USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

Umeishi na mtu kwa miaka 15, mmezaa watoto 4, unakuja kumuacha kisa hakukwambia kua aliwahi kuzaa kabla!!?

Ukisikia kutafutiana sababu ndio huko sasa.
Alikuwa anapasha kiporo huyooo...

Hata mie ningemuacha.
Ongea ukweli wakati wa Uchumba.
 
Alafu kuna kisa kimoja kimemtokea mwenzetu wa ofisini kimenishangaza kwa alivyo react ila nikasema acha nije nishirikishe na wanajamvi huku.

Huyu dada kakaa kwenye ndoa kama miaka mitatu hivi. Sasa anakuja kugundua mume wake aliwahi kuchepuka na ex wake tena sio mara moja kipindi wapo kwenye mahusiano. Yaani kabla ya ndoa. Yani wame date miaka saba, mwaka wa nne mwanaume akawa na mahusiano na ex wake wameenda kama miaka miwili na ex malavidavi kama yote ila huyu dada anasema hakuwahi kuhisi. Sasa mke mtu kaja kujua wakati wameshaoana. Anasema ye bado kinamuuma kwasababu alimuamini sana mme wake inakuwaje alimsaliti kipindi ambacho alimpenda na kumuamini.

Wengi tukamshauri aache yaliyopita wagange yajayo. Akauliza ingekua nyinyi mngesahau na kusamehe? Nikasema wanajamvi mpo kibao mna majibu em mshaurini na nyinyi.
Aliambiwa na nani!? Alijuaje!??
 
Basi nilidhani una akili kumbe wale wale, unasemaje watoto waliolala tumbo moja na kunyonya ziwa moja sio ndugu kisa baba zao tofauti?

Hebu usinichoshe mie kama unatafuta comments nyingi ushazipata
Wewe dada nimefuatilia posts zako una vitu hivi;

1. Una tabia ya faizafoxy
2. Una kisani sana utakuwa singo maza wewe.
3. Utakuwa akina mwajuma ndala ndefu wacheza vigodoro
 
Kwa maelezo ya mtoa mada ni kua, mwanamke aliolewa akiwa ana miaka 21, na sasa mtoto ana miaka 20, hatujui sababu ya yeye kutengana na mtoto wake na hatujui sababu ya yeye kutokumwambia mumewe kua ana mtoto, mtoto alikua analelewa na baba ake, what if alinyang'anywa mtoto akaamua kuanza upya na huyo mume wake? Kwanini umuite muhuni kisa tu hakukwambia kuhusu mtoto,

Kwanini uumie sana hadi utoe talaka, alikuomba matumizi ya mtoto? Kama miaka yote mlikua vizuri hilo tu ndio umuache? hapo ni wazi ulikua unamtafutia sababu hakuna kingine unless kuwe na jambo lingine mleta mada halijui.
Sababu ya talaka ni mwanamke kuficha jambo kubwa kiasi hiki.

Mwanamke au mwanaume kuficha jambo la mtoto hiyo ndoa ni batili.

Sio tu mwanamke kuficha hata mwanaume akificha anastahili hiyo adhabu ya kuachwa.

Mapenzi yamejengwa juu ya msingi UAMINIFU TU.

Uaminifu ukikosekana hakuna mapenzi tena..mapenzi yakikosekana ndoa inakufa.

Inaonyesha wewe ni kipanga, sio muaminifu ndio maana umekomaa kuandika mataputapu hapa we mkwere
 
Back
Top Bottom