Ushauri: Nina mchumba anasoma chuo cha Mkwawa Iringa, napitia magumu sana!

Unashitakiwa kwa kuongea ukweli, fika Kituo cha police kilicho karibu nawe
 
Mkuu
Unadhani hawa wanaokuja kulia lia jukwaani dhidi ya wanawake ni wanaume kamili basi?

Wengi ni mchicha mwiba. Wananitutumua kuonesha wana mahusiano kumbe hasara tupu
Mkuu sio Kila mtu anaweza kukabiliana changamoto zake, tatizo unaloliona wewe dogo Kuna mwenzio limemshinda
 
Pole sana... Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Daah pole sana.
Inaumiza, nasikitika kwamba kila linalozungumzwa ni negative na mie nawaza negative mpaka naogopa kuchangia.

Naomba tu niseme neno moja, moja ya watu wasio na msimamo ni wasukuma. Maisha yao yanaenda kwa mood ya group au watu waliomzunguka. Akizungukwa na watu wabaya atachukua tabia hizo na akizungukwa na wazuri atachukua tabia hizo. Jaribu kujua rafiki zake na waliomzunguka ni watu gani lakini pia fuatulia kujua kwao na familia imekaaje, mie yalishanikuta kwa wasukuma sitakagi wasukuma tena.

Najua sababu ni mke wa kuoa na ushamtolea mahari si kazi kufuatilia hayo na ukipata majibu chukua hatua sahihi kwa busara.

Nawasilisha.
 
HUYO KAOLEWA anaishi na jamaa hapa chuo nje ya geti kuna mtaa mmoja hivi.. huku njia ya MTWIVILA..POLE SANA kwa kusomeaha mchumba .achana nae fanya maamuzi haya magumu
 
Inaelekea mtaalam utakuwa unapiga simu za usumbufu zenye viashiria vya wivu na ufuatiliaji (si unajua wadada huwa hawapendi kuonyeshwa kwamba hawaaminiki) hivyo ameamua liwalo na liwe

Ukiwa na demu mwanachuo na unadhani una future nae. Sio unakuwa mtu wa kupigiana simu tu semister nzima, kuonana mpaka afunge chuo.Wakati mwingine unatenga bajeti ya kuwa una safiri kwenda kumtembelea angalau kuimarisha bond na kuonyesha uwepo wako kwenye maisha yake. Of course haiwezi kufanya asichepuka ila angalau na yeye moyoni anaona una lengo nae!Hata kama atachepuka itakuwa kimachale.

Wewe msikilizie tu mkuu huku kichwani ukiwa na plan B.Wakati mwingine unatakiwa upambanie kombe hata kumtembelea ili kupata uhalali wa kumpiga chini kama analeta mauzauza. Mwisho wa siku asietaka kutafutwa kwa simu wakati mwingine nae hupotezewa!!
 
Aunt abiria simu zinapaswa ziwe kwa kiasi, sio kupiga piga tu simu kama watafuta msaada kituo cha wateja...

Dizaini jamaa itakuwa kafanya kama dozi, hana ishu za kufanya...
Ohoooo….okay
 
Hicho ni kimeo. Yaani kina kata kiu ya hela kwako na penzi lipo kwa mwingine. Msichana anayekupenda wala hawezi kosa muda wa michapo. Tafuta mwingine fasta then achana naye huyu tapeli. Utanishukuru!
 
Darasa moja kuoana ni rare cases. Ila elewa mchumba hasomeshwi buloo.
 
Lazima akukumbuke sana.
 
Kupitia comments zako inaelekea umepigwa sana na vitu vizito kchwani [emoji23] pole sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta Mwanamke mwingine mkuu, acha kua mdhaifu kiasi hicho.

Kama hapokei simu usiku ukipiga kwanini akiwa na shida wewe unapokea?

Toka kwenye hilo ombwe mkuu unatumiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…