Ushauri wangu kwa vijana wa kidato cha 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya Chuo Kikuu

Vipimo kati ya elbow moja na nyingine hapo ni universal havibadiliki.

Hiyo ni shower hapo kuna elbow ya maji moto naya maji baridi. Kikawaida kutoka centre ya elbow moja hadi nyingine ni 15 cm kokote uendapo duniani haibadiliki
Nija nyingine mwanzo mwa elbow ya kwanza mpaka ya pili ni cm 18 au center to center kati ya elbow na elbow ni inch 6
 
Yes wale jamaa naona wanafundishwa mamichoro tu mara nyingi wanacheza na program za computer kuchora ramani za nyumba huo mda wa kushika konobao sijui koleo mwiko atautoa wapi?
Nenda kampuni za ujenzi kutoka nchi za nje injinia anajua kujenga kushika mwiko inshort ni fundi kamili lakini kwetu ni tofauti sana
 
Yes ndicho ninachokisema, lakini hayo masomo ya kukusaidia mbeleni ndio hayo yawe ya ufundi wa VETA iwe option lakini kwa wanafunzi wanaopenda.
Shida ni moja Veta wana kwenda kwa level na kule mwisho ni level 3 ina maana ina masomo ya sceince kama hesabu,egineering scince ambayo ni kama physics so kwa mtu aliye kimbia masomo ya science kwake bado itakuwa mtihani
 
Nitakuwa wa mwisho katika watu zaidi ya bilioni 7 waliopo duniani kukubaliana na hii hoja ya mleta uzi. Kusema vijana waache kwenda kusoma degree ili waende VETA kwanza ni ufinyu wa fikra na kukata tamaa. Ni sawa na wale wanaosema hela sio kila kitu huku hawajawahi zishika za kutosha. DEGREE NI MUHIMU KULIKO CHETI CHA VETA. Degree itakusaidia kufika ambako mtu wa VETA hawezi fika.

Tusipotoshane kwamba degree haina maana. Kama kwa nchi maskini kama yetu degree haitakuwa na maana basi huko Ulaya na kwingine kulikoendelea inabidi wafunge tu vyuo. Bado kwa nchi yetu tunahitaji wasomi wengi. Haya mabadiliko tunayoyataka yatapatikana haraka kukiwa na wasomi wengi. Kijana mwenye ndoto za kuwa daktari bingwa aache kwenda MUHAS ajiunge VETA? Aisee acheni kukata tamaa. Kama wewe bado maisha hayajakaa vizuri usitake kupotosha vijana. Zamu yako ikifika hata wewe utafanikiwa.

NINAWASIHI VIJANA WAUPUUZE HUU UZI NA KUCHANGAMKIA DEGREE HUKO UDSM, MUHAS, SOKOINE, SAUT na vyuo vingine vinavyotoa degree. Ila pia wasiridhike na degree peke yake. Wajiongeze na maarifa mengine.
 
Serikali haina budi kuueleza huu ukweli kwa Wananchi wake.
 
Shida ni moja Veta wana kwenda kwa level na kule mwisho ni level 3 ina maana ina masomo ya sceince kama hesabu,egineering scince ambayo ni kama physics so kwa mtu aliye kimbia masomo ya science kwake bado itakuwa mtihani
Sijakuelewa mkuu, courses zote zinazotolewa na Veta zina science content ndani yake? Fafanua please
 
Sasa hapo itategemea na maamuzi ya wizara husika ingawa sio suala baya ingawa linahitaji mchakato wa mda,
Hili nalo wakalitazameβ€¦πŸ˜ŽπŸ˜€

Kama wameshindwa kuincorporate ujuzi kwenye syllabus za hizo degree , basi watoe additional classes za ufundi …

I guess vijana wakiambiwa what to expect Huku mtaani, watachukulia positive hizo opportunities za masomo ya ufundi
 
Mkuu Mr kucha man sawa anamake hela..
housemaid uarabuni achana nao ile sio kazi labda wawe tofauti na hao niliowaskia mimi..nina evidence ni unyanyasaji tu majamaa wa uarabuni wanao.sio case moja.ila moja ni close kabisa ndugu wa damu.aliapa hatarudi tena huko.Wana ROHO MBAYA sana.
 
Yeah ni kweli
 
Ushauri muhimu sana kwa vijana wetu
 
Ndivyo ilivyo kwa hakika
 
Sijakuelewa mkuu, courses zote zinazotolewa na Veta zina science content ndani yake? Fafanua please
Kozi za mda mrefu nyingi zina masomo ya science
Ushonaji
Magari
Bomba
Umeme
Uchomereaji
Ujenzi

Fani chache ambazo najua hazina masomo ya acience ni mifugo na upishi

Masomo ya scince ambayo yana somwa kama somo ni engineering scince hili somo ni physics kwa upande wa secondary kuna math ni ya kidato 1 kwanza mpaka 4 na mwisho Technical drawing hili lina patika chuo kikuu kwa wanao chukua engineering
 
Elimu ya Tz inahitaji mabadiliko makubwa mno sababu asilimia kubwa imebase kwenye kukariri karibia levo zote , kwenye mitaala vitu vingine vipi lakini havina umuhimu wala msingi , sehemu kunaweza kuwepo mafunzo ya kwa vitendo lakini vitendea kazi ni duni na vichache kucompare na idadi ya wanafunzi..
 
Kila sehemu ni matobo matobo tu yamejaa
 
Pesa ndiyo elimu.

Huna pesa huna elimu.
Binafsi nashukuru sana Mungu kunipa ujasiri waakuacha chuo semister ya pili mwaka wa tatu.
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ Mkuu usitutanie bhana
 
Niliutambua ukweli huu baada ya kumaliza chuo na kukaa mtaani kwa miaka miwili bila ajira hadi pale rafiki yangu aliponishika mkono na kuanza kupata tumaini jipya.Mungu akubariki rafiki yangu sina cha kukulipa ila nakuombea kwa Mungu akupe baraka katika maisha yako.
Kuna haja kubwa ya kuzingatia ujumbe wako mkuu japokuwa siyo dhambi kuitafuta degree.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…