USHAURI: Rais Samia suluhisho pekee kwa Bandari Tanzania ni hili

Hata biashara nyingi za watanzania zinakufa kutokana na hizi tabia za uvivu na wizi za Watanzania!

Mtu unawekeza pesa nyingi kuanzisha biashara unaajiri watu na unawalipa ila wanaishia kukuibia na kukuulia biashara yako
 
Ni ujinga kushindwa kusimamia serikali na kudhani kukabidhi kila kitu kwa wawekezaji ndiyo suluhisho. Huu ni uvivu na uzembe uliovuka mpaka, Kuna nchi nyingi tu zainafanya mambo yao bila kutegemea wawekezaji
Serekali ndio kikwazo cha bandari zetu kufeli angalia bandari kama Durbun inavyofanya kazi vizuri nimefika pale mazingira yake ni kama hii ya Dar wametenga eneo kama kigamboni wafanya biashara wamejengewa yard za kuzia biashara zao wanakodishwa wakiagiza mizigo meli zinashusha kwenye eno walilotengewa kwajili bila kulipia ushuru,wakiuza bidhaa moja nfano godoro wanalipia bidhaa iliyonunuliwa watu wa custom wako kwenye mageti ya kutokea mixigo bila kukilipia ushuru mizigo upitishi pake sio kama hapa kwetu ujuaji mwingi tungefanya kama wenzetu bandari zetu zingetengeneza ajira nyingi sana nchi jirani wasinge agiza mizigo kutoka nje wangenunulia hapa kwetu ukiwa na mtaji kidigo wa kununua mzigo unafanya biashara bila tatizo lakini hapa kwetu kizungumkuti nfanya biashara anaumiza kichwa gharama za manunuzi kusafirisha mzigo kulipia gharama za bandari kulipia ushuru storege akichekewa kidogo mnada unamuhsu akifika mtaani parchising power zero shida tupu tunapelekana mperapera sana nakukomoana ndiomana umasikini ningumu kuisha mwisho utasikia CAG riport yake anakuambia pesa zilizokusanywa zimeibiwa
 
Just imagine wewe ni hicho kimzigo umeagiza kutoka hapo Zanzibar tu

Kuzuia ukiritimba huu ndo mana kuna nchi zingine watumishi wanavaa body camera na inatakiwa kuwa on muda wote ukiwa kazini

Hata akija muwekezaji inabidi ashauriwe kuweka body camera kwa watumishi wake wote wa Bandarini

Hizi body camera pia zivaliwe na watumishi wote wa TRA
 
Siamini katika kuwapa kampuni binafsi kuendesha bandari kwa nchi yetu. Kuna hila zinafanyika ili kufikia lengo kama hilo na wahuni aliyowaingiza samia serikalini.
Kinachotakiwa ni uongozi wa serikali makini na imara usiyoweka maslahi binafsi ya vigogo serikalini.
 
Mwl Nyerere alisema ili nchi iweze kuendelea, inahitaji ardhi, watu, siasa Safi na utawala bora, sasa katika hivi vitu vinne tz imekosa watu.
 
Vyote hivyo vitafeli sababu kuu tatu wizi, rushwa na siasa basi. Njoo na suluhisho ya hivyo vitatu na utapata Tanzania ya 1st world.
 
Tunazunguka mbuyu kwa hoja za kitechnical lakini ukweli ni kwa tatizo LA bandari linatokana na marais hao wenyewewe.
Rais Mwinyi na Mkapa wake zao walipitishia mizigo lukuki pasipo kodi,na kampuni zingine zilitumia mwanya huo kuagiza mizigo kupitia kampuni za familia za hao viongozi.Hivyo,hivyo alichokifanya Kikwete & Magufuli.kwa sasa SAMIA ana cover hizo dili za Kikwete.

Tunawaita Raia namba 1 ndio wanaotuangusha hii Nchi kiufupi hawana uchungu wowote.ndio maana Paul Kagame alituzodoa kwa kusema ukweli.
 
Nimependa mapendekezo yako 1,2&3 yatasaidia kui-decongest Dar port na Dar jiji generally! Privatisation Pia ni mbinu mbadala wasiwasi wangu ni jinsi ya kusimamia mapato ya nchi na maswala ya usalama wa nchi going forward! Big up mkuu[emoji2]
 
Ndugu zanguni, kwanza kabisa tuelewe inaposemwa bandari hafanyi kazi kwa kasi inayotakiwa maana yake ni nini.
Kuna vigezo kadhaa vya kimataifa vinavyopima jambo hili lakini kikubwa kabisa ni kasi ya uingiaji wa meli nchini na kupata gati, kupakua kupakia na kuondoka. Ndio maana kitendo cha meli kukaa nje baharini kusubiria gati linapaka sana matope bandari yetu kimataifa.
Vigezo vingine lakini vyote ni vya kussuport hili la meli.
Sasa jambo la kujiuliza kabla kufikiria Bagamoyo je. Bandari yetu imetekeleza yote yenye kuongeza kasi ya meli kuingia na kutoka??
1. Je shughuli zote za bandari au zihusuzo mizigo zinafanyika masaa 24?? Watanzania bado tunapenda sana kupumzika. Hebu jiulizeni kama huduma za vitengo vyote vihusuzo mizigo kama kweli zipo masaa 24 kama hutakuta ni kule kwenye maji tuu
2. Je, urasimu wa vibali tokea custom, bandarini, TBS... Nk. Imekwisha??
3. Tecnohama inatumika ipasavyo kila kitengo?
4. Kwa nini hadi leo mizigo hazitoki bandarini kutoka kwenye meli moja kwa moja kwenye lorry la mwenye mzigo.. Under hook direct delivery
5. Kwa nini full swing use of Icds haufanyiki. Bandari sio mahali Pa kulundika mizigo
6. Je vifaa bandarini ni vya kisasa na vinatumika effectively

Nadiriki kusema PPP ni mhimu baada ya mageuzi makubwa kuonyeshwa na TICTS jambo ambalo halipashwi kusubiri kwenda gati zingine hata kwa mwekwzaji mwingine ikibidi ili ashindane na Ticts. Pia hadi General cargo vessels hadi kwenye magari

Tunaweza kufungua gati nyingine nyingi lakini mind set zetu zokabaki kufanya kazi kwa mazoea. Bandari na associated partners lazima ziwe kazini masaa 24.
Hakuna haja kufoleni maofisini kutafuta vibali vya kutoa au kuingiza mizigo kupakia.. Let computer do the work
Mizigo inayoweza kubaki bandarini ni Ile maalum au yenye matatizo tuu. Mingine itoke siku inapakuliwa. Malipo yote kabla meli haijafika
 
Hivi bandari ya dar es salaam
Kwa mwaka zinakuja jumla ya vessels
Ngapi?

Ova
 
Tatizo kubwa si watu kutojua kuongoza, la hasha, tatizo ni magodi faza ambao akikuweka na usipotimiza matakwa yake ya kupiga, unatafutiwa visa unaondoka. Unapotimiza matakwa yao na kwa bahati mbaya ukawashika mikono waliokuteua, unaondokea Kisutu.

Yangu macho na masikio.
 
Ishu ni mipango ya wapigaji waliozoea kupiga huwezi wambiaa kitu kinachobana masilahi yao wakakubari never...
 
Weye ndio mwenye mawazo sahihii
 
It is a good idea. Lakini kwasababu ya ufisadi, tunachaguwa wawekezaji wasiokuwa na sifa. Hakuna muwekezaji wa maana atakuja kuwekeza kwenye nchi inayonuka rushwa. Hakuna muwekezaji atakuja kuwekeza kwenye nchi isiyokuwa na (manpower). Hakuna muwekezaji mpenda haki atakuja kuwekeza kwenye nchi yenye sheria mbili, moja ya masikini, na moja ya watu wenye fedha. Muwekezaji mpenda haki kwa wote anakuwa fair kwenye uwekezaji wake, ikiwa pamoja na haki za Watanzania . Nchi inayoongizwa na viongozi mafisadi, Wasio jail sauti za wananchi wawo, na wawekezaji wataingia na dhalau hiyo hiyo, wenye kufanana na viongozi wetu, mwishowe itafeli tu. Ndiyo maana wawekezaji wetu ni watu wenye asili ya kihindi, waarabu na wachina ndiyo wako interested. Tuseme bila kuficha wengi ni wahuni wenye nia ya kuvuna na kuondoka. Wengi ni watu wasiojail maendeleo ya wengine ila wenyewe tu. Na hii sio racism, but it is facts. Kwanza tujenge nidhamu. Tupigane na ufisadi. Sheria moja kwa wot. Siku polisi hataogopa kumukamata mtoto wa Kikwete ama waziri ama mtoto wa Samia basi ujuwe Tanzania itasonga mbele. Kwasababu kila mtu ataheshimu sheria. Kwa sasa tuko mbali sana. Wawejezaji tutakao wapate ni wale wenye nia ya kuchukuwa chawo na kuondoka. Tumedanganywa sana. Tumeibiwa sana. Na watu wanaoitwa WAWEKEZAJI.
 
Hata mwekezaji ambaye tutampa lazima afanyiwe vetting kisawasawa kujua uwezo wake kabla ya kupewa Bandari
 
I can agree with you
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…