The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Lakini sio kosa la kumuacha Mke, kama mmeishi miaka zaidi ya 18 pamoja ndiyo mje kuachana Uzeeni?
Tumeambiwa tusamehe 7x70
Huyo jamaa walikua wameshachokana, amepata sababu tu ya kumwachia mkewe.
Kingine, angejipa muda wa kutulia na kutafakari, kama amefanya haya maamuzi haraka akiwa na hasira inaweza kuja kimgharimu mbele ya safari na kubadili mambo itakua mchakato mrefu.
Kingine unawezakuta huyo Mama alificha haya mambo akijua analinda ndoa yake matokeo yake mambo yameenda kinyume, inatokea kwenye maisha unawezafanya jambo Kwa Nia nzuri likapokelewa tofauti au matokeo yakawa sio yaliyotarajiwa.
Mwisho, hapa tumepata habari Kwa juu juu tu, Kuna mengi hayajasemwa, inakua ngumu kutoa maamuzi au ushauri Kwa hizi taarifa zilizoletwa. Mfano, huyu Mama alikua anahusikaje na matunzo ya huyo mtoto? Kulikua na mahusiano au mawasiliano ya aina Gani kati ya hao wazazi?
Ukute jamaa aliwahi kuulizia akaambiwa hakuna kitu kama hicho, Sasa akija kubaini lazima awe kifaru.