Mimi bhana sio mfuasi wa mada za aina hii lakini wacha tu nikuambia ukweli...
Kabla hujauliza "waliopita chuo hicho", je wewe mwenyewe umefika elimu ya chuo hata kama sio hapo Mkwawa?
Na kama umepata elimu ya chuo, je wadada wa hapo walikuwa na tabia ipi?
Nirudi kwa upande wangu na nitazungumzia darasa langu TU...
Tukiacha sisi wa direct entry, tulikuwa na akina dada watu wazima watatu na wote hawa walikuwa wake za watu
Pale chuo, mmoja alikuwa chakula ya lecturer
Mwingine alikuwa chakula cha mtu mzima mwenzake ambae pia ni mwanafunzi...
Huyu mwingine hakuwa na mtu but taarifa zilikuwa zinasema alikuwa Mwathirika!
So, out of 3, 2 walikuwa na mabwana zao pale ingawaje waliacha ndoa kwao!
Sie wa direct entry sasa...
Kuna Wadada watatu hawa walikuwa hawavutii kabisa... na wote hawakuwa na maboyfriends...
Kuna mmoja ndo alikuwa jeuri na kiburi kuliko wote, including boys... huyu ndo alikuwa Mzigo wa Chige manake huwa napenda sana mademu wajeuri na wakorofi!
Sipendi mambo ya kunyenyekewa mimi...
Wengine waliobaki karibu wote walikuwa na watu wao hapo hapo chuo, na nina uhakika, huko kwao pia waliacha ma-boyfriends! Hata wa kwangu nae alikuwa na boyfriend huko kwao!
That having been said, chuo ilikuwa kila mtu na mtu wake, na tukirudi home, tunaenda kupasha viporo vya makoloni... vile viporo vilivyokuwa vinaishi kwa matumaini kwa kuona kwavile tupo chuo basi nyota njema ipo mbele yetu!
Hakika hapo chuo kama kulikuwa na yeyote ambae hadi kamaliza hakuwa na mtu, basi huyo amesamehewa dhambi zake zote, na moja kwa moja ataenda mbinguni ingawaje wale watatu niliowataja mwanzo hawahusiki na msamaha huu!!
Hao ndo classmates wangu... je, wewe chuoni kwako ilikuwaje? Chukua maelezo yangu, changanya na jibu lako, kisha vuta picha hapo Mkwawa itakuwaje...
All in all, acha wivu bhana...
Mwenzako anajisomea halafu unaanza kumsumbua sumbua usiku, ndo mambo gani hayo?!