Ushauri: Nitumie mbinu gani kuongea na baba aachane na mchepuko wake?

Wakuu salaam....

Mara kadhaa mama amekuwa akimtuhumu mzee kujihusisha kimahusiano na mama flani ambae ni shemeji yake. Mama amejaribu kufanya jitihada zakuwaachanisha kwa njia ya mazungumzo lakini wamegoma kuachana kabisa.
Una umri gani? Halafu nitaendelea
 
[emoji23]nimecheka utadhan mazuri.Asante mkuu
 
Haya mambo yanahitaji akili na utulivu; ukileta hisia za kumpigania bi.mkubwa unaharibu sana
Ndo maana me bi mkubwa akisema niongee na mzee inabdi ntulize akili kwanzaa lasivyo mzee lazima mkosane
 
Haya mambo wewe kama mtoto hayakuhusu na ulipaswa kumuambia mama kuwa hayo ni mambo ya mahusiano yenu kati yenu nyie hivyo wajue namna ya kuelewana wao kwao.

Hii tabia ya kuhusisha watoto kwenye masuala ya mahusiano ya kimapenzi baina ya wazazi siyo busara na halipaswi kufanyika.

Mzazi kaa na mzazi mwenzio muone namna ya kuelewana na kila mmoja aeleze kile anachokikosa kwa mwingine ili ajirekebishe na siyo kumuambia mtoto aongee na Baba kuhusu hayo mambo.

Baba yako akikuambia mama yako hamridhishi utamsaidiaje??

Utaenda kuongea na mama pia kuwa amridhishe baba yako kitandani??

Mahusiano kati ya watu wawili yana mambo mengi na mengine mazito, wewe mtoto hayakuhusu maana hata kipindi wanatongozana wewe hukuwepo na hujui mengi kuhusu wao wawili.

Mwambie mama yako hilo suala halikuhusu na waongee wao wamalizane na uendelee na majukumu yako.
 
Unaweza ukafanikiwa kumachanisha mshua na huyo mchepuko wake, halafu mshua akachukua mchepuko mwingine.
Vipi utaendelea na hiyo kazi mpaka lini?
 
Nimepokea
 
Sijui ni Mimi tu yaan mi mtu kuwa na mchepuko naona is not big deal ilmradi anatunza familia tu...Cha kumkumbusha hapo ni kondomu au kupima mara Kwa mara.Maana maradhi nayo ni changamoto yakiingia ndani coz hapo tayari ni rectangle relationship
 
Mkuu mda mwingine huwa nakuelewa sana nataman hii mindset wangekuwa nayo wanawake wote..kikubwa ni kujilinda na maradhi tu

NB:mke/mume asiekua na hofu ya Mungu ni lazima ipo cku atachepuka tu
 
Sijui ni Mimi tu yaan mi mtu kuwa na mchepuko naona is not big deal ilmradi anatunza familia tu...Cha kumkumbusha hapo ni kondomu au kupima mara Kwa mara.Maana maradhi nayo ni changamoto yakiingia ndani coz hapo tayari ni rectangle relationship
Ujue hata mimi hayo mahusiano yamzee na mchepuko wake sikuona Yana shida San cz majority ya wanaume tupo hivyo.Hata hapa kinachonichanganya sio mzee kuchepuka,noo...kinachonisumbua ni jinsi bimkubwa alivyoamua kunishirikisha.
 
Talking about my experience mzee wangu aliwahi kuwa na mchepuko na sisi kama watoto(mimi na kaka yangu) tuliamua kukaa chini na kumuandikia barua mzee kumchimba mkwara kwamba tumeshajua mambo yote na tunamuomba aachane na huyo mchepuko mara moja kabla hatujaamua kufanya maamuzi magumu

Mbinu hii ilisaidia sana kwan tangu kipindi tumeandika hiyo barua hatukuwahi kumuona akipokea tena simu zake wala yeye akimpigia
 
Nakushauri, acha na masuala ya baba na mama yako.Pambana na maisha yako hao ni watu wazima kwani mambo ya ndani ya shuka za wapenzi usijaribu kuingilia.Vinginevyo unatafuta laana ya asubuhi na mapema
 
Alibadilisha mbinu na jiulize wewe hauna mchepuko pamoja na kuwa katika ndoa?
 
Poleni sana, kwenye familia yakishaingia mambo kama haya hata Ile amani inatoweka, too bad mzee wako ameahindwa kucontrol issues zake za Nje, Wadau wamekwambia umwambie kwa utaratibu na hekima ukifika Tu umeharibu fanya hivyo, kama ni mzazi mwelewa basi atajifunza kitu.
 
Ujue hata mimi hayo mahusiano yamzee na mchepuko wake sikuona Yana shida San cz majority ya wanaume tupo hivyo.Hata hapa kinachonichanganya sio mzee kuchepuka,noo...kinachonisumbua ni jinsi bimkubwa alivyoamua kunishirikisha.
Bas anakwepa dharau,msaidie Kwa kumwonya mwanamke huyo wa nje
 
mkuu mda mwingine huwa nakuelewa sana nataman hii mindset wangekuwa nayo wanawake wote..kikubwa ni kujilinda na maradhi tu

NB:mke/mume asiekua na hofu ya Mungu ni lazima ipo cku atachepuka tu
Yeah sure
 
Usijiingize kwenye mambo hayo, usimuulize baba yako ni kumkosea heshima......mama amekosea sana kukushirikisha alitakiwa awashirikishe watu wazima...ikishindikana...amlilie Mungu
 
Ongea na mzee mwambie aache nyege za kitineja acheat kwa akili, afiche michepuko yake....

Nb: usimshauri aache make michepuko inaimarisha ndoa, mwambie tu afanye kwa siri.
Jibu sahihi ni hili. Ila huwa natamani nikuine we mwanamke, UNAFAA SANA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…