USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

Wanadhani Ndoa ni kama hizo betting zao,
Mijinga ya mwisho.
Madam mimi sijui hii issue umeichukuriaje.
Jaribu kuvaa viatu kwanza wewe.
Mimi kiendelea nae wale.
Siwezi huo ndomwisho .

Issue kama hii sijajua hat dawati la suruhisho walijaribu kusolve vipi.
 
Mwanamke / mwanaume kama ulishawahi kupata mtoto wa ujanani hakikisha unaweka wazi mambo yako pindi unapoingia kwenye mahusiano mapya. Hili suala la kuficha ficha linawaumbua wengi hususani wanawake hawapendi kuweka mambo yao wazi.

Weka wazi me/ke ajue ukweli na aamue lipi lililo bora kwake aendelee na wewe au muachane mapema.

Mwisho ukikitana na me/ke aliwahi kupata mtoto kabla ya ndoa na hakuwahi kukwambia, jua hao wazazj bado wana mahusiano kwa kigezo cha mzazi mwenza.

Epuka matapeli mwanamke aliyezalishwa na mwanaume wake yupo hai hafai.
Hata wanaume wapo wanaficha.
 
Hongera Mwanaume imara umeandika point kubwa sana, Wanawake wa Kiafrica wameshikiwa akili na the so called Mila na Desturi, mfumo dume umewaharibu kiasi cha kutoitambua hata thamani yao,

Kosa hilo hilo angefanya Mwanaume na Mwanamke akataka kuachika wangemwambia avumilie tu alee watoto ndio ishatokea,

Ujinga ujinga tu.
Wapo wanaume wengi tuu wanaficha watoto.
 
Mleta mada hiki kisa ni pasua kichwa sana, kuachana ni process, kuachana kuna dalili, kuishi ndoa kuna makwazo na makosa mbalimbali, kuishi ndoa kuna viashiria vya uaminifu na kukosa uaminifu, wapo baadhi ya wanandoa huambiwa umbea na kuupuza, wapo wanandoa hupeana limbwata, wapo baadhi waume hauno dalili mbaya za kubambikiwa watoto, Mahakama zina Baraza la ushauri kabla ya hukumu, kuna pia Baraza la kata, ustawi wa jamii, nafikiri na nawaza hakuna ndoa isiyo na mapito ya makwazo, yumkini hii ndoa imehitishwa kwa kuna dots nyingi sana zimeshabihiana.

Baada ya kupata maarifa kidogo kwenye maisha nimeamini binadamu hutengenezwa na elimu na maarifa mbalimbali ikiwemo waalimu mbalimbali mfano katika Mila, dini, wazazi, Babu, bibi, elimu Dunia. Maturity, wisdom, ability to contain and absorb and dilute life shocks.

Naelewa mtazamo tofauti na akili tofauti na pia ni haki kukubali kutokukubaliana, na kulinda haki na fikra za mwingine mwenye tofauti na mimi, pia ipo haja ya kujenga hoja ya kimantikk kwa tusiokubaliana.

Asante sana nimepitia kila comment nimejifunza mengi sana. 🙏🙏🙏

Ndugu mleta mada kati ya mke na .mme yupi ni mhasibu ambae na office mate wako?

Kwenye maisha referee habebi dhamana ya wachezaji hivyo si kila jambo linahitani deep thinking, peripheral issues zisikukoseshe afya ya akili.

Madam Dream Queen, Maranatha, Macho_ na wengine wote, kama Mungu alituumba tofauti japo kwa mfano wake, na yeye ni God of variety si ni nani tusiwe na fursa ya kuwa na mtazamo tofauti na afya ya mahusiano bado ikawa njema?

"Emotional intelligence draws the line of separation"

🙏🙏🙏

Wadiz
 
....mimi niligundua tu ana namba ya simu ya siri ambayo anaitumia nikapiga chini, sembuse toto tena la miaka 20 kabisa. Mke kama huyo anakuwa anakuia timing tu kwa hiyo napiga chini, Naanza upya, hakuna nilipochelewa wala ninapowahi.
 
N
Katika vitu vya kuzingatia kwenye mahusiano kabla ya kuingia kwenye ndoa ni ukweli na uwazi hasa hasa wa vitu ambavyo ni muhimu kama kuwa na mtoto. Ni bora kumwambia mwenza wako ukweli ili yeye aamue kukubali kuendelea au lah.

Mwenzetu alikosea sana miaka 15 kumficha mume wake sio busara kabisa kinachoumiza sio kuzaa kabla ila ni kumficha mwenzie. Ila inawezekana kuna sababu kubwa nyuma yake au alijua akisema ana mtoto hataolewa maana wanaume wanawadharau sana single mothers na inapelekea situations kama hizi.
Nahic iyo ndo sababu alikuwa anahc ataolewa.
 
Sababu lazima anayo, hayo ni mambo yanayoongeleka na sio kuvunja ndoa, angemfumania hapo sawa ila sio hilo ni dogo sana kikubwa ni kumpa nafasi atoe sababu zake.
sababu mdada....hujui maumivu ya kulishwa iliyoliwa kwa ushahidi kwa miaka 15 bila kujua.
 
Umeanza mihemko isiyo na sababu.
Pili tusijadili mambo kimazoea ya kiswahili.

Mwanzo wa mahusiano una mambo mengi.

Kuna mwanamke mkianza mahusiano anakutaka uwe wazi kwake kama umewahi kuoa au kuzaa nje.

Kwa moyo mkunjufu unamweleza ukweli.

Naye anakwambia hajawahi kuolewa wala kuzaa, baada ya miska 15 ukagundua alizaa na alikuficha kwanini udimwache?

Mwanzoni ukiniambia hata una watoto wawili kwa uwazi huo mimi nitakuoa.

Napendezwa na mwanamke muwazi, makosa kila mtu hufanya.

Lakini kitendo cha kumficha binadamu aliyetoka kiunoni mwako, si unaweza kumficha mmeo jambo lingine kubwa?
Ongea uhalisia uache hasira
Glenn Unaweza kakuta anamtetea huyo dada cos na yeye amewahi kufanya huo mchezo si unajua wanawake akili zao zinafanana
 
Ndani ya hizi ndoa wengi tunaowaita mashemeji mara nyingi huwa ni watoto wa wake zetu.

Unakuta katoto unatambulishwa kama mdogo wa mwisho au mtoto wa dada/kaka kumbe ni mtoto wa mkeo.

Ni nadra kwa wanaume kuficha watoto waliopatikana kabla ya mahusiano ila wanawake mara nyingi wanahusisha kuwa na mtoto kabla na kushuka kwao kwa thamani kupelekea kuficha watoto wao wa kabla ya ndoa/mahusiano.
Oa kwenye Koo ambayo babu wa babu wa mtu wako anajulikana. Kuoa sio unakutana naa mtu town akapendeza hujui vizuri Koo yake, kisa akapendeza,kavutia machoni,akasoma,anafanya kazi nzuri panono,ana biashara kubwa za uhakika,hisia zinazidi akili unaoa/unaolewa nay. Inabidi umjue mtu nje ndani Koo yake ambaye unaunda naye familia,Kuna watu Koo zao Zina makandokando.
Sema Sasa sijui siku hizi vijana wanaenda na ukisasa ,usomi eti wameelimika wanachukua mtu kisa akavutia machoni.machoni ukificha mavi ndani yaa paja la kuku litavutiwa na utaanza kulila Ila utakula na mavi ndani yake.
Yaani mke wa Kuja kuingiza dna kwa Koo yangu why nisimjue nje ndani yaani mpaka Koo yake ,
 
Umeishi na mtu kwa miaka 15, mmezaa watoto 4, unakuja kumuacha kisa hakukwambia kua aliwahi kuzaa kabla!!?

Ukisikia kutafutiana sababu ndio huko sasa.
Unaachwa tu maana siyo mwaminifu na msema kweli........
 
Jamaa aliowa kwa mbwembwe kweli si unajua ile umeyapatia, kidigrii kichwani, shirika kubwa linamlipa vizuri. Akajenga mjengo wa kisasa akaowa bwana binti mrembo. Ndani ya mwaka jamaa kagundua dada alikuwa na mtoto yupo huko kwao kijijini. Eeeenh mbona kiliwaka si kitoto. Bwana akahama nyumbani akaenda kukaa huko kwa miezi kadhaa lakini yaliisha na kuishi pqmoja. Kilichokuwa kinamuuma yule bwana ofisi nzima mashauzi nimeowa,nina mke, hii kanipa wife, si unajua siku hizi nina mwenzangu, majogambo yalikuwa mengi na wenzake wakapata cha kumchapia alijuata.
 
Habari wana JF.

Kuna Ndoa imevunjika hapa ndoa ya miaka 15.

Mke alizaa kabla ya ndoa, sasa mama huyu alimficha mtoto,

Huyu mtoto alikuwa anaishi na Baba yake.

Mume alijua kwa mawasiliano ya simu Mama alipokuwa anaongea na mwanae.

Na mtoto ana umri wa miaka 20.

Mume wa ndoa kazaa naye watoto 4.

Dawati la suluhisho walijaribu kuweka sawa ili wasiachane ila ilishindika. Hata wachungaji walishauri kuwa asamehe tuu kwani hata mtoto kashakuwa mkubwa hakuna shida yoyote lkn ndo hivyo ndoa imevunjwa jana na mahakama.

Huyu mama alizaa kipindi ana umri wa miaka 21.

Sasa wanajamii hivi vitu vinatokana na nini mpk mmoja anaamua kuficha mtoto?

NI NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUJUA HATA KWA MUME KAMA ALIFICHA KUWA ALIKUWA ANAMTOTO.
Huyo mume kuna uwezekana mkubwa alikuwa ameishamchoka huyo mke; alikuwa anatafuta sababu tu na hiyo sababu tayari imeishapatikana. Anyway, ndoa ni maua. Cha muhimu baba awatunze watoto na kama walifanikiwa kujenga nyumba na kumiliki mali nyingine, basi hizo mali zimilikishwe watoto kwa usimamizi wa mama yao. Mume aondoke hapo akatafute chaka lingine aendeshe maisha yake mapya, isiwe shida.
 
Ningemsikiliza sababu yake lazima iwe na mashiko na kuendelea na Maisha, nisingeivunja ndoa
Unajua mwanamke aliyezaa na mwanaume mwingine, kumbuka yule ni mzazi mwenzake unajua kile kilichokuwa kinaendelea? Kosa lingine anaweza kusameheka ila siyo udanganyifu
 
Glenn Unaweza kakuta anamtetea huyo dada cos na yeye amewahi kufanya huo mchezo si unajua wanawake akili zao zinafanana
Inawezekana nikawa namtetea huyo dada kumbe hata mama ako mzazi aliwahi kufanya hayo.... maana hata mama ako ni mwanamke.
 
Wengi hawasemi ukweli.

Tatizo ikijulikana ambapo na ni lazima ijulikane tuu.

Mume anaona kama walikuwa wanaume wawili kwa mwanamke mmoja.

Better to be open karma kusuka au kunyoa ijulikane mapema
Wewe umemjulisha mwenzako au bado hujafanya maamuzi? 😀 😀 😀 😀
 
Kama alificha hilo anaweza kuwa kama huyu; mwamba watoto 6 kumbe moja tu ndio wake
1696569067905.png
 

Ubinafsi na Unafki wa Wabongo unajionesha katika nyuzi hizi mbili
 
Back
Top Bottom