USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

Umeishi na mtu kwa miaka 15, mmezaa watoto 4, unakuja kumuacha kisa hakukwambia kua aliwahi kuzaa kabla!!?

Ukisikia kutafutiana sababu ndio huko sasa.
trust me, kwenye watoto 4, possibly kuna mmoja au zaidi siyo wa yule wa mwamba, Imagine mkeo ana mawasiliano ya siri na mzazi mwenzie na mtoto kwa miaka karibu 20...na unaishi nae na kulala nae kitanda kimoja....
 
Kama umenificha miaka 15 yote vipi hao watoto 4 uliozaa na mimi nitaamini vipi kama ni watoto wangu?
Bora mwanume muongo kuliko mwanamke muongo
 
Hapana kwa tukio lako ni tofauti kabisa, huyo mwanamke alikudanganya tena vibaya, kitendo cha kumleta mwanae na kudai ni wa marehemu rafiki yake huo ni uongo mkubwa hata mimi siwezi kuusapoti hata kidogo,

Tukija kwenye tukio hili la mleta mada, Mama hakumwambia kama ana mtoto hadi pale mtoto alipomtafuta mama ake, so Mama alipaswa apewe nafasi kwanza kujua why alificha pili ibaki hivyo kama alivyotaka kuishi
Yani umataka kusema mwanamke unazaa afu hujui kuwa unamtoto au???
 
Mume angemsamehe. Kama amefikiria vizuri. Awaze kwamba sii jambo. Jema kutoa mimba na pia sii jambo jema kuficha jambo, ila kwa. Sababu ya upendo alifanya hivyo. Akiri kosa. Na aombe msamaha.
 
Habari wana JF.

Kuna Ndoa imevunjika hapa ndoa ya miaka 15.

Mke alizaa kabla ya ndoa, sasa mama huyu alimficha mtoto,

Huyu mtoto alikuwa anaishi na Baba yake.

Mume alijua kwa mawasiliano ya simu.

Mama alipokuwa anaongea na mwanae.

Na mtoto anaumri wa miaka 20.

Mume wa ndoa kazaa nae watoto 4.

Dawati la suruhisho walijaribu kuweka sawa ili wasiachana ila ilishindika. Hata wachungaji walishauri kuwa asamee tuu kwani hata mtoto kashakuwa mkubwa hakuna shida yoyote lkn ndo hivyo ndoa imevunjwa jana na mahakama.

Huyu mama alizaa kipindi anaumri wa miaka 21.

Sasa wanajamii hivi vitu vinatokana na nini mpk mmoja anaamua kuficha mtoto?

NI NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUJUA HATA KWA MUME KAMA ALIFICHA KUWA ALIKUWA ANAMTOTO.
Binafsi sijaona Cha kufanya ndoa ivunjike Kuna madhara gani yanatokea baada ya kugundua hakuna..so why kufanya mambo magumu huyo baba alikua anatafuta sababu tu .
 
Mkuu hivi vitu huwa mtu namwambia fuata moyo wako unavyopenda ukiona kaleta mpk hapo officini ujue imemuumiza sana.

Watu wengi wanachukuria kirahisi sana kwa sababu ijatokea kwao.
Umeona ee? Ndo maana tukawa tunampoza tunamwambia alifanya mkiwa hamjaoana. Msamehe muangalie ya sasa.

Ila kiukweli nikiwaza nashindwa kupata majibu. Mwanaume anamwambiaje potezea yalishapita sijui
 
Umeishi na mtu kwa miaka 15, mmezaa watoto 4, unakuja kumuacha kisa hakukwambia kua aliwahi kuzaa kabla!!?

Ukisikia kutafutiana sababu ndio huko sasa.
Unapoficha jambo kama hilo na baadaye kujulika a jua kwamba umevunja trust aliyokuoatia muhusika! Usishangae mkaachana hata kama ndoa ina miaka 50!

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Unapoficha jambo kama hilo na baadaye kujulika a jua kwamba umevunja trust aliyokuoatia muhusika! Usishangae mkaachana hata kama ndoa ina miaka 50!

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Kuna mama mmoja aliachwa ndoa yao ilikuwa na zaidi ya miaka 40 kisa mama alipokea mahari ya mtoto wao bila kumuambia mume wake.
 
Lazima kuwe na sababu ya yeye kutokusema,

Kuna Mama alipokonywa mtoto na Mwanaume aliyezaa nae, mtoto alikua ana miezi 11, yule Mama alihangaika kuanzia Ustawi wa jamii hadi Mahakamani, kote aligonga mwamba basi akamuachia Mungu na kurudi kwao (Mikoa ilikua tofauti) baada ya miaka kupita, akaja akapata Mwanaume akamuoa hakumwambia kuhusu tukio lile yeye anasema alijaribu kulisahau hakuona sababu ya kulizungumzia tena, Mtoto alikuja kumtafuta Mama yake ameshakua mtu mzima na wajukuu akamletea, Mume ndio kujua hilo sakata lakini hakureact tofauti zaidi ya furaha familia imeungana tena.
Kwahiyo huyo mwanaume ndio unamtolea mfano?,hapo umefeli sana
 
Ninyi ni wabinafsi sana ndio maana hamuwezi kuona hili suala kwa jicho la tatu, umeishi na mtu miaka 15 na ameshazaa watoto wanne unamuacha akaanze maisha ya usingle, mna watoto wanne tayari watoto waanze kulelewa bila wazazi wote wawili mlishawaza jinsi gani mnawaathiri kisaikolojia? je mahusiano ya mama na mtoto aliyemficha kwa miaka 20 yatakuaje? hamuoni kuna chuki itazalika kua ujio wake ndio umemfanya ameikosa ndoa yake?

Kosa lenyewe la kijinga kabisa.
Wewe una vituko utadhani mtoto,sasa kama saikolojia ya Baba kama haipo sawa hao watoto watalelewaje??.Kuoana kwa miaka 10,20 au 40 sio tatizo issue kubwa ni uaminifu.Mahusiano is all about trust huwezi kuishi ndani na mtu usiye mwamini-hata kama ndoa mna miaka 60 ukagundua mwezi wako alikudanganya jambo kubwa you call it off.

Huyo jamaa angekuwa tahira wa mwaka kama angeendelea kuishi na huyo Mwanamke.
 
Kweli kabisa mkuu.anaongea simple tu je kuhusu kumwamin kutakuwepo tena?
Wewe una vituko utadhani mtoto,sasa kama saikolojia ya Baba kama haipo sawa hao watoto watalelewaje??.Kuoana kwa miaka 10,20 au 40 sio tatizo issue kubwa ni uaminifu.Mahusiano is all about trust huwezi kuishi ndani na mtu usiye mwamini-hata kama ndoa mna miaka 60 ukagundua mwezi wako alikudanganya jambo kubwa you call it off.

Huyo jamaa angekuwa tahira wa mwaka kama angeendelea kuishi na huyo Mwanamke.
 
Ila wanaume huwa mnanishangaza jambo moja. Nyinyi mnazaa na michepuko yenu ilhali mpo kwenye ndoa, wake zenu wanakuja kujua mkishakufa. Mbona hawa vimbi mashavu kama mnavyovimba nyinyi??? Wengine mnawaletea kabisa nyumbani, na wanawapokea maisha yanaenda. Sasa huyu wa zamani kabla ya ndoa mnaumia nini. Wanafki nyinyi muwe mnatunza energy mnayoyafanya yakirudi kwenu mvumilie
Sisi ni wanaume na nyinyi ni wanawake FULL STOP,
 
Kama tulivyo kubaliana kwenye kikao cha mwisho kwamba wazazi hawaachani[emoji4]
 
Back
Top Bottom