USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

Wanadhani Ndoa ni kama hizo betting zao,
Mijinga ya mwisho.
Madam mimi sijui hii issue umeichukuriaje.
Jaribu kuvaa viatu kwanza wewe.
Mimi kiendelea nae wale.
Siwezi huo ndomwisho .

Issue kama hii sijajua hat dawati la suruhisho walijaribu kusolve vipi.
 
Hata wanaume wapo wanaficha.
 
Wapo wanaume wengi tuu wanaficha watoto.
 
Mleta mada hiki kisa ni pasua kichwa sana, kuachana ni process, kuachana kuna dalili, kuishi ndoa kuna makwazo na makosa mbalimbali, kuishi ndoa kuna viashiria vya uaminifu na kukosa uaminifu, wapo baadhi ya wanandoa huambiwa umbea na kuupuza, wapo wanandoa hupeana limbwata, wapo baadhi waume hauno dalili mbaya za kubambikiwa watoto, Mahakama zina Baraza la ushauri kabla ya hukumu, kuna pia Baraza la kata, ustawi wa jamii, nafikiri na nawaza hakuna ndoa isiyo na mapito ya makwazo, yumkini hii ndoa imehitishwa kwa kuna dots nyingi sana zimeshabihiana.

Baada ya kupata maarifa kidogo kwenye maisha nimeamini binadamu hutengenezwa na elimu na maarifa mbalimbali ikiwemo waalimu mbalimbali mfano katika Mila, dini, wazazi, Babu, bibi, elimu Dunia. Maturity, wisdom, ability to contain and absorb and dilute life shocks.

Naelewa mtazamo tofauti na akili tofauti na pia ni haki kukubali kutokukubaliana, na kulinda haki na fikra za mwingine mwenye tofauti na mimi, pia ipo haja ya kujenga hoja ya kimantikk kwa tusiokubaliana.

Asante sana nimepitia kila comment nimejifunza mengi sana. πŸ™πŸ™πŸ™

Ndugu mleta mada kati ya mke na .mme yupi ni mhasibu ambae na office mate wako?

Kwenye maisha referee habebi dhamana ya wachezaji hivyo si kila jambo linahitani deep thinking, peripheral issues zisikukoseshe afya ya akili.

Madam Dream Queen, Maranatha, Macho_ na wengine wote, kama Mungu alituumba tofauti japo kwa mfano wake, na yeye ni God of variety si ni nani tusiwe na fursa ya kuwa na mtazamo tofauti na afya ya mahusiano bado ikawa njema?

"Emotional intelligence draws the line of separation"

πŸ™πŸ™πŸ™

Wadiz
 
....mimi niligundua tu ana namba ya simu ya siri ambayo anaitumia nikapiga chini, sembuse toto tena la miaka 20 kabisa. Mke kama huyo anakuwa anakuia timing tu kwa hiyo napiga chini, Naanza upya, hakuna nilipochelewa wala ninapowahi.
 
N
Nahic iyo ndo sababu alikuwa anahc ataolewa.
 
Sababu lazima anayo, hayo ni mambo yanayoongeleka na sio kuvunja ndoa, angemfumania hapo sawa ila sio hilo ni dogo sana kikubwa ni kumpa nafasi atoe sababu zake.
sababu mdada....hujui maumivu ya kulishwa iliyoliwa kwa ushahidi kwa miaka 15 bila kujua.
 
Glenn Unaweza kakuta anamtetea huyo dada cos na yeye amewahi kufanya huo mchezo si unajua wanawake akili zao zinafanana
 
Oa kwenye Koo ambayo babu wa babu wa mtu wako anajulikana. Kuoa sio unakutana naa mtu town akapendeza hujui vizuri Koo yake, kisa akapendeza,kavutia machoni,akasoma,anafanya kazi nzuri panono,ana biashara kubwa za uhakika,hisia zinazidi akili unaoa/unaolewa nay. Inabidi umjue mtu nje ndani Koo yake ambaye unaunda naye familia,Kuna watu Koo zao Zina makandokando.
Sema Sasa sijui siku hizi vijana wanaenda na ukisasa ,usomi eti wameelimika wanachukua mtu kisa akavutia machoni.machoni ukificha mavi ndani yaa paja la kuku litavutiwa na utaanza kulila Ila utakula na mavi ndani yake.
Yaani mke wa Kuja kuingiza dna kwa Koo yangu why nisimjue nje ndani yaani mpaka Koo yake ,
 
Umeishi na mtu kwa miaka 15, mmezaa watoto 4, unakuja kumuacha kisa hakukwambia kua aliwahi kuzaa kabla!!?

Ukisikia kutafutiana sababu ndio huko sasa.
Unaachwa tu maana siyo mwaminifu na msema kweli........
 
Jamaa aliowa kwa mbwembwe kweli si unajua ile umeyapatia, kidigrii kichwani, shirika kubwa linamlipa vizuri. Akajenga mjengo wa kisasa akaowa bwana binti mrembo. Ndani ya mwaka jamaa kagundua dada alikuwa na mtoto yupo huko kwao kijijini. Eeeenh mbona kiliwaka si kitoto. Bwana akahama nyumbani akaenda kukaa huko kwa miezi kadhaa lakini yaliisha na kuishi pqmoja. Kilichokuwa kinamuuma yule bwana ofisi nzima mashauzi nimeowa,nina mke, hii kanipa wife, si unajua siku hizi nina mwenzangu, majogambo yalikuwa mengi na wenzake wakapata cha kumchapia alijuata.
 
Huyo mume kuna uwezekana mkubwa alikuwa ameishamchoka huyo mke; alikuwa anatafuta sababu tu na hiyo sababu tayari imeishapatikana. Anyway, ndoa ni maua. Cha muhimu baba awatunze watoto na kama walifanikiwa kujenga nyumba na kumiliki mali nyingine, basi hizo mali zimilikishwe watoto kwa usimamizi wa mama yao. Mume aondoke hapo akatafute chaka lingine aendeshe maisha yake mapya, isiwe shida.
 
Ningemsikiliza sababu yake lazima iwe na mashiko na kuendelea na Maisha, nisingeivunja ndoa
Unajua mwanamke aliyezaa na mwanaume mwingine, kumbuka yule ni mzazi mwenzake unajua kile kilichokuwa kinaendelea? Kosa lingine anaweza kusameheka ila siyo udanganyifu
 
Glenn Unaweza kakuta anamtetea huyo dada cos na yeye amewahi kufanya huo mchezo si unajua wanawake akili zao zinafanana
Inawezekana nikawa namtetea huyo dada kumbe hata mama ako mzazi aliwahi kufanya hayo.... maana hata mama ako ni mwanamke.
 
Wengi hawasemi ukweli.

Tatizo ikijulikana ambapo na ni lazima ijulikane tuu.

Mume anaona kama walikuwa wanaume wawili kwa mwanamke mmoja.

Better to be open karma kusuka au kunyoa ijulikane mapema
Wewe umemjulisha mwenzako au bado hujafanya maamuzi? πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Kama alificha hilo anaweza kuwa kama huyu; mwamba watoto 6 kumbe moja tu ndio wake
 

Ubinafsi na Unafki wa Wabongo unajionesha katika nyuzi hizi mbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…