Dream Queen
JF-Expert Member
- Nov 4, 2015
- 8,263
- 18,201
Upo sahihi kabisa, kosa hilo Wanawake wengi hulifanyaa kwa hofu ya kuachwa au kughairishwa kwa ndoa japo kwa upande mwingine wengine wanakua na sababu tofauti kabisa, kuna story niliiweka mwanzoni mwanzoni kabisa ya mama aliyenyang'anywa mtoto wa miezi 11, akaamua kufuta hiyo memory mbaya kwake na kuanza family upya hadi mtoto alipokuja kumtafuta mama ake akiwa na yeye ana watoto tayari, mumewe alielezwa sababu na akaelewa maisha yakaendelea,Kwanini alificha. Jibu naweza kubuni japo sisemi kuwa niko correct. Alificha kwa sababu wanaume wengi hughairi kuoa wanawake wenye mtoto/watoto. Hili ni kosa ambalo wanawake wengi hulifanya. Ni bora useme ukweli kuliko kuficha. Ukificha hawa kama bwana hata-mind sana lakini maisha hayatakuwa kama yalivyokuwa asilan. Utajengeka ukuta mkubwa sana wa kukosa uaminifu kati yenu. Hata kwenye issue yangu alijitetea kuwa alificha kwa sababu aliona akisema ukweli kuwa ana watoto wawili ningeachana naye.
Hoja yangu ni haya mambo yaangaliwe pande zote ili suluhisho lipatikane na sio kuangalia upande mmoja na lawama kama zote.