Ushauri, niwahusishe watoto wangu wa nje ya ndoa kwenye urithi?

Yah bro
 
Sasa kesi yako na huyu ni tofauti.
Huyu alizaa nje akiwa yupo kwenye ndoa kabisa kaka. Watoto au mtoto uliempata kabla ya ndoa kuwatambulisha sio ngumu kaka.
 
Kama kweli jamaa anawapenda wanae aliozaa nje ya ndoa kamwe asiwatelekeze kwenye mirathi Yake.
Ahakikishe kila mtoto anapata urithi wake ipasavyo
 
Wagawane na mkewe nusu Kwa nusu then mgao wake agawe Kwa watoto wote wa4.
 
Inauma sana yani unatengeneza mali wewe na mmeo afu yanatokea hayo.
Sawa ni mwanae ila daa inauma sana jamani
 
Kama kweli jamaa anawapenda wanae aliozaa nje ya ndoa kamwe asiwatelekeze kwenye mirathi Yake.
Ahakikishe kila mtoto anapata urithi wake ipasavyo
Sawa ndio ila nyie ndo zenu nyie wanaume, mnapanga na wale zenu kuwa mali ni zenu na watoto wenu , baadae yanatokea hivyo inaumiza sana.
 
Wakina mama ukiona mume wako kaja tuu kukwambia anamtoto nje ya ndoa ,

Yani maana yake mahusiano yenu hayajajengwa kwa kuaminiana.

Yani mumeo anakuona kama kinyago tuu hapo home.

Na ni sawa tuu kwa upande mwanaume kwa mkewe.
SIO MTOTO TU,AKIKWAMBIA FLANI NITAMUOA NA USHAHIDI UNAO JUA KABISA WEWE MWANAMKE HUPENDWI NA UKO KAMA TAKATAKA HAPO,KIMBIA
 
Nimekuelewa ila nilichokujibu ni kuwa lazima confession iwepo kwa sababu bila kujali mali ni zake binafsi, lazima wosia umhusishe mke kama shahidi, sasa usipomwambia ukweli mkeo atakubali vipi kushuhudia wosia wako!!
Lengo ni kutoa attention ya kuwa kuna watoto nje... Whether wosia ni valid au sio valid... Watarithi tuu kwa sheria ilivyo sasa
 
awape watoto wake wa ndoa maana hata akiwapa na hao watoto wa nje umoja wa familia hautakuwepo tena. kuzaa nje ya ndoa ni kuisambaratisha familia. mimi naenda zangu
 
Lengo ni kutoa attention ya kuwa kuna watoto nje... Whether wosia ni valid au sio valid... Watarithi tuu kwa sheria ilivyo sasa
Hapana mkuu, as long as jamaa anataka kuandika wosia ni lazima aconfess kww mkewe. Halafu hii ya kusema watarithi kwa sheria ya sasa sio rahisi kihivyo. Watoto kama hawajatambuliwa kwa ukoo (pamoja na mke) hao hawawezi kurithi chochote, mahakama ya Rufani ilishaamua na ikasema kuwa watoto haramu watafurahia maisha na mali za baba yao wakati wa uhai wa baba yao, siku baba akifa, ndio mwisho wa mchezo.
 
Nipe hiyo case ya wazee... Mkuu
 
Nipe hiyo case ya wazee... Mkuu
VIOLET ISHENGOMA KAHANGWA AND JOVIN MUTABUZI vs THE ADMINISTRATOR GENERAL AND MRS. EUDOKIA KAHANGWA [1990] TLR 72(CA)
Walifanya reference kwa kesi ya Kiingereza ya In re Harrington [1908] Ch. 678 where it was held that,

A putative father's obligation under a bastardy or affiliation order ends with his death, that such obligation is personal and the arrears under such an order are not recoverable against his estate.
 
Aache u selfish,,,Kama ana uhakika ni damu yake Wana Haki ya kupata urithi watoto.
Na hii tabia t.ya kuithamini Mali Kama tumehamia duniani sijui hata imekaaje yaani.
 
Mbona kama hii precedent imekuwa overruled na hizi case za Elizabeth mohamed case na Judith Patrick kyamba case
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…