Ushauri: Tundu Lissu usihudhurie Interview nyingine itakayopangwa na WASAFI FM

Ushauri: Tundu Lissu usihudhurie Interview nyingine itakayopangwa na WASAFI FM

Wakulaumiswa nihao walioisitisha shughuli ya kumhoji Lissu. Aibu sana kutumia nguvu ya Dola kuzuia jambo halali nahisi inadhihirisha jinsi wanavyoogopa kwakuwa wanajua hawatoweza kuzijibu hoja zake!!!
 
View attachment 2896938

Baada ya leo kushindikana kwa Mahojiano yaliyopangwa kufanyika kwenye Studio za Wasafi FM , Baina ya Watangazaji wa kituo hicho na Tundu Lissu , imekubaliwa kwamba itapangwa siku nyingine kwa ajili ya jambo hilo

Ukweli ni kwamba Sababu zilizotolewa na Wasafi media kama utetezi wa mkanganyiko huo hazitoshi hata Chembe , na baada ya uchunguzi wetu tumeanza mara moja kutilia mashaka jambo hili iwapo litafanyika wakati mwingine .

Sababu kuu iliyotolewa na Wasafi Media ni kwamba HAWAKUJIPANGA , mahojiano muitishe nyie halafu mnasema hamkujipanga ! mwataka kujipangaje , ili iweje ?

Ushauri wetu kwa Tundu Lissu asithubutu kuhudhuria mahojiano mengine kwenye studio hiyo , au kama ni lazima ahudhurie basi ni muhimu na ni lazima aende na mic yake pamoja na kiti chake , hii ni kwa sababu za kiusalama .

Naomba kuwasilisha .
sio lazima na wala sio muhimu...
 
Sasa kama hizi media za ndani zinaogopa wafanyeje? au ndio wawalazimishe kama Lissu alivyogoma kuondoka hapo ofisini kwa WASAFI mpaka wamwambie nani kawatuma kuzuia interview yake?

Siku zote ukweli hujitenga na propaganda bwashee, ukiusema hata kama ni kwa media yako wanaojielewa watauelewa na kuuamini, wasiokubali watakuwa ni wale wafia vyama wasiotaka kusikia jema lolote toka kwa upande wa pili.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Aende Star tv, Diallo anajitambua!
 
wazee wa kususa

mambo hayaendi namna hiyo rafiki zangu wa chadema
 
Dawa ni kutoisikiliza na kuotazama tena WCB.

Bias kwenye eneo ambalo hupaswi kuweka upendeleo ni eviction ticket.

Wanaenda kuporomoka
Kwamba Wasafi waporomoke kisa kutomuhoji Lissu?
 
Lisu naye ataendaje wasafi fm wakati anajuwa fika hao ni ccm machawa.

Kwanza wasafi wanamuandishi gani wa kumhoji lissu/kufanya naye mahojiano

Wale wasafi habari zao zinajulikana ni umbea udaku tu

Ova
 
Kama tungekuwa na akili kisoda kama unavyodhani unadhani tungeleta uzi huu hapa ? , hatuandiki kibwege
hamna cha kufanya sasa ni lazima mgeleta uzi coz you have limited altenatives....

kokote pale muendako mnabuma na 2025 hiyo apo kwa kona ya moise katumbi yanawafuata kwa karibu sana 😀
 
Tahadhari ya nini?Mnapenda yellow journalism na uzushi wa kijinga.Kuhusu Lisu yeye ndiye ana hiari ya kuhojiwa au kutohojiwa kwa kuangalia faida na hasara. Na hayo madai yako mengine ni ukichaa ambao sistahili kukujibu.Unataka ujibiwe paranoia?
Wewe ndio upunguze kiherehere.unaangaika nini na maisha ya mtu anapopewa tahadhari juu ya maisha yake.jinga kabisa wewe.
 
Dawa ni kutoisikiliza na kuotazama tena WCB.

Bias kwenye eneo ambalo hupaswi kuweka upendeleo ni eviction ticket.

Wanaenda kuporomoka
Nimekuuliza wasafi wataanguka sababu ya kutomuhoji Lissu si kituko hicho? Jibu hoja acha kuruka ruka kisanii
 
Back
Top Bottom