USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

Lakini sio kosa la kumuacha Mke, kama mmeishi miaka zaidi ya 18 pamoja ndiyo mje kuachana Uzeeni?

Tumeambiwa tusamehe 7x70

Huyo jamaa walikua wameshachokana, amepata sababu tu ya kumwachia mkewe.

Kingine, angejipa muda wa kutulia na kutafakari, kama amefanya haya maamuzi haraka akiwa na hasira inaweza kuja kimgharimu mbele ya safari na kubadili mambo itakua mchakato mrefu.

Kingine unawezakuta huyo Mama alificha haya mambo akijua analinda ndoa yake matokeo yake mambo yameenda kinyume, inatokea kwenye maisha unawezafanya jambo Kwa Nia nzuri likapokelewa tofauti au matokeo yakawa sio yaliyotarajiwa.

Mwisho, hapa tumepata habari Kwa juu juu tu, Kuna mengi hayajasemwa, inakua ngumu kutoa maamuzi au ushauri Kwa hizi taarifa zilizoletwa. Mfano, huyu Mama alikua anahusikaje na matunzo ya huyo mtoto? Kulikua na mahusiano au mawasiliano ya aina Gani kati ya hao wazazi?

Ukute jamaa aliwahi kuulizia akaambiwa hakuna kitu kama hicho, Sasa akija kubaini lazima awe kifaru.
 
Na wanaume ndio visababishi vikubwa vya situations kama hizi. Kwanza ndio wanaozalisha na kutelekeza wanawake halafu wanakuwa wa kwanza kuwaponda na kutukana wanawake waliozaa hadi kufikia hatua ya kujiona sio chochote na hana thamani. Inauma sana kuificha damu yako ila judgement ya jamii inafanya watu wafanye mambo wasiyoyapenda.
@trudie mama kipenzi.
Bila shaka nawe ni muhanga wa hii situation, kuzaa na mtu na akasepa;

Nisikilize kwa makini.
1. Kukimbiana hutokana na kuzaa na mtu ambaye hamkuwa na malengo, mara nyingi ni ushikaji hatimaye mtoto....kosa ni lenu, unapaswa ubane mapaja hadi uchumbiwe na uolewe ksma hutaki hii kadhia

2. Kudate na wavulana au waume za watu, mnaingia kichwa kichwa nyie tena wengi kwa tamaa za kijinga tu.

3. Ni ukorofi wenu, mkishapewa mimba huanzi vitimwi kwanini msiachwe, mwanaume hapendi mwanamke korofi kama Dream Queen au faizafoxy

4. Kudate na wanaume wahuni, unategemea nini?

Narudia, kama hutaki aibu, bana mapaja hadi uolewe.

Wanaume tunapenda sana kuoa wanawake wagumu kutoa UCHI, hii ni siri.

Kama utanipa mzigo kirahisi, napata hisia kuwa wewe malaya, napiga nasonga mbele kama injili....tulizeni vidude vyenu.

LAKINI IKITOKEA UMEZAA...JIKUBALI...UKIPATA MUOAJI MWAMBIE UKWELI, USIOGOPE KUACHWA, KUNA MTU ATAKUPENDA NA MWANAO.

Pili utaepuka kuachika baadae mmeo skiujua ukweli.
 
Kuna watu hawawezi kuupokea uongo, yupo tyr apewe ukweli wa namna yoyote ile.....ww unahakika kama hawakuulizana hayo mambo, na vp kama alisema hajawahi kuzaa? Hii nakumaind ww na ukoo wako af mazoea yanakufa
Kua kwanza, ujue umuhimu wa familia na uchungu wa watoto ndio uje ucomment kwenye hii mada.
 
Hapo ngumu kumeza, kwamba huyo baba ataenda kuoa mwanamke mwingine na yeye amdanganye kwamba sijawahi kuzaa kumbe Ana watoto wanne
Anaweza kuoa hata hapo mtaani tu.
Unajua ukimwacha mke au mume kuna mtu hapo nje anamsubiri amdake.

Kila mtu huwa anatamani asicho nacho.
Huyo anaoa tena kwa harusi na wanwe wa 4
 
Umeishi na mtu kwa miaka 15, mmezaa watoto 4, unakuja kumuacha kisa hakukwambia kua aliwahi kuzaa kabla!!?

Ukisikia kutafutiana sababu ndio huko sasa.
Sio kutafutiana sababu kusema ukweli ni jambo la msingi kwenye relationship, kwanini alimficha hizo siku zote ? Huon kama kuna kitu hapo ?
 
Kama ni over 50, kutelekeza watoto na kuanza upya pagumu sana , pressure sukari itakuwa nyumbani kwake!! Kuendesha Gari jipya ataweza!?
Labda kama Hana kipato Wala uwekezaji na sio lazima aoe
 
Umeishi na mtu kwa miaka 15, mmezaa watoto 4, unakuja kumuacha kisa hakukwambia kua aliwahi kuzaa kabla!!?

Ukisikia kutafutiana sababu ndio huko sasa.
Kwanini amfiche mtoto? Hicho ni kiashiria kuwa alikuwa bado anaendelea na mzazi mwenza wa awali. Hata mimi ningevunja ndoa au shingo la mtu.
 
Hapo Mume amewaza kama amefichwa suala la Mtoto kwa miaka yote hiyo, na kulikuwa na mawasiliano ya siri Baina ya Mkewe, Baba Mtoto pamoja Mtoto mwenyewe, basi kuna uwezekano mkubwa kuna vingine vingi vya siri vilikuwa vinaendelea baina ya Mkewe na huyo Baba wa Mtoto.. Na hapo ndipo panampa ugumu kusamehe..
NAKAZIA
 
Habari wana JF.

Kuna Ndoa imevunjika hapa ndoa ya miaka 15.

Mke alizaa kabla ya ndoa, sasa mama huyu alimficha mtoto,

Huyu mtoto alikuwa anaishi na Baba yake.

Mume alijua kwa mawasiliano ya simu Mama alipokuwa anaongea na mwanae.

Na mtoto ana umri wa miaka 20.

Mume wa ndoa kazaa naye watoto 4.

Dawati la suluhisho walijaribu kuweka sawa ili wasiachane ila ilishindika. Hata wachungaji walishauri kuwa asamehe tuu kwani hata mtoto kashakuwa mkubwa hakuna shida yoyote lkn ndo hivyo ndoa imevunjwa jana na mahakama.

Huyu mama alizaa kipindi ana umri wa miaka 21.

Sasa wanajamii hivi vitu vinatokana na nini mpk mmoja anaamua kuficha mtoto?

NI NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUJUA HATA KWA MUME KAMA ALIFICHA KUWA ALIKUWA ANAMTOTO.
Aiseh huyo mama ni mpuuzi sana
 
Unaona ni kosa dogo?
Kosa sio tu kuzaa, kosa kubwa ni uwazi.

Hili jambo hufufua mambo mengi.

Huenda kuna nyakati alikuwa akiomba ruhusa asafiri aende mahali akidanganya kwa ndg....jamaa anakuja kuunga dots anagundua huenda alikuwa anaenda onana na mume wa awali.

Jambo moja hufufua mengi uliyoyasamehe....waza vizuri usikomenti kirahisi kama hujui umuhimu la hili
yaani lazima lazima alikuwa akikutana na Baba mtoto! haiwezekani mama amsahau mtoto wake daima aliyemweka kwenye tumbo lake miezi tisa.

naamini mpaka ndoa jamaaa ameamua kuivunja kuna vitu vingi sana vimepelekea ndoa hiyo kuvunjika.

uongo haudumu.

unaweza kudanganya lakini huwezi kudanganya wakati wote.
 
Huyo jamaa itakuwa Kuna viashiria alikuwa anaviona kwa huyo mke ila alivumilia muda wote akiamini ni mke mwema.....sasa huenda kwenye hivyo viashiria kulikuwa Kuna ukweli....huenda alishakutana hata na baba wa mtoto akiongea na mkewe ila alidanganywa.....MIMI NAMPA KINGOLE HUYO JAMAA,ACHANA NAE MWANAMKE WA NAMNA HIYO
uwezekano huu ni mkubwa! watu wasiangalie tu alimficha mtoto! kuna mengine makubwa!!! huenda hata huyo jamaa alishakuja mpaka nybani kwake!
 
Kwa mtu mwenye akili timamu, rijali, aliyepitia malezi bora ya wazazi wote wawili hawezi kuacha mke aliyeishi nae miaka 15 na kuzaa nae watoto wanne kisa alimficha kua alizaa kabla, hilo ni kosa dogo sana na linazungumzika.....

Na kama mtu hayupo tayari kuzungumza ya nyuma kwanini alazimishwe??? Kila binaadam ana siri yake na maamuzi yake yanapaswa kuheshimiwa, huwezi jua hilo tukio lilimuumiza vipi akaamua kulifukia na kuanza upya.
na kama je baba mtoto aliwahi kumtambulisha kwa mume wa ndoa ni kaka yake?
 
Umeishi na mtu kwa miaka 15, mmezaa watoto 4, unakuja kumuacha kisa hakukwambia kua aliwahi kuzaa kabla!!?

Ukisikia kutafutiana sababu ndio huko sasa.
Huna akili wewe, hiyo ni cheating ya hali ya juu, uongo wa namna hiyo hauvumiliki na hiyo ndoa ni batili kama ni ya kikristo. Yani aondoke zake. Wanawake mnapenda kurahisisha mabaya yenu sana. Sababu ni hiyo hapo ,kwanini amfiche? Ni kumfanya mjinga. Hakuna mwanaume mjinga. Safi kabisa aachane na kahaba hilo litamtia stress tu.
 
Back
Top Bottom