wanajua Sheria sio utani

Mke Yuko sahihi kuondoka Kwa usalama wake na wanawe
Kuondoka na watoto ni ushahidi kuwa anajali wanawe angekuwa hajali asingeondoka nao angekuachia

Ngoma bado mbichi kwako kisheria subiri mziki wake mahakamani uko nje Kwa dhamana kesi Iko palepale ni ya kanisa dhidi Yako sio ya mkeo dhidi Yako.Unalo hilo
Hamna lolote ,acha kumtia jamaa woga makanisa yenyewe hayana hata vibali vya kufanya hizo kazi ,case kama hii utaishia kulipa faini tuu,Kwa sababu zipi mke wako akubali ufungwe Ili akae peke yake?Hakuna fujo yoyote ulifanya hapo ya kusema ulipiga mtu ,kwanza kisheria mwanamke akibadili dini ya awali ndoa inaweza kufa.
 
Wasaalam?
Ipo hivi juzi asubuhi Jumapili niliingia nyumbani nilikuwa SA kwa mambo ya kikazi, kufika nyumbani nilimkuta binti yangu wa kwanza pamoja na dada wa kazi kumuuliza mama yako yuko wapi? Akasema ameenda kanisani, nikamuuliza mbona hajaenda na watoto(watoto ni mapacha wana miezi 4) wakashindwa kunipa jibu nikapiga kimya nikaenda kupumzika kutokana na uchovu.

Imefika saa 7 mchana nikashtushwa na kelele za watoto walikuwa wanalia mno nahisi walikuwa wanataka kunyonya kuangalia makopo ya maziwa yameisha nikatoa pesa wakaenda kununua lakini nilipiga marufuku matumizi ya maziwa ya kopo.

Nimebuy time mpaka saa 10 jioni kimya mtu hajarudi nikipiga simu inaita tu haipokelewi, nikashikwa na gadhabu sana nikachukua watoto nikawatupia kwenye gari safari mpaka kanisani kwa wife.
Nimefika kanisani nimemkuta wife yupo madhabauni anaombea watu nikachukua watoto nikawaweka pale pale madhabauni nikamwambia awanyonyeshe watoto wana njaa, akagoma akasema nimemfanyia vitendo vya aibu!!

Ghafla mchungaji mkuu akaja akauliza kuna nini? Mimi nikamwambia mchungaji hayakuhusu nataka watoto wanyonye niondoke nao nyie endeleeni na ibada zenu,mchungaji akadakia akasema ibada ya leo inahitaji utulivu ndio maana tulitangaza watoto wote wabaki majumbani.

Nikamvuta kinguvu wife nikaondoka nae nikamwambia Leo ndio mwanzo na mwisho kusali katika makanisa ya kiroho kama hauwezi kusali roman Catholic pumzika nyumbani tu.

Nimepigiwa simu sasa hivi natakiwa kituo cha polisi kwa kosa la kufanya fujo kanisani na kufanya shambulio la kimwili dhidi ya wife, niende au nisiende? Kwa sababu kesho asubuhi inabidi niende Bujumbura kikazi.

Asante

MREJESHO.
Nimeripoti police nimewekwa selo kwa dakika 30 mama mkwe amekuja ameniwekea dhamana nimetoka.
Cha ajabu muda huu nimerudi nyumbani nimemkuta dada wa kazi tu.. kuuliza naambiwa ameenda kanisani yeye na watoto wote .

Kusikia kwa kenge mpaka damu zimtoke ngoja niende kwanza Bujumbura.
Asante
Pole sana aseee! Huyo mwanamke anaivunja ndoa Kwa mikono yake mweneyewe. Pia ninawasiwasi na huyo mchumgaji wenda wakawa na mahusiano.
 
Mke akiwa kakosea mume afungue jarada polisi na polisi wapeleke kesi mahakamani kesi iamuriwe huko. Haiwezekani kuwa na kangaroo court mume anaibuka tu na kutuhumu kuwa ohh mke kanitelekeza au katelekeza watoto

Ifike mahali utawala wa sheria uzingatiwe Asante Kwa Hilo kanisa lililofungua kesi dhidi ya huyo mume ili mbivu na mbichi zikajulikane mahakamani

Kila kanisa au msikiti ukipata changamoto kama huyo mume kafanya wburuze
Nadhani tumsikilize pia ndugu dronedrake tuone kama ana maoni tofauti.
 
Back
Top Bottom