Namimi najiwazia hivyo hivyo kwani akigoma kutetewa na kujitetea waamue wenyewe...imeonekana hakuna haki dhahiri...kuna haja Gani ya kupoteza nguvu na muda kujibu mambo yao ya kipumbavu.
Ninachokiona, lisu akitolewa wakati huu...atakuwa maarufu sana na atakuwa anazungumzwa yeye tu Hadi pale uchaguzi utakapoisha..tutasahau kuwa nchi Ina viongozi wakuu...viongozi wa nchi watazidiwa Kila kitu kwa Kila mahali na huyu Bwana..na akiitisha mikutano ndio itakuwa balaa zaidi...uongozi wa nchi una hofu hapa...ndio maana wanajaribu kumsitiri bimkubwa asidhalaulike zaidi kwa muda mrefu
Pili naona baada ya uchaguzi kupita, atakayepewa nchi kuiongoza atapata tabu sana..maana huko duniani wanaona kinachoendelea mahakamani..wanajionea wazi haki haitendeki, wale wawekezaji waliokuwa na lengo la kuja kuwekeza nchi wajipange vizuri...maana wakija kuikosea serikali kesi zikiwa mahakamani wajue nao watakuwa wanahukumiwa hivyo...ndio picha inayoenda duniani huko...wawekezaji wengi wataogopa sana hii nchi....yaani tumetupa taulo tupo uchi wanatucheka tu tumeshindwa kujifanyia usafi hekalu letu...
Ni aibu, lisu angekubali kujitoa zaidi awe sadaka...asitetewe na yeyote na asijiteteee ili dhamila yao itimie yaishe...tumeaibika taifa Zima...tunaonekana matahila wote