Sidhani kama upo sahihi, naamini labda huenda wewe binafsi katika maisha yako ya hapa duniani kamwe haujawahi kukumbana na dhahama za udhalimu na dhuluma za kiutawala za kuwahi kutotendewa HAKI na Watawala. Endapo kama ungewahi nadhani usingeweza kuandika hicho ulichoandika hapa. Tambua tu ya kwamba Wapo Watu wengi sana katika Nchi hii wameshawahi kuumizwa vibaya sana, Wananchi hao wanaishi huku wamebeba maumivu makubwa na makali Sana mioyoni mwao. Watu hao wamekuwa wakiungulika ndani kwa ndani kwenye mioyo yao, na hawana mahali pa kwenda ili kuweza kupunguza maumivu yao waliyonayo Wala hakuna njia yoyote ile ya kuweza kupunguza maumivu hayo waliyonayo.
Kwa taarifa yako, yule marehemu Hamza Mohammed wa tukio la pale Daraja la Sealander Dsm kamwe hakuwahi kuugua kichaa katika enzi za uhai wake! Endapo kama huyo marehemu Hamza Mohammed angeamua kukaa kimya Kama Watu wengine ambao wamewahi kufanyiwa udhalimu mbaya wa namna ile, badi naamini kwamba hadi leo hii mtu huyo angekuwa bado yupo hai uraiani huku akiendelea kuishi maisha yake yaliyojaa maumivu tele kwenye moyo wake kutokana na kitendo hicho kiovu alivyofanyiwa na wale Watu aliopambana nao pale kwenye Daraja la Sealander. Aidha, hata sisi Wananchi wa kawaida tusingeweza kujua kwamba mtu huyo amewahi kufanyiwa udhalimu mbaya Sana wa namna hiyo.