Ushauri: Nitumie mbinu gani kuongea na baba aachane na mchepuko wake?

Una umri gani? Halafu nitaendelea
 
Una umri gani? Halafu nitaendelea
 
Ushauri nimeupokea mkuu.Kuna shangazi yangu(dadaake baba)nilimdokezea.Kwa kuwa nimtu wa dini Sana alichonijibu nikwamba anafunga nakuomba kwa ajili ya hilo jambo na soon Mungu atatenda muujiza.
@sepema yaani baba yako hakose utamu baada ya maombi ? Kama ni hivyo embu muache mzee ajilie vyake tu.
 
Sijaona tatizo hapo,unaweza kumbana mzee afu wewe kesho ukachepuka.

Wanawake wanatakiwa wakubali kuwa mwanaume hawez kuwa na mwanamke mmoja.

Na kitaalamu huwa wanasema mwanamke ikifikisha miaka 35+ hamu ya tendo inaanza kupungua,sasa kwanini mzee aanze kuhangaika kuomba tunda kwa mtu ambae labda hataki kutoa.

Kitu ambacho sitakagi kabisa kuwaingilia wazee wangu ni kwenye hayo mambo ya kufurahisha miili yao,mwacheni mzee amalizie uzee wake kwa furaha
 
Pole sana ila usimchukue mama yako vaa moyo wa ujasiri muulize huyo mzee wako kuhusu hizo tuhuma usikie atajibu nini lakini ajabu huyo baba mkubwa wako nae hakubali kama anachapiwa ni jambo la ajabu maana ilibdi iwe kesi ya UKOOO hiyo... usikurupuke

Mzee anapiga kimasihara mkuu. Mtoto huwezi kumuuliza baba yako hayo mambo. Vaa kiatu chake
 
Mtoa mada chukua huu ushauri[emoji115]. Nina experience na jambo kama hilo. Usisahau kuvaa kimaafia kama siku unamtimbia huyo mamdogo. Mzura, jacket kubwa, buti, gloves za mikononi zile za sweater halafu sauti kama umekula ndumu na ulikuwa umepania kungawanya vipande ila umensamehe na kumpa chance ajirekebishe mwenyewe. Muwe watu wawili au watatu. Akitoka hapo amejikojolea na mnaweza kumvuta masikio kidogo. Au unaweza kunipa hiyo kazi, tunamweka mtu kati , sie machalii wa chuga huwa haturembeshi. Au ukitaka huyo mshua wako tunamweka kitako na bapa za sime kuwa sisi ni vijana(ndugu) wa huyo mamdogo au mimi nae ni mchepuo wangu na ukituruhusu tunampiga bapa moja tuu kisha tunampa chance atimue mbio
 
[emoji848][emoji848][emoji4][emoji4][emoji4][emoji1787][emoji23]
 
Mwambie vijana wamemchukua video na wanasubiria tu muda muafaka waiweke kwenye mtandao. Siku atakayojiona kwenye mtandao ndiyo atajua mbivu na mbichi.

Mawazo tu ya aina ya mikwara ya kupiga.
 
Angalia namna ya kumfariji mama.... Ila kuingilia mahusiano ya wazaz haina afya sana... Nikuulize tu swali wakiwa huko chumbani hua unakaa nao? Either mtafute mzee mwenye busara wa ukoo au family friend awaite awasuluhishe
 
Ndugu,

Licha ya upendo mkubwa uliyonao kwa mama yako, nikushauri tu hili jambo ni la kuliendea kwa akili na sio mhemko.

Moja; huna mamlaka juu ya mahusiano ya baba yako na huyo mwanamke mwingine, kama ameshindwa kuwasikia na kusitisha mahusiano baada ya kusemwa na mkewe pamoja na ndugu zake, unadhani una nafasi kubwa sana ya kumshawishi huyo mzee?

Mbili; usianzishe chuki na baba yako kwa kuwa tu ana mahusiano nje ya ndoa na kwa namna moja yanamuumiza mama yako. Wewe ni mtoto wa kiume; endelea kutafuta suluhu bila kuharibu mahusiano yao.

Tatu; kamwe usithubutu kumuuliza mzee wako juu ya hayo mahusiano; endelea kutafuta suluhu bila kumuuliza huyo mzee. Hapa ni vyema ukatumia wazee wenzake na sio wewe mtoto aliyekuzaa mwenyewe.

Nne; fanya uchunguzi binafsi juu ya hilo jambo na sio kuamini moja kwa moja maneno ya mama yako; alisema mzee Kikwete ''za kuambiwa changanya na za kwako''

Mwisho ; japo si kwa umuhimu; yaone mahusiano ya baba na mama yako kama mahusiano ya watu binafsi; mapenzi yana mengi; kuna siku watakuja kupatana huku wakipeana huba zito na wewe utabaki unashangaa usijue namna ya kuwatazama.

Nimekueleza haya kutokana na uzoefu mbalimbali.

Uwe na siku njema.
 
Sisi wazee wa zamani tunaelewa kinachoendelea,usidhani hapo baba anachepuka hapana

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app

πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€haya mambo hayana umri kesho wanapatana wanaanza kukuona huna adabuuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…